Hili la baraza kusahihisha upya mitihani ya kidato cha nne 2012 vipi!

KUGS

Member
Joined
Mar 28, 2013
Posts
45
Reaction score
9
Habari wadau wa Elimu! Tangu siku ya leo ianze moja ya habari zilizoenea mtaani ni kuhusu ufutwaji wa matokeo ya kidato cha nne 2012 ambayo tume iliyoundwa na Waziri mkuu kubaini sababu za kufeli na kutoa mapendekezo ya nn kifanyike imeshakamilisha kazi yake, baada ya taarifa yao serikali imeamuru baraza kufuta matokeo na kusahihisha mitihani upya kwa kujitetea na kutoa sababu lukuki likiwemo la upangaji wa madaraja, yapo mambo kadhaa ninayojiuliza kama kweli yaweza kuwa suluhu ya janga hili katika Elimu;
1:Hivi baraza la mitihani ni akina nani? hiki si kitengo tu katika Wizara ndani ya serikali hiyohiyo! kama ndiyo walikuwa wapi kustuka kwa hili kabla ya matokeo? au kwa kuwa waliofelishwa ni wengi kuliko miaka mingine, na vipi kwa waliofelishwa miaka mingine kwa taratibu zenu binafsi maana kuna wahanga wa hili wengi sana na bado wapo mtaani na wengine wanaendelea kutafuta Credit kwa kufanyiwa maksudi haya. au mpo kibiashara kwa malipo ya ada za mitihani?
2:Kufuta matokeo na kusahihisha upya ndo litaondoa tatizo la Elimu nchini? au mnakwepa hoja za wapinzani


Tatizo si kusahihisha upya wala madaraja, ni Mfumo mbovu wa mitaala ya Elimu,uduni wa maslahi kwa Walimu, miundombinu mibovu ya Elimu Tanzania,ukosefu wa walimu na kushuka kwa maadili.
 

nakuunga mkono mkuu kwa hoja zako
 
zipo sababu nyingi za kimsingi zilizoibuliwa na wabunge wa chadema na hili suala la mapungufu ya baraza la mitihani mheshimiwa nasari alipeleka hoja binafsi bungeni lakini ikawa rejected bila sababu za msingi na pia necta ni taasisi iliyopo chini ya uangalizi wa wizara ya elimu na wao wana implement yale waliyoagizwa na wizara husika katika evaluation sasa ni kitu gani gvt inataka kuwaambia wananchi ina maana hawashauriani kabla ya kufanya maamuzi kama haya waliyajua tangu mwanzo kwanini walitangaza matokeo bila kufanya marekebisho na je vip kuhusu maisha ya wale vijana waliokufa kutokana na uzembe huu na vip kuhusu wale waliokata rufaa na pia wale waliojiandikisha kufanya mitihani upya.politics is a dirty game ccm mnatupeleka wapi mnafanya kazi ya kuwatetea majambazi na wakosefu lakini naamini mungu yu pamoja nasi na atazidi kuwaumbua mpaka mkome.poleni sana wadogo zangu mlioathirika kwa makosa ya hawa waiba vyeti akina hamimu aka mulugo na wenzake Tanzania ni muungano wa visiwa vya pemba na zimbabwe .
 
Tatizo si kusahihisha upya wala madaraja, ni Mfumo mbovu wa mitaala ya Elimu,uduni wa maslahi kwa Walimu, miundombinu mibovu ya Elimu Tanzania,ukosefu wa walimu na kushuka kwa maadili.[/B][/I]

samahan kama ntakukwaza but akili yako haujaishughulisha vya kutosha?
umesema tatizo sio usahihishaji wala madaraja hapo umetafakari nini?
Kama tatizo sio hayo yaliyotajwa kwanini ulinganishe matokeo hayo na ya miaka mingine?
hayo mamtaala ndo madude gani?
Miaka ya nyuma walitumia mtaala upi?
Hiyo miundombinu mibovu,inamaana waliomaliza zamani madarasa yao yalikuwa na ac?
kwaiyo wakitoa mtaala mpya ndo wanafunzi watapata 100% wote?
Kila mtu apewe haki yake anayostahili co kufelisha watu ili baadae tuchague jamaa zetu kwenye tume za kuchunguza matokeo

Siasa ni mchezo mchafu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…