Hili la BoT na akiba ya dhahabu ni kazi kweli kweli

View attachment 3538624

View attachment 3538627

Tuishi na nani hapa?! Hii nchi tunazungushwa mpaka tunasikia kizunguzungu halafu wanatuacha.

Fedha za miradi kwa kawaida zinatokana na mikopo na unapokopa unaeleza kwa mchanganuo jinsi huo mkopo utakavyotumika kutekeleza mradi husika. Ni baada ya mkopeshaji kuridhika na feasibility ya mradi husika ndipo disbursement hufanyika. Je ununuzi wa dhahabu kutumia hizo fedha za miradi ulikuwa katika michanganuo iliyotumika kupata mikopo?
Mikopo huwa designated in foreign currency na kama kweli serikali ilitaka kununua dhahabu hapa hapa nchini kwanini itumie forex badala ya local currency? Maelezo ya kuwa wanauza dhahabu ili kurudisha fedha za miradi walizotumia kununua dhahabu hayajitoshelezi!! Serikali inajikanyaga na hiyo ni ishara kuwa kuna kitu nyuma ya pazia wanachotuficha wananchi!
 
Hapo ni kujichanganya Tu, ndio mambo yetu hayo. Unaweza kukuta kwenye Taasisi ya serikali mkurugenzi anatoa maelekezo Haya na wakuu wa idara nao Wana maelezo Yao yaani vurugu tupu basi ilimradi Tu Kila mtu apate mshahara, hii ndiyo maana halisi ya nchi kupatwa na kiwewe.
 
Wanaweweseka balaa, hii ishu ilivuja, hawakutegemea. Walitaka kuiuza kimya kimya. Sasa kuikanusha wanaweweseka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…