Hili la Idris Sultan limewaacha wasanii wa Tanzania uchi wa mnyama

Lord Diplock MR

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2015
Posts
1,393
Reaction score
3,237
Je idris Sultan ni jambazi la kutumia silaha? Je ni gaidi? Ni alshababu au alkaida? Na je jambazi hana ndugu na jamaa? Hana ndugu wanaompenda na yeye anawapenda? Je gaidi wa alkaida hana ndugu na jamaa? Alishababu hawana watoto? Mbona amekuwa mpweke hivi? Mbona wasanii wenzake wamemwacha? Mbona hawakujitokeza hata kumpa pole siyo lazima wapost basi si wangehudhuria tu hata mahakamani?

Hivi wasanii wa Tanzania mtamjali nani akipata tatizo? Mtaamka na kupaza sauti nani akiwa matatani kama msanii mwenzenu anapata shida nyie mnajifungia ndani mnawaachia wanaharakati wa Twitter wamtetee?

Kiukweli kwa hili limewavua nguo sana wasanii wa Tanzania na mnaonesha ni jinsi gani msivyopendana huu ni udhaifu mkubwa sana kwa kweli.
 
Mjini ni washikaji wa kula bata tu,

Ukipata shida jua ni wewe na mke wako, kama huna mke basi utajuta.

Mkeo na wanao ndio watakaokujali na kukuzika

Wengine watakuja kuangalia "hivi hili jamaa limejengwa hata kibanda au alikuwa anavimba na mademu tu hapa mjini "
 
MOSI; Asilimia 99 ya wasanii wa bongo ni CCM, hii ni kwa Bongo movies na Bongo flava... Kwa hiyo wengi wanahofu ya kuhoji, kutetea au kuonyesha msimamo wao hadharani kwa kujua watawatibua au kuwachukiza wakubwa wao chamani... wote tunajua wasanii wana nguvu kubwa kwenye jamii, ikitokea wakaungana na kumtetea Idris unafikiri wataeleweka vipi mkuu kwa wakubwa zao. Ndio maana hata wanaojitahidi kuonyesha kujali bado wanafanya kwa uoga na hofu.

PILI; Wasanii wengine pia walikuwa wanachukizwa au walichukizwa na aina ya uchekeshaji wa Idris toka mwanzoni kabla ya hili la juzi. Ulitegemea wataweza kusimama upande wake kweli?
 
Tatizo kalitafuta makusudi kosa iloilo unalirudia huo ni ukosefu wa akili kama lingekua kosa la kwanza watu wangempigia kelele lakin kosa analifanya makusudi tena analiruda tena kumdhihaki raisi tena kipindi cha kampeni kinakuja nani yupo tayari kutetea ujinga wake hata kama ingekua wewe mtoa mada usinge kubali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wasanii wa Tanzania hawana umoja,,kila mtu anajali tumbo lake tu,kasoro lady jaydee tu
 
Una ushahidi wowote wa Kitakwimu kwamba 99% ya wasanii wa bongo ni CCM?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo jamaa ndio ni mrefu na ana ndevu ns v*zi ila sasa ana akili za kitoto, yani ni kama ana balehe hivi bado hajawa mtu nzima.

Post yake ya mwisho kapost yupo bafuni sijui kashika sabuni ya kuogea kaandika house girl wake analalamika sabuni zinsisha haraka yeye kasema ananawa sana mikono, yaani kamaanisha sabuni inaisha kwasababu ya kupigia punyeto......pasipo na shaka kijana bado hajamaliza kubalehe, ni mtoto mwenye umaarufu unaomsumbua.

Naona afungwe mwaka hivi akili zitarudi, watu hata hawajui anawacheka cheka tu,
 
Bongo celebrities wanashirikiana kwenye misiba, bata, insta na kwenye kampeni
 
Ko
Kosa gani?
 
Mkuu umegeneralize sana.
Lady Jaydee alikuwepo.
 
Usitake kusema hata WEMA SEPETU hajamjulia Hali?
 
Kwaio msanii akikamatwa wasanii wote wajazane maakaman? Pia inategemea na jina la msanii angekua diamond kiba au harmonize wema lazima wangekua na watu wamekuja mahakaman Ila idrisa bado ndogo Sana

Pia sote tunajua kua Idris kakosea so mnataka wasanii waende pale ili waonekane wanabarik ujinga Wake?
 
kuna wimbo wa abiudi siku ya mateso yangu nani atanitazama?,,
 
Mkuu jifunze kuandika ndio urudi hapa.
 
Sababu ni hiyo ya kwanza.
 
Uchaguzi mkuu umekaribia, wasanii hutumika na kupiga hela kwenye kampeni.... kusimama na Idris hadharani ni kupinga juhudi na kujikosesha michongo.
 
Hao ni kaka watoto wa bibimdogo na bimkubwa, hufarijiana kwa nadra ukitokea msiba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…