TheChoji
JF-Expert Member
- Apr 14, 2009
- 5,771
- 17,849
Nianze kwa kuipongeza serikali na mamlaka husika kwa kutilia mkazo suala la kuweka vifaa vya kunawia mikono karibu katika maeneo yote ambayo watu wanaingia. Utekelezaji wa hili umekua mkubwa na kwa sasa maeneo mengi sana wameweka vifaa vya kunawia mikono.
Kilichofanya niandike uzi huu, ni observations zangu binafsi juu ya jinsi watu wanavyochukulia zoezi hili la kunawa mikono.
1. Watu wengi wananawa mikono kama ushahidi tu kwamba wamenawa ili wasisumbuliwe na walinzi au wahusika wa sehemu wanazoingia. Yaani mtu anasimama pale kwenye ndoo, anafungua vimaji kidogo na kujipakapaka vidoleni kisha anafunga maji na kuondoka.
Kulingana na wataalamu wa WHO, unatakiwa unawe mikono kwa ANGALAU SEKUNDE 20 huku ukihakikisha umesugua sehemu zote mbele, nyuma ya viganja na katikati ya vidole na kama una kucha pia usafishe ndani ya kucha. Hili naona kwa wengi bado halijaeleweka
2. Wengi tunazingatia kunawa mikono WAKATI WA KUINGIA sehemu mbalimbali, lakini si wakati wa kutoka! Ukisimama nje ya maduka makubwa, supermarkets nk utaona idadi kubwa ya watu wakinawa mikono ili waingie humo ndani. Cha ajabu wakati wa kutoka, kila mtu ananyoosha njia kuelekea anakoelekea bila kunawa tena! Wataalamu wanashauri kunawa wakati wa kuingia na kutoka sehemu za mikusanyiko.
3. Kujifuta mikono baada ya kunawa. Wataalamu wanasema mikono yenye majimaji ni rahisi zaidi kunasa vijidudu kuliko mikono mikavu. Hili la kujifuta ni kama halipo katika maeneo mengi nadhani ni kutokana na gharama ya tissue. Kama vipi beba tissue zako/anjifu za kujifutia mara unaponawa.
4. Wengi sasa tunadhani kunawa mikono ndio kinga pekee ya kupata corona. Kwamba ilimradi umeshanawa mikono mlangoni, basi humo ndani mnaweza "kujiachia" mpendavyo, kukusanyika, kukumbatiana, kupiga makelele nk. Hili utaliona sana kwenye sehemu kama bar, hotelini na kwenye maduka. Wataalamu wanatuambia kwamba pamoja na kunawa mikono, pia tuhakikishe tunakaa mbalimbali (at least 1 meter) kati ya mtu na mtu iwe ni kwenye foleni, mezani, kaunta nk. Pia kuongea, kucheka, kupayuka nk kunaweza kutawanya virusi hewani.
5. Pamoja na kunawa mikono, nadhani ni muhimu sana kwa baadhi ya wafanyakazi hasa wale wanaokutana na watu wengi walazimike kuvaa mask. Hawa ni pamoja na wafanyakazi wa benki, supermarkets, maduka makubwa, maduka ya dawa, wahudumu wa hoteli/bar/migahawa, madereva bajaji/bodaboda, makondakta wa mabasi/daladala, madaktari, manesi, wakatishaji ticket za mabasi, wanaokusanya ushuru wa parking, na wengine walio kwenye mazingira hatarishi kama hayo.