Hili la NBC Je Huu si Udini Jamani?

Hivi hujui au huelewi kuwa 'Islamic Banking' ni product ?
Hiyo ni product kama ile ya Posta ya 'WADU' yaani weka akiba daima kadiri unavyopata ! sasa kama 'ukatoliki' ni 'product' washauri NBC waweke/wauze !
 
Mchana mwema Mh.EH, Nyongeza na utitiri wa mjadala wetu tafadhali naomba tuupe pumzi ndefu na kifua kikubwa ili tuhimili
hisia na jazba za washiriki humu. Cha zaidi kwenye biashara kuna mbinu fulani hivi; wekeza 1000 ukirudisha 900 na ukiendelea kupata kwa mfumo huo basi 900 zitazaa na kukuza kipato endelevu, Sasa NBC itagharamia mfano Dola efu kumi ($10,000) Lakini watakao jiunga na kufungua accounti hapo wataingiza maradufu au zaidi. Sasa kipato hicho benki itaweza kulipa kodi ya mapato kwa serikali na kunyanyua mzunguko mzima wa ukopeshaji na wengi kufaidika hata ambao huridhika na RIBA (interest). yote hayo Benki inalenga fedha zilizomo mafichoni na manyumbani ambao baaadhi ya waisilamu hawahusiani na mabenki kibiashara.. Zaidi Pesa/fedha haina Dini !!
 
hapo mwisho wa maelezo yako ndio umesomeka ! ni shida yako imejulikana !
kumbe ulikuwa unataka viashiria vya kikatolikikatoliki hivii !
 
Waislamu waanzaishe benki yao ndo waweke masharti kama haya!! Ila sii benki za umma za watu wote!

Hii haina tofauti na mahakama ya Kadhi!

Kwa nini watu walazimishwe huduma za benki ya Immani wao wasiyoitaka??

What is the logic??
 
Ndg yangu ni bora ungeisoma tu hii mada kuliko kuitolea maelezo sababu unaonekana upo kama Serikali ya Tanzania!!!
 
Waislamu waanzaishe benki yao ndo waweke masharti kama haya!! Ila sii benki za umma za watu wote!

Hii haina tofauti na mahakama ya Kadhi!

Kwa nini watu walazimishwe huduma za benki ya Immani wao wasiyoitaka??

What is the logic??

Yaani na wewe eti umenena kitu fulani!!
Unajua maana ya islamic bank wewe.??
Na unafahamu maana ya mahakama??

Basi unakurupuka tu ukaamua kujiandikia maneno. Halafu unauliza: "what is logic"

You should show some logic in you statement before asking others about their logic!.
Sio unaandika vitu ambavyo maana huijui halafu. Unajipiga kofi mwenyewe!

Pata elimu japo kidogo kwa unayoyaandika. Manake unaweza kuja adhirika siku moja!
 
Kumbe ndo kinachowauma............' mnaona uchungu na waislamu nao kuendelea.......kumbe ni hilo tuuu. Pole sans!!!!
 
Yaani mtu roho inamuuma kuona alama ya uislamu katika makaratasi tu....Hivi ukisafiri kwenda uarabuni (kule wakristo wengi wanakofuataga bidhaa) huwa wanaugua kabisa!!!! Maana kila kitu kina nembo ya uislamu kule kuanzia viza, risiti mpaka muhuri....
Lakini mnaouchukia uislamu msijali sana....kuna andiko katika korani linasema kama huupendi uislamu chukua kamba ukajinyonge....
 
hapo mwisho wa maelezo yako ndio umesomeka ! ni shida yako imejulikana !
kumbe ulikuwa unataka viashiria vya kikatolikikatoliki hivii !

Mburula Yule achana naye .. anawivu tu ..
 
kwa walio wengi kazi ya benki ni kuwatunzia hela yao kwa mda mfupi tu, sana sana wiki moja baada ya mshahara kutoka, kwa upande wangu mimi vyovyote ambavyo NBC wanavyofanya wafanye ilimradi tu hela yangu haiathiriki, basi..
 
Waislamu waanzaishe benki yao ndo waweke masharti kama haya!! Ila sii benki za umma za watu wote!

Hii haina tofauti na mahakama ya Kadhi!

Kwa nini watu walazimishwe huduma za benki ya Immani wao wasiyoitaka??

What is the logic??

.......una uhakika watu wamelezimishwa ? .....au umeingia humu kuropoka tu !:heh:
 
Waislamu waanzaishe benki yao ndo waweke masharti kama haya!! Ila sii benki za umma za watu wote!

Hii haina tofauti na mahakama ya Kadhi!

Kwa nini watu walazimishwe huduma za benki ya Immani wao wasiyoitaka??

What is the logic??
jioni njema Mzalendofeki; nakujulisha kuwa Waisilamu hawakuweka masharti wala hawakulazimisha kitu hapa , ila Benki ndiyo inawalenga na kuwatongoza wawekeza na kuingiza mali zao kuBenki. Miaka mingi Waisilamu wanashirikiana na Mabenki ya kila aina LAKINI huwa hawachukui RIBA (interests)za rasilimali yao..... Kwa kifupi hakuna aliyelalamika wafanyaBiashara wengi ni waiisilamu na wenye Rasilimali nyingi ni waisilamu kwa idadi yao kubwa NBC imejipendekeza kuwapiku na kuwaLaghai ili watawapa ZAWADI ya gharama za safari ya HIJA huko MAKKAH endapo wataendelea kuchangia kibiashara na BENKI yao. Sasa hapo ni HIAYARI kuna waisilamu hawata chukuwa hiyo zawadi na wapo watakayo chukuwa na kuibadilisha wapendavyo. Kwa upande wa sio waisilamu hapatakuwepo hasara yeyote au UPUNGUFU wa aina yeyote huo ni ujanja wa SOKO la mabenki naTAASISI za RASILIMALI.. Wote Tutaendelea kutumia BENKI zetu nchini TZ. tuweze kukuza uchumi kwa njia ya kisasa. kila la heri kwa wote
 
Islamic banking ni product ya nbc na benk nyingineduniani ambayo inafuata sheria za kiislamu.product hii ni kwa mteja yeyote.na ulaya wateja wengi ni wakristo.benki nyingi duniani sasa hivi zinajikita sana kwenye product za kiislaam kwa kuwa risk ya kupoteza pesa zao ni ndogo.hapa benki haiangalii dini inaangalia ni wapi wapeleke zaidi mtaji wao kwa ajili ya usalama na faida kubwa.
 
NA je CRDB kuwamwagia mapesa wakatoliki kujenga kitega uchumi pale Msasani huoni huo nao ni udini? Acheni uchochezi nyie! wakifanyiwa maprotestants ni sawa waislamu udini?! mna kazi kweli kweli !

Mleta mada ana uelewa mdogo na Islamic Banking, NBC wako sahihi. Lakini hata wewe pia una uelewa mdogo, wakatoliki WAMEKOPA WATAREJESHA, WANAIPA FAIDA BENKI!
 
Islamic Banking ina faida gani kubwa kwa benki? Tuchanue kidogo mkuu.
 
Waislamu waanzaishe benki yao ndo waweke masharti kama haya!! Ila sii benki za umma za watu wote!

Hii haina tofauti na mahakama ya Kadhi!

Kwa nini watu walazimishwe huduma za benki ya Immani wao wasiyoitaka??

What is the logic??

Mkuu, hakuna anayelazimishwa. Lakini huduma hii inanivutia hata mimi Mkristo, hasa suala la kukopa bila riba.
 
Islamic Banking ina faida gani kubwa kwa benki? Tuchanue kidogo mkuu.
Wandugu; Iligundulika na kutambulika Islamic Banking ilipo savivu mwaka 2008/2009/2010 palipotokea Financial crisis ulimwenguni(Poromoko na mgogoro wa Rasilimali) kwakuwa Isl-banking hutumia mfumo HALALI wa "murabaha'na open transperncey schemes Mbadala wa kibiashara bila kutegemea Riba(interest) hayo yaliProve kuihami na kuilinda msingi wa Rasilimali. Hapo ndipo western banks wakakubali na kuridhika kuwa kuna USALAMA wa mfumo huo. zaidi pita NBC upate majibu.
 
hapo mwisho wa maelezo yako ndio umesomeka ! ni shida yako imejulikana !
kumbe ulikuwa unataka viashiria vya kikatolikikatoliki hivii !

Nenda tawi lolote la MCB, huwezi kupata viashiria vya aina yoyote vya Ukatoliki. Well nilichokisoma hapa ni kuwa "ISLAM" is but a marketing product.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…