Hili la Ngorongoro halijaisha, tumefunika kombe

Mzee Rufiji

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2024
Posts
261
Reaction score
395
Ili Tanzania tupate maendeleo ya kweli ambayo ni endelevu, ni lazima tujifunze kuukubali ukweli halisi jinsi ulivyo na kukitokea tatizo, tukabiliane nao kwa kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa tatizo hilo na sio kufunika kombe mwanaharamu apite.

Ngorongoro kuna tatizo, Serikali ilitaka kulitatua kibabe, Wamasai wakagoma, alichofanya Rais Samia Suluhu Hassan ni kufunika kombe tu, lakini tatizo bado lipo na linahitaji ufumbuzi wa kudumu ili tuendelee kuwa na Ngorongoro yenye maendeleo endelevu.

Kufuatia hali ya Ngorongoro ilivyokuwa tete, jambo la kwanza ni pongezi kwa Rais Samia kunusuru Ngorongoro kwa kuepusha shari kwa mtindo wa funika kombe mwanaharamu apite, kwa kupooza tu, lakini ukweli unabaki palepale, Ngorongoro kuna tatizo, tutafute suluhisho la kudumu kwa kuwatendea haki wananchi wa Ngorongoro kwa mujibu wa Katiba, sheria, taratibu na kanuni.

Rais Samia ameupooza mtanziko wa Ngorongoro kupitia tamko la Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), William Lukuvi wakati akizungumza na wananchi wa kata 11 zilizopo tarafa ya Ngorongoro, akiwasilisha maagizo ya Rais aliyewatuma kuwasilikiza wananchi hao waliokuwa wamekusanyika na kukesha kwa siku tano wakitaka kujua hatima ya malalamiko yao.

Waziri Lukuvi alisema Rais ameagiza uchaguzi katika tarafa hiyo kwa kutumia mipaka ya zamani, ufanyike kama utakavyofanyika maeneo mengine nchini. Baada ya Rais Samia kuepusha shari Ngorongoro, Serikali iwawajibishe wale waliotufikisha hapo kwa kutotimiza majukumu yao kikamilifu.

Mwaka 1976, kulitokea mauaji ya vikongwe mikoa ya Mwanza na Shinyanga, Serikali kupitia Makamu wa Rais, enzi hizo, Rashidi Kawawa, Waziri wa Mambo ya Ndani, Ali Hassan Mwinyi, Waziri wa Usalama, Peter Siyovelwa, Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa (DGIS), Emelio Mzena, Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Samweli Pundugu na kamati za ulinzi za mikoa ya Mwanza na Shinyanga, walijiuzulu.

Katika mahojiano ya Mwanza, watuhumiwa wawili, Masaga Makhula Mazengenuka na Isaack Ng’wana Nkhobhoko wakapoteza maisha mikononi mwa polisi. Mwalimu Nyerere alisafisha wote kutokea juu kwa kuwastaafisha kwa manufaa ya umma, Kawawa akashushwa cheo, wakuu wa mikoa ya Mwanza na Shinyanga wakafutwa kazi, maofisa wasimamizi, RPC, RSO, OCD na DSO, wote wakapandishwa kizimbani isipokuwa mshitakiwa mmoja tu, RSO wa Mwanza, aliyeponea tundu la sindano kutokana na kutetewa na wakili mahiri, Murtaza Lakha, lakini wengine wote walikula mvua za kutosha.

Hakuna tofauti ya kilichotokea Mwanza lakini mwaka 1976 na kinachofanyika Ngorongoro, kitendo cha Rais Samia kuingilia kati ni cha kupongezwa, lakini waliotufikisha hapo, wanapaswa kuwajibishwa na pili hatua za Rais Samia kuituliza hiyo hali ni funika kombe, tatizo la Ngorongoro bado lipo, litafutiwe ufumbuzi wa kudumu

Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro (NCA) lilianzishwa mwaka 1959 kwa Wamasai kutoka mbuga ya Serengeti kuhamishiwa Ngorongoro kama eneo la kipekee la matumizi ya mseto ambapo uhifadhi, utalii na maisha ya jadi ya jamii ya Wamasai vingeweza kuishi pamoja.

Idadi ya Wamasai ambayo ilikuja mwanzo kutoka Serengeti ilikuwa takriban 8,000 katika miaka ya 1959, sasa eneo hilo lina watu zaidi ya 100,000. Ongezeko hili la watu limeleta mzigo mkubwa kwenye rasilimali za eneo hilo, hali iliyosababisha uharibifu wa mazingira, ulishaji wa mifugo kupita kiasi na migogoro kati ya uhifadhi wa wanyamapori na shughuli za binadamu na wingi wa watu kutishia ekolojia ya eneo hilo. Japo mpango huu umelenga kuboresha hali ya maisha ya Wamasai ili wapate maisha bora na ya kisasa, unawahatarisha pia watu hao kupoteza uasili wao.

Malengo ya Serikali kuwahamisha Ngorongoro ni jambo jema lakini utekelezaji wake umekumbana na changamoto ikiwemo kuwalazimisha waliogoma kuhama, kutaka kuwahamisha kikuku kwa kutaka kutumia nguvu kwa kuvifuta vijiji na kuzuia vyakula huku akiwakatia huduma muhimu ili kuwashinikiza kuchagua kuhama au kufa njaa kwa Serikali kuvifuta vijiji vyao kinyume cha Katiba, sheria, taratibu na kanuni.

Alichokifanya Rais Samia ni kutuliza mtanziko wa tatizo kwa kulipooza, lakini tatizo bado lipo. Mapendekezo yangu ni; mosi, katika utekelezaji wa mpango huo, Katiba, sheria, taratibu na kanuni za uhamishaji zifuatwe.

Pili, ushirikishwaji wa wahusika kwa kuwatumia viongozi wa Wamasai wenyewe kwa kuanza na malaigwanani wao. Tatu, kufanya tathmini mpya ya kuwatambua Wamasai kama wakazi wa asili na kufanya upembuzi yakinifu nini kina faida zaidi kati ya binadamu na wanyamapori.

Binadamu wakiwa na faida zaidi kiutalii, wanyama ndio wapishe na Tanzania tuanzishe utalii wa wakazi asilia (indigenous people tourism) kama ilivyo kwa wahindi wekundu (red indians) huko Marekani, Aborigines huko Australia na Maori huko News Zealand.

Nne, jamii zote za asili za Tanzania, wakiwemo Wahadzabe, Wamang’ati, Watindiga, Wabarbaig, Wabalungi na jamii asili za makabila mbalimbali zitambuliwe zilindwe na zitunzwe kama kivutio cha utalii.

Tano, kitu muhimu kwenye taifa lolote, haiwezekani mnyama akathaminiwa kuliko binadamu, lakini huyu binadamu akizidi kuzaliana na kutishia ekolojia, lazima adhibitiwe, Marekani walitumia dawa ya kudhibiti uzazi ya Depo Provera, sisi tusifike huko.

Namalizia kwa kuuliza swali hili! Baada ya Rais Samia kuepusha shari kwa kupooza tuu kwa mtindo wa funika kombe, je, Watanzania tujifunze kuukubali ukweli wa tatizo, tutafute ufumbuzi wa kudumu wa tatizo husika, au tuendelee na huu mtindo wetu wa sasa wa kufunika kombe mwanaharamu apite?

Ukweli unabaki pale pale kuwa Ngorongoro kuna tatizo, je, tufunike kombe au tutafute suluhisho la kweli la kudumu kwa kuwatendea haki wana Ngorongoro kwa mujibu wa Katiba, sheria, taratibu na kanuni?

Mungu Ibariki Tanzania.

©Mwananchi
 
la Ngorongoro bado lipo, litafutiwe ufumbuzi wa kudumu.

Siasa ikiwekwa pembeni- watu na wanyama kwa style ya Ngorongoro hawawezi ku co exist na kuweza kuwa wote salama. Something will have to give.
  • Wanyama wakibanwa na mifugo eco system inakuwa challenged na uwindani haramu unaongezeka, magonjwa ya mifugo yanawaingilia wanyama pori, pia mioto ya asili ya pori inabdilika maana mifugo inaweza pia introduce mimea ya kwinginepo inapotoka kupitia kinyesi.
  • ⁠kwa upande wa binadamu, ni ngumu sana kupeleka huduma za kijamii kwa makundi yanayoishi kwa kuwa scattered tena kwenye maeneo yenye hatari. Hivyo it’s hard to have your cake and eat it too. Maendeleo ya service za jamii ili wayapate hiyo namna wanavyoishi inabidi ibadilike.
 
Hapa kuna tatizo kabisa huko mbeleni.
Sasa Inatakiwa tuchague moja kati ya haya mawili
1. Wamasai waondoke Ibaki hifadhi ya Wanyama
2. Wanyama waondoke wabaki Wamasai

Ila kiuhalisia Wamasai ndio wameingia eneo la hifadhi (wao ndo wamevamia hifadhi)

Ila hatuwezi kuwa na wamasai wengi kwenye crater na tukawa na wanyama pia
 
Nne, jamii zote za asili za Tanzania, wakiwemo Wahadzabe, Wamang’ati, Watindiga, Wabarbaig, Wabalungi na jamii asili za makabila mbalimbali zitambuliwe zilindwe na zitunzwe kama kivutio cha utalii.
Kwa nchi hii ni ngumu hayo kuwezekana, ubinafsi wa watendaji wa serikali ni moja ya vikwazo vikuu vya hayo kutekelezeka
 
Ili Tanzania tupate maendeleo ya kweli ambayo ni endelevu, ni lazima tujifunze kuukubali ukweli halisi jinsi ulivyo na kukitokea tatizo, tukabiliane nao kwa kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa tatizo hilo na sio kufunika kombe mwanaharamu apite.

Ngorongoro kuna tatizo, Serikali ilitaka kulitatua kibabe, Wamasai wakagoma, alichofanya Rais Samia Suluhu Hassan ni kufunika kombe tu, lakini tatizo bado lipo na linahitaji ufumbuzi wa kudumu ili tuendelee kuwa na Ngorongoro yenye maendeleo endelevu.

Kufuatia hali ya Ngorongoro ilivyokuwa tete, jambo la kwanza ni pongezi kwa Rais Samia kunusuru Ngorongoro kwa kuepusha shari kwa mtindo wa funika kombe mwanaharamu apite, kwa kupooza tu, lakini ukweli unabaki palepale, Ngorongoro kuna tatizo, tutafute suluhisho la kudumu kwa kuwatendea haki wananchi wa Ngorongoro kwa mujibu wa Katiba, sheria, taratibu na kanuni.

Rais Samia ameupooza mtanziko wa Ngorongoro kupitia tamko la Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), William Lukuvi wakati akizungumza na wananchi wa kata 11 zilizopo tarafa ya Ngorongoro, akiwasilisha maagizo ya Rais aliyewatuma kuwasilikiza wananchi hao waliokuwa wamekusanyika na kukesha kwa siku tano wakitaka kujua hatima ya malalamiko yao.

Waziri Lukuvi alisema Rais ameagiza uchaguzi katika tarafa hiyo kwa kutumia mipaka ya zamani, ufanyike kama utakavyofanyika maeneo mengine nchini. Baada ya Rais Samia kuepusha shari Ngorongoro, Serikali iwawajibishe wale waliotufikisha hapo kwa kutotimiza majukumu yao kikamilifu.

Mwaka 1976, kulitokea mauaji ya vikongwe mikoa ya Mwanza na Shinyanga, Serikali kupitia Makamu wa Rais, enzi hizo, Rashidi Kawawa, Waziri wa Mambo ya Ndani, Ali Hassan Mwinyi, Waziri wa Usalama, Peter Siyovelwa, Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa (DGIS), Emelio Mzena, Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Samweli Pundugu na kamati za ulinzi za mikoa ya Mwanza na Shinyanga, walijiuzulu.

Katika mahojiano ya Mwanza, watuhumiwa wawili, Masaga Makhula Mazengenuka na Isaack Ng’wana Nkhobhoko wakapoteza maisha mikononi mwa polisi. Mwalimu Nyerere alisafisha wote kutokea juu kwa kuwastaafisha kwa manufaa ya umma, Kawawa akashushwa cheo, wakuu wa mikoa ya Mwanza na Shinyanga wakafutwa kazi, maofisa wasimamizi, RPC, RSO, OCD na DSO, wote wakapandishwa kizimbani isipokuwa mshitakiwa mmoja tu, RSO wa Mwanza, aliyeponea tundu la sindano kutokana na kutetewa na wakili mahiri, Murtaza Lakha, lakini wengine wote walikula mvua za kutosha.

Hakuna tofauti ya kilichotokea Mwanza lakini mwaka 1976 na kinachofanyika Ngorongoro, kitendo cha Rais Samia kuingilia kati ni cha kupongezwa, lakini waliotufikisha hapo, wanapaswa kuwajibishwa na pili hatua za Rais Samia kuituliza hiyo hali ni funika kombe, tatizo la Ngorongoro bado lipo, litafutiwe ufumbuzi wa kudumu

Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro (NCA) lilianzishwa mwaka 1959 kwa Wamasai kutoka mbuga ya Serengeti kuhamishiwa Ngorongoro kama eneo la kipekee la matumizi ya mseto ambapo uhifadhi, utalii na maisha ya jadi ya jamii ya Wamasai vingeweza kuishi pamoja.

Idadi ya Wamasai ambayo ilikuja mwanzo kutoka Serengeti ilikuwa takriban 8,000 katika miaka ya 1959, sasa eneo hilo lina watu zaidi ya 100,000. Ongezeko hili la watu limeleta mzigo mkubwa kwenye rasilimali za eneo hilo, hali iliyosababisha uharibifu wa mazingira, ulishaji wa mifugo kupita kiasi na migogoro kati ya uhifadhi wa wanyamapori na shughuli za binadamu na wingi wa watu kutishia ekolojia ya eneo hilo. Japo mpango huu umelenga kuboresha hali ya maisha ya Wamasai ili wapate maisha bora na ya kisasa, unawahatarisha pia watu hao kupoteza uasili wao.

Malengo ya Serikali kuwahamisha Ngorongoro ni jambo jema lakini utekelezaji wake umekumbana na changamoto ikiwemo kuwalazimisha waliogoma kuhama, kutaka kuwahamisha kikuku kwa kutaka kutumia nguvu kwa kuvifuta vijiji na kuzuia vyakula huku akiwakatia huduma muhimu ili kuwashinikiza kuchagua kuhama au kufa njaa kwa Serikali kuvifuta vijiji vyao kinyume cha Katiba, sheria, taratibu na kanuni.

Alichokifanya Rais Samia ni kutuliza mtanziko wa tatizo kwa kulipooza, lakini tatizo bado lipo. Mapendekezo yangu ni; mosi, katika utekelezaji wa mpango huo, Katiba, sheria, taratibu na kanuni za uhamishaji zifuatwe.

Pili, ushirikishwaji wa wahusika kwa kuwatumia viongozi wa Wamasai wenyewe kwa kuanza na malaigwanani wao. Tatu, kufanya tathmini mpya ya kuwatambua Wamasai kama wakazi wa asili na kufanya upembuzi yakinifu nini kina faida zaidi kati ya binadamu na wanyamapori.

Binadamu wakiwa na faida zaidi kiutalii, wanyama ndio wapishe na Tanzania tuanzishe utalii wa wakazi asilia (indigenous people tourism) kama ilivyo kwa wahindi wekundu (red indians) huko Marekani, Aborigines huko Australia na Maori huko News Zealand.

Nne, jamii zote za asili za Tanzania, wakiwemo Wahadzabe, Wamang’ati, Watindiga, Wabarbaig, Wabalungi na jamii asili za makabila mbalimbali zitambuliwe zilindwe na zitunzwe kama kivutio cha utalii.

Tano, kitu muhimu kwenye taifa lolote, haiwezekani mnyama akathaminiwa kuliko binadamu, lakini huyu binadamu akizidi kuzaliana na kutishia ekolojia, lazima adhibitiwe, Marekani walitumia dawa ya kudhibiti uzazi ya Depo Provera, sisi tusifike huko.

Namalizia kwa kuuliza swali hili! Baada ya Rais Samia kuepusha shari kwa kupooza tuu kwa mtindo wa funika kombe, je, Watanzania tujifunze kuukubali ukweli wa tatizo, tutafute ufumbuzi wa kudumu wa tatizo husika, au tuendelee na huu mtindo wetu wa sasa wa kufunika kombe mwanaharamu apite?

Ukweli unabaki pale pale kuwa Ngorongoro kuna tatizo, je, tufunike kombe au tutafute suluhisho la kweli la kudumu kwa kuwatendea haki wana Ngorongoro kwa mujibu wa Katiba, sheria, taratibu na kanuni?

Mungu Ibariki Tanzania.

©Mwananchi
Mtuhumiwa namba moja eti ndiye anapongezwa.
Cause a problem then solve the problem you caused.
 
Mwandishi alieandika hapa ana akili sana. Tunahitaji waandishi wa hivi...anaandika kama Paschal
 
Sasa Inatakiwa tuchague moja kati ya haya mawili
1. Wamasai waondoke Ibaki hifadhi ya Wanyama
2. Wanyama waondoke wabaki Wamasai

Ila kiuhalisia Wamasai ndio wameingia eneo la hifadhi (wao ndo wamevamia hifadhi)

Ila hatuwezi kuwa na wamasai wengi kwenye crater na tukawa na wanyama pia
Kwani kuna wamasai crater?? Hata siku moja hutakaa umkute masai crater., crater kule shimoni wanaishi wanyama tuu. Wamasai wanaishi juu. Na wamasai wanalinda wanyama na hawawaui. Wamasai sio majangili
 
..Nini kinachomvutia Mmaasai kiasi kwamba hataki kuhama Ngorongoro?

..Nini unashauri kifanyike ili baadhi ya Wamaasai wahamie eneo lingine nje ya linalopendekezwa kwa uhifadhi.
 
Sasa Inatakiwa tuchague moja kati ya haya mawili
1. Wamasai waondoke Ibaki hifadhi ya Wanyama
2. Wanyama waondoke wabaki Wamasai

Ila kiuhalisia Wamasai ndio wameingia eneo la hifadhi (wao ndo wamevamia hifadhi)

Ila hatuwezi kuwa na wamasai wengi kwenye crater na tukawa na wanyama pia

..kama hoja yako ni ya kweli basi serikali itafute namna ya kufanya maeneo nje ya Ngorongoro kuwa more attractive kwa Wamaasai kufuga.

..pia suala hilo kifanyike kwa kushirikisha jamii inayohusika na sio kutumia mabavu na kurupushani.

..Ngorongoro inaingiza mapato mengi sana, sielewi kwanini serikali inashindwa kuandaa program endelevu ya kupunguza idadi ya Wamaasai ktk hifadhi zetu.

..Lengo lisiwe kuwaondoa Wamaasai wote. Pia lengo lisiwe kuwaondoa Wamaasai na kuleta Waarabu.
 
Issue kubwa hapo Ngorongoro ni ukuaji wa population ya watu kutoka 8,000 hadi kufikia zaidi ya 100,000. Pamoja na idadi ya mifugo kuongezeka hivyo kupelekea binadamu kutafuta eneo zaidi ndani ya hifadhi kwaajili ya makazi na malisho ya mifugo yao, kitu ambacho kwa hakika ni changamoto kwenye uhifadhi wa mbuga hiyo ya Ngorongoro.

Project ya kuwaondoa wakazi wa Ngorongoro nadhani imekuwa too rapid, Serikali haijaweza kutake time kufanya research juu ya amdhara yanayoweza kujitokeza wakati wa utekelezaji wa zoezi hili, pia kushindwa kuwaandaa wananchi wake juu ya zoezi hili huku wakiendelea kutoa elimu juu ya umuhimu wa zoezi hili kwa maisha endelevu ya Hifadhi yetu.

Kuna madhara makubwa yanayojitokeza kwa kutizama kwa haraka tu
Ikiwa ni pamoja Na kupoteza utulivu katika hifadhi, pia kuwaondoa wananchi jamii ya wamaasai ni kupoteza kivutio cha kipekee ndani ya maisha ya Ngorongoro ambapo ni hifadhi pekee kama sitokosea ambayo inamjumuiko wa wanyama pori pamoja na binadamu kwa pamoja.

Cha muhimu kabisa serikali ingeanza kutoa elimu juu ya wananchi wa Ngorongoro kuhusu udhibiti wa idadi ya mifugo yao kulinganisha na eneo la makazi.

Pili, juu ya ongezeko la idadi ya watu na eleo linaloruhusu watu kuishi bila kuathiri ecology, dunia ya sasa elimu katika kila jambo ni muhimu kuliko kutumia nguvu bila maelewano ili kuepuka madhara makubwa yanayoweza kujitokeza baada ya mchakato kufanyika.
 
Binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja.Je CCM wanaitendeaje hii Ahadi?
 
Binadamu ni kiumbe cha thamani kubwa mno hata mbele za Mungu, ila pia ni kiumbe hatari na muharibifu sana hivyo inabidi kumdhibiti ili maisha yawe mazuri, tatizo kubwa hapa ni njia zinazotumika ndiyo kandamizi.

Sehemu zote zilizohifadhiwa zinapaswa kuheshimiwa kwa kufuata sheria husika pia kwa kuzingatia utu wa mtu.
 
Watu wenye nguvu na akili wakiajiliwa sehemu mbalimbali za nchi utashangaa jamii hiyo inapungua taratibu katika eneo hilo maana hata vijana watakimbilia sehemu nzuri walikoajiriwa wengine na sehemu hiyo itabaki salama.Lakini kuwahamisha Wamasai kwa nguvu na kuwapeleka sehemu nyingine ambayo hawakuizoea ni uonevu uliopindukia.Cha ajabu zaidi unamwamisha Mmasai halafu unamleta Mwarabu,hivi hiyo inaingia akilini kweli?
 
😂😂💔
 
Kwa nini ongezeko la wamasai kwenye eneo lao la asili iwe sababu ya kuwapeleka uhamishoni wakati wanyama nao kwa vyovyote tangu mwaka 1959 wameongezeka pia?
Kwa nini wanyama wasihamishiwe sehemu nyingine kwenye mapori ya akiba kama Moyowosi na Kigosi? Kwa nini macho yote ya Serikali na wafadhili wake yanaelekezwa Ngorongoro na Serengeti tu? Kwa nini wamasai waondolewe lakini waarabu wakaribishwe?
Kati ya wamasai na Serikali ya mkoloni iliyoanzisha upuuzi huu wa kuthamini wanyama kuliko wanadamu, nani aliyetangulia kuwepo Ngorongoro? Hiyo hadhi ya kuwa urithi wa Dunia ambayo Serikali yetu inaitetea zaidi kuliko wananchi wake, si mwendelezo wa ukoloni? au kuna watu Serikalini wanaonufaika na mgao unaotokana na mpango huu wa kidhalimu?..... Nawaza kwa kuweweseka kama sina akili nzuri lakini itoshe tu kusema INASIKITISHA!! 🤔
 
Back
Top Bottom