Hili la Sakho si jambo geni kwetu

Msimu wa 2014 YANGA ilitoa Top Scorer wa CAF Champions League/LIGI YA MABINGWA AFRICA hata na wala huezi kukuta wachambuzi wa mchongo wanaisema hii kwa ukubwa wake!

Mkuu, changamoto iliyopo ni top scorer wetu wa Jangwani alifunga jumla ya magoli SITA dhidi ya timu moja tu tena dhaifu ya Komorozine ya Comoro ktk hatua ya awali ya mtoano ligi ya MABINGWA AFRICA,
Na kwa bahati mbaya timu yetu haikufika hata hatua ya makundi kwani ilitolewa round iliyofuata

Ukija kwa wenzetu wanaMsimbazi, mchezaji wao kawa top scorer kwa kufunga magoli dhidi ya timu ngumu tofauti tena hatua ngumu ya makundi na kisha timu yao ikafanikiwa kuingia hatua ya ROBO FAINALI

Tumpe kongole PO SAKHO,,kaipaisha timu yake, kaipaisha ligi yetu
 
Hahaaaaaa unadhani hatukumbuki... hahahaaaaaa

Ngassa alifunga magoli yote kwenye mechi moja utopolo walivyokutana na kibonde sijui kutoka wapi huko...

Hiyo tuzo yake alipokelea Afghanistan au Iraq?
Venezuela 🤣🤣🤣🤣
 
P. O. S kapokea tuzo ya goal of the year na sio top scorer.

Ila kaipaisha Simba na yeye mwenyewe kapanda zaidi sitaona ajabu akiitwa hata timu ya taifa, Simba kibiashara wanaweza kumuuza kwa bei kubwa, japokuwa mkataba wake haueleweki
 
P. O. S kapokea tuzo ya goal of the year na sio top scorer.

Ila kaipaisha Simba na yeye mwenyewe kapanda zaidi sitaona ajabu akiitwa hata timu ya taifa, Simba kibiashara wanaweza kumuuza kwa bei kubwa, japokuwa mkataba wake haueleweki
Mkataba unaeleweka vzr tu, wakati wanakuja wachezaj watatu walisain miaka mi3
Sakho
Banda
Kanoute
Achana na yule mzee wa kudere
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…