Sexer
JF-Expert Member
- Oct 22, 2014
- 8,440
- 8,149
Haya maigizo wanayofanya Simba sc sio ya kufumbiwa macho kabisa na mamlaka, zichukuliwe hatua kali kwa viongozi wa Simba, Meneja wa uwanja ambaye pia ni mwanasimba pamoja na kamishna wa mchezo (mwanasimba) kwa kula njama ya kuzuia Simba sc isiingie uwanjani Taifa kufanya mazoezi ili wapate kisingizio cha kulalamika na kutoleta timu uwanjani tarehe 8 ili kukwepa kufungwa goli 8 na Yanga SC. Kazi kwenu TFF, tumieni wale mabaunsa wanasimba waliokuwa wanaigiza kuzuia Basi mtapata ukweli wote.