Hili la Vincent Bossou lina somo kubwa sana. Tusiache kujifunza

Hili la Vincent Bossou lina somo kubwa sana. Tusiache kujifunza

GuDume

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2015
Posts
6,651
Reaction score
14,337
Huu ni muendelezo wa utovu wa nidhamu ambao unaoneshwa mara nying Na wachezaji wa Kigeni na pia hata wa ndani. Huu ni udhaifu ambao unaendelezwa saba na wachezaji wa kiafrika.

Sikatai madai yake ya mshahara ni sahihi kabisa. Lakini kuna haja gani ya kuutangazia umma na kujibishana na wanachama? Kama suala lake amelipeka kwa viongozi haoni kama inatosha? Lakini je kuna haja ya kugomea mechi?au kuwaidhalilisha team husika?

Nakumbuka msimu uliopita kiiza naye alifanya uhuni kama huu na kufikia kuwashawishi wachezaji wenzie wagome au wacheze chini ya kiwango na watu wasiofaham hili waliuliza simba inamwache mchezaji aliyekuwa na magoli mengi aende zake? Kumbe tatizo lilikuwa ni ukosefu wa nidhamu alioobesha hamis kiiza.

Mimi binafsi siwez kumsajili vincent bossou hata angekuwa na magoli 200 katika mechi 20. Mchezaji wa namna hii ni mfano mbovu wa kimaadili katika soka.

Yanga mnapaswa kujifunza kuwa kuwa wa kimataifa si kupanda ndege. Ni kulipa wachezaji wenu mishahara kwa wakati na bila kigugumizi. Ila kama mnadhan hawa wachezaji wamekuja kupanda ndege basi endeleeni tu kuwapandisha ndege muone kama hilo litawasaidia.
 
Mnyonge mnyongeni ila haki yake mlipeni, najua yanga wengi bado tuna hasira za kufungwa na simba na kinacho onekana bado tuna wenge na tunatafuta wa kumuangushia jumba bovu, ki ukweli nyuma pazia yanga kuna matatizo mengi yanayotokana kumtegea mtu mmoja kwa kila kitu,
 
Biashara ngumu saa hizi, hela za kulipa mishahara mikubwa itakuwa ngumu kuipata.
 
0bcbf9cd022ce2e23562ae62b16c69bf.jpg
kuna huyu pia naye ana matatizo na Yanga
 
Bila mshahara ataishi vipi!,madai yake ni ya msingi sana,acheni ngonjera,mpeni haki yake..
 
Back
Top Bottom