Mara kadhaa hukutana na Ma-ustaadhi wakiwa na visanduku au mifuko wakiomba Sadaka/Swadaka kwa ajili ya misikiti
(Sio michango)
Hapo Huwa najiuliza huu ni utaratibu mzuri kweli? Maana waumini wanafika au wanatakiwa kufika ibadani katika misikiti au makusanyiko ya kiibada, na hapo ndipo mahala sahihi pa kutoa Sadaka zao pamoja na kufanya Ibada.
Sasa hii ya kuzunguka barabarani na visanduku au mifuko kuomba sadaka, ndio tunawaambia waumini inatosha wasije ibadani? Au wakija Ibadani hakuna haja ya Sadaka wasubiri watembelewe na visanduku? Kwanini wakati swala mbali mbali kama Ijumaa au nyinginezo za Kila siku zisitumike na waumini kutoa Sadaka zao katika Ibada hizo?
Lakini pia jambo hili haliwezi kutumiwa na watu wasio na sahihi au na maadili, wakaamua kuzungukia watu kwa kisingizio kuwa ni Sadaka ya msikitini kumbe sio?