Leo nimekaa na mke wangu tunakula ghafla maziwa yakamuuma akaniambia mtoto anakojoa ndani ndo Mana yananiuma, maana mtot ana miezi miwil alikuwa amelala.
Nikamwambia acha Imani zako za kiswahili twende tukahakikishe, tumefika tumemfunua mtoto kweli kakojoa.
Na akanambia mtoto akiwa amelala yeye yupo nje maziwa yakimuuma ima anakuwa amelala kwahiyo ndiyo anaamka anaanza kuliaau kakojoa.
Wakati nimeanza kazi, kuna watu waliniudhi kazini, nikagombana nao na nikalia sana. Muda huo huo mama yangu aliekuwa mkoa mwingine akanipigia simu na kuniuliza "kuna shida gani imetokea".
Hii ni kusema kwamba, kwa wamama wenye bond na watoto wao, huwa wanapata hisia fulani linapotokea jambo kwa mtoto wake. Hisia hizo ziko juu zaidi kati ya mama na watoto wachanga. Lakini pia zinaendelea hata mtoto akiwa mkubwa.