Hili nalo ni tatizo/changamoto? Inawezekana kuliepuka?

kuku dume

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2012
Posts
414
Reaction score
62
Jamani kila mara huwa natafakari nashindwa kuelewa.

Nilipokuwa darasa la saba pale Mandaka yalitokea mauaji ya mume wa mpishi wetu wa shule. Nilisikia kwamba aliuwawa na wapenzi wa mke wake na mara nyingine nikasikia kwamba aliuwawa na watu walioandaliwa na mke wake maana alikuwa kizuizi cha yeye kufanya mambo yake.

Sio hilo tu ila ninauchungu kwa kuwa kuna jambo la namna hii lililowahi kuikumba familia yetu.

Jamani ninachotaka kuulizo ni kwamba Je, mtu anaweza kukuambia anakupenda kumbe wala hana hisia kama hizo kwako? Binafsi nahisi kwamba anaye fikisha ombi la kupenda ndiyo mpendaji. Huyo mwingine siamini kama kweli anakuwa mpendaji.

Ebu fikiri yalivyo mapenzi ya siku hizi. Fedha, magari, beautness, nyumba vinanguvu ya kuhamua wa kuwa naye badala ya true love.

Napatwa na wakati mgumu nikifikiria wakati wangu wa kuwa na mtu utakapofika.

Sijui dunia ikoje. Sifahamu itakuwaje.
 
Utafahamu yakikukuta, kupenda ni kubaya sana - kupendwa ndo raha!
 
yatakuwa poa tu IN THE NAME OF JESUS
 
Uhondo wa ngoma uingie ucheze.Ingia kwenye mahusiano ndo utajua wa2 wanahusianaje coz kila m2 anakituko chake so subiri na we chako
 
Ngoma yenyewe inaonekana hamna uhondo. Huu umekuwa uhondoa.

Watu wanauwawa, wanatoswa, wanakuwa machizi na wengine kufikia hatua ya kujiuzulu. Huo ndiyo uhondo?

Nyie huko ndani kazaneni ila sisi wengine hatuna hamu ya kuingia na huenda hatuta ingia kwabisa. Wacha nione kama wakati ukifika wa kuitwa mzee wengine watabaguliwa kisa hawakuoaga wala kuolewa.
 
Usijichoshe akili utaumia kwa fikira tumuachie jalali muweza alo na kudra,nnajua wateseka kweli kwashauku na wingi wa hamu namimi nakutaka kweli uwewangu muathamu,hilini jambo sahali kilibariki kareemu Kama nia zetu safi kweli mola aatalirahamu,poa moto usijali hub a sitokuthulumu yailahi ya jalaali tusaidiee kareemu......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…