Hili ndilo lilikuwa lengo la tcu kuingilia udahilishaji wa wanafunzi vyuo vikuu.

Chagga King

JF-Expert Member
Joined
Jul 6, 2011
Posts
1,866
Reaction score
1,076
..watanzania hasa wale wa hali za chini tulishukuru kukuwa kwa sekta ya elimu hasa katika ngazi ya vyuo vikuu, ongezeko la vyuo binafsi lilipunguza idadi ya wanafunzi wenye sifa za kuendelea na chuo kukaa nyumbani kwani kilammoja alipata nafasi, (hata mimi pia) kwani vyou viliweza kumudu idadi kubwa ya wanafunzi waliokuwa wanahitimu elimu ya sekondari,
...tume ya vyuo vikuu (tcu...tanzania commission for universities) nayo ilichangia kwa kiasi kikubwa katika ongezeko la vyuo hivi, kwani ndio taasisi pekee yenye mamlaka ya kudahili vyuo hivi katika ngazi zote hadi kuwa "chartered", na tunatambua kila muombaji wa chuo alikuwa na haki ya kuomba chuo chochote akipendacho ilimradi tu awe ametimiza vigezo.
...mnamo mwaka 2011, tcu ilikuja na utaratibu wa tofauti hasa katika udahilishaji wa wanafunzi vyuoni, kwani ilijipa jukumu la kudahili mwanafunzi katika chuo, hili jambo limeleta utata na ni tatizo kubwa kwa wanafunzi, kwani
1. Imeondoa uhuru wa mwanafunzi kusoma chuo akipendacho, maana tumeona muombaji anaweza kuweka tchuo cha tumaini kuwa ndio 1st choice, lakini unakuta amepangwa udsm.
2. Imeondoa haki ya mwanafunzi kusoma course aipendayo na aiwezayo, hilo nalo limeonekana pia
3. Utaratibu wa kuomba nao umekuwa ni mgumu sana, hasa kwa wale ambao wanatoka sehemu za vijijini ambapo hakuna internet
.
..........
Lakini lengo langu kubwa ni kuhusu nia ya tcu kuingilia jukumu la allocate wanafunzi,
....baada ya chuo kikuu cha dodoma (udom) kuanzishwa, miaka michache baadaye ndio tcu wakaja na huo utaratibu, tunajua ukubwa wa chuo hicho, na tuliona ni jinsi gani chuo hicho kilianza kupoteza muelekeo, hivyo wanafunzi wengi wakawa wanakikimbia, hilo likawa ni tatizo kwa chuo, basi ndio tcu wakaingilia kati jukumu la kupangia wanafunzi chuo watakachosoma lengo ikiwa ni kuki feed chuo cha udom, maana waliogopa competition na vyuo vingine binafsi mfano saut walikuwa wameshakuwa na matawi zaidi ya kumi, vivyo hivyo kwa tumaini na vyuo vingine binafsi.

Huu ni mtazamo tu, inaweza ikawa ndivyo au sivyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…