BAKIIF Islamic
JF-Expert Member
- Jul 11, 2021
- 600
- 1,843
Naam,
Siku moja Nabii Mussa (a.s) alimueleza MUNGU yakwamba; Ewe Mwenyezi MUNGU nina maombi nataka nikuombe.
Mungu akamjibu, omba ombi lako lolote Mussa, mimi nitakujibu.
Mussa akamueleza Mwenyezi Mungu
Ewe mwenyezi Mungu, ninakuomba hizi habari za kuwachoma watu kwenye moto siku ya mwisho ni vyema ungeziondoa, watu wenyewe ni dhaifu hawana nguvu wala uwezo, wewe ndio una nguvu zote, na wewe ndio mwenye uwezo wa kila kitu, kwanini sasa uwachome hawa binaadamu dhaifu kwenye moto, mimi nakuomba ondoa hii adhabu ya kuchoma watu kwenye moto. Haya ni maombi yangu nakuomba ewe Mwenyezi Mungu.
Mwenyezi Mungu akamueleza Mussa:
Ewe Mussa, haraka sana tengeza shamba. Mussa akaanza kutengeneza shamba, akalisafisha shamba lake, akalima kisha akapanda mazao, baada muda kukamilika akaja akavuna mazao yake, akayahifadhi vizuri na kuyatunza, kisha akarudi shambani kwake, akakusanya vijiti, yaani mabua ya mimea yaliyokauka na kubakia hapo shambani, akavikusanya sehemu moja kisha akavichoma moto.
Mungu akaumueleza, ewe Mussa umefanya nini hapo?
Mussa akajibu: Nimekwisha vuna mazao yangu safi nimeyahifadhi ndani, sasa nina mpango huwenda msimu mwingine nitalima tena kwa hivyo hivi vijiti naona vitanisumbua ndio nimeamua nivichome moto kwasababu ni mabua sina faida nayo.
Mungu akamueleza Mussa;
Hivyo hivyo ulivyofanya Mussa, ndivyo na mimi Mwenyezi Mungu ninafanya kwa wanaadamu, katika binaadamu kuna watu ambao sina faida nao, nitawachoma katika moto wa Jahannam. Japokuwa wamezalika katika dunia hii lengo kuu ni kupata ile mbegu safi, ambayo mimi nitaihifadhi katika pepo yangu, na waliobakia ni mfano wa vijiti au mabua nitawachoma katika moto wa Jahannamu kwasababu sina faida nao hata kama wamezalika katika dunia. Kama ulivyofanya wewe Mussa.