Hili Neno Kama Ugonjwa wa Kuambukiza! Wengi wameambukizwa, Kila Mtu analitumia.

Hili Neno Kama Ugonjwa wa Kuambukiza! Wengi wameambukizwa, Kila Mtu analitumia.

SHIEKA

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2011
Posts
8,240
Reaction score
4,265
Ni uvivu wa mawazo au ni kitu gani? Ukimsikia mbunge akichangia bungeni, ukimsikiliza mtangazaji redioni au kwenye
tv, lazima utamsikia akisema, kimsingi........ Yaani kila mazungumzo sasa hivi ni kimsingi tu. Huko nyuma neno tawala lilikuwa .....swala zima...... Sasa ni kimsingi, kimsingi, nk. Ni maambukizo gani haya makali hivyo?
Yaani inanifanya kuwaza kwamba kama mtu hajatumia hilo neno atashindwa kutoa wazo lake.......kitu ambacho si kweli.
Nakereka sana pale mtu anapolitumia zaidi ya mara moja.Kila kitu kwake ni Kimsingi tu.........kimsingi.Naona ni aina ya uvivu wa lugha.
 
Kimsingi unatakiwa ukubali kuwa hiyo ndio lahaja ya sasa na ujue kuna lugha ya wakati fulani kutegemea na uhalisia wa wakati huo. KIMSINGI kubali matokea hata kama KIMTINDO linakukwaza mheshimiwa SHiEKA.!
 
SHIEKA usikwazike na matumizi ya muda ya baadhi ya maneno, yataibuliwa na kufifia kwa mtindo wa misimu mfano neno "kasheshe" lilikuwa maarufu sana miaka ya 90 lakini leo halina nguvu tena na linatumika kwa nadra sana.

"kimsingi umekosea pia kuandika neno swala badala ya suala kwenye hili suala zima la kuelimisha wadau". Teh teh teh mkuu hapo kwenye semi nimejaribu tu nikashindwa, kumbe kweli ni kero.
 
Last edited by a moderator:

Nayakubali maoni yenu wandugu, hasa pale mnapogusia kwamba ni neno la msimu kama ilivyokuwa kwa neno 'kasheshe' ambalo lilivuma sana na sasa halitumiki tena.
 
mtoa mada sijakuelewa kinachokukwaza ni nini.
kimsingi mtu huchagua misamiati ambao amevutiwa nao na ambao utavutia usikivu wa wasikiliza na ndio maana maneno kama haya huzuka
 
kimsingi hata kitaani kwetu limevuma kiasi chakunikera aghalabu.
 
Mkuu umesahau neno hili "kwakuwa...." nalo linakera sana kwa hao wabunge.
 
Kimsingi mimi neno KIMSINGI halinikeri ila nakereka sana na neno KWAKUWA, kwakuwa linatumiwa na kila mbunge bungeni as if liko kwenye kanuni
 
kimsingi itungwe sheria kabisa ya wachafuz wa lugha
 
Back
Top Bottom