Kimsingi unatakiwa ukubali kuwa hiyo ndio lahaja ya sasa na ujue kuna lugha ya wakati fulani kutegemea na uhalisia wa wakati huo. KIMSINGI kubali matokea hata kama KIMTINDO linakukwaza mheshimiwa SHiEKA.!
Nayakubali maoni yenu wandugu, hasa pale mnapogusia kwamba ni neno la msimu kama ilivyokuwa kwa neno 'kasheshe' ambalo lilivuma sana na sasa halitumiki tena.SHIEKA usikwazike na matumizi ya muda ya baadhi ya maneno, yataibuliwa na kufifia kwa mtindo wa misimu mfano neno "kasheshe" lilikuwa maarufu sana miaka ya 90 lakini leo halina nguvu tena na linatumika kwa nadra sana.
"kimsingi umekosea pia kuandika neno swala badala ya suala kwenye hili suala zima la kuelimisha wadau". Teh teh teh mkuu hapo kwenye semi nimejaribu tu nikashindwa, kumbe kweli ni kero.
Linakeraje? Au huelewi? UlizaMkuu umesahau neno hili "kwakuwa...." nalo linakera sana kwa hao wabunge.