Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kabisa, pia badala ya kipofu tunasema Mtu asiyeona au mwenye uoni hafifu.BBC hao hao nilimsikia reporter wao akiwaita watu wasioona 'vipofu'. Kutumia maneno kama zeruzeru, vipofu au viziwi kunakuwa kuna hali fulani ya udunishi ndani yake.
Ni vyema tukatumia majina yenye kuonesha thamani ya mtu mfano badala ya kuita
-zeruzeru tutumie mtu mwenye ulemavu wa ngozi
-kiziwi tutumie mtu mwenye ulemavu wa kusikia n.k
Sent using Jamii Forums mobile app
Sio tatizo, ila inashauriwa tusitumie hilo jina.Ni sahihi, maana Albino nj english. Zeruzeru kiswahili. Sioni kama kuna tatizo.
Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi neno "zeruzeru" linadharirisha vipi, si ni neno la kiswahili kumaanisha mtu mwenye ulemavu wa ngozi!Si vema kutumia maneno yenye mlengo wa kudharirisha. Tunashauriwa kutumia tafsida zaidi kuliko maneno magumu.
Sent using Jamii Forums mobile app
Waarabu wa afrika buana!!Inaitwa TAFSIDA kupunguza ukali wa maneno, hivyo BBC iwapo wamelitumia neno ZERUZERU kama kilivyo pasi na nia ya kudadavua kua "neno hili lisitumike hivi" kiandishi watakua wamekosea na inawezekana ni makosa tu ya kibinadam.
Katika kiswahili fasaha utangulizi wa maneno haya huonyesha tahadhari kabla ya matamshi ASHAKUM SI MATUSI ndipo ukalitaja neno ZERUZERU ingeweza kuswihi pia.
Sent using Jamii Forums mobile app
mzee sasa hapo unakuwa unatoa maana sasa, kwa hiyo hao watu hawapaswi kuitwa majina yao bali kuelezewa sifa zao?BBC hao hao nilimsikia reporter wao akiwaita watu wasioona 'vipofu'. Kutumia maneno kama zeruzeru, vipofu au viziwi kunakuwa kuna hali fulani ya udunishi ndani yake.
Ni vyema tukatumia majina yenye kuonesha thamani ya mtu mfano badala ya kuita
-zeruzeru tutumie mtu mwenye ulemavu wa ngozi
-kiziwi tutumie mtu mwenye ulemavu wa kusikia n.k
Sent using Jamii Forums mobile app
Duh basi hao wenzako wana matatizo.Hakuna cha "Waarabu wa Afrika" hapo bali hata kwa wenzetu na lugha zao, huwa wanatumia lugha za staha katika kuelezea ulemavu wa mtu! Kwa mfano, kwao kwa mtu aliye muungwana hawezi akasema XYZ is disabled bali atakuambia XYZ has disability.Au hawezi kusema "Disabled people come forward" bali "people with disability...."
Au XYZ has hearing impairment badala ya kusema XYZ is deaf! Badala ya kutumia XYZ is blind, watasema has visual impairment/visually impaired!!
Sio kwamba kumuita mtu deaf ni kosa but it sounds kind of rude and offensive kwa sababu kuwa kipofu ni zaidi ya kushindwa kuona; kuwa kiziwi ni zaidi ya kushindwa kusikia