Shark
JF-Expert Member
- Jan 25, 2010
- 29,775
- 29,746
Asubuhi ya tarehe 28 October niliamka mapema tu nikiwa na furaha. Nilikua nimepanga lazima " Nikachinje" watu watatu kutoka chama kile "Cha Siku Zote". Kichinjio changu kilikua tayari tayari stand by.
Siku hiyo jinsi nilivokua na hamu ya kuchinja wale Jamaa watatu hata chai niliwaza nije kunywa nikirudi kutoka "Machinjioni". Nikapiga number za kucheck kituo kilipo ili nisije nikaenda kwengine. Kituo ni kile kile Cha 2015, na bahat nzuri sijahama mtaa.
Basi nimefika eneo la tukio sikupata tabu kujua chumba kilipo. Tukio lilifanyika kwenye Shule ya Msingi, hivyo kituo changu ni darasa Mojawapo. Kura zinapigwa mbele kwenye angle ya opposite na mlango.
Nimeingia pale nikakuta jamaa kama wanne wa tume wamevaa T-shirt nyeupe zenye nembo ya tume. Pia kulikuwepo na wengine wawili wamevaa kawaida tu wanapiga story, nikajisemea hawa bila shaka ndo mawakala wa vyama. Kimoja labda ni CCM Ila kingine sijui ni kipi.
Mfanyakazi wa kwanza wa tume alioko karibu na mlango alichukua kadi yangu na kuanza kuita jina langu mara tatu. Niligeuka kule kwa mawakala nikaona wanasikiliza tu, hawafanyi chochote. Hapa ndipo nilipoanza kukosa nguvu, nikaona kabisa lengo langu la "kuchinja" halitotimia ipasavyo.
Baada ya hapo nikamaliza taratibu zingine na kuondoka kinyonge. Nilijua kabisa tu kwa utaratibu ule "hatutoboi" hata chembe. Kwa jinsi navyowajua "Wale Jamaa" pale tayari tushapigwa bao za mapema tu, kushinda hii game ni majaaliwa.
SHIDA IKO WAPI?
Vyama vilipewa orodha / register ya wapiga kura, ilifaa kila kituo wakala awe nayo angalau. Ili tukiwa tunaita majina wawe wanaweka tiki kwenye hizo nakala zao. Hii itawezesha kujua wangapi wamepiga kura kwenye kituo husika.
Lakini Sasa ndio unakuta mambo kama ya Kahama Ubunge jumla kura 50,000+ wakati Urais jumla kura 167,000+. Hakuna wakala anaejua idadi kamili ya waliopiga kura kwenye kituo alichosimamia. Sasa vitabu/register tulipewa za nini jamani? Wakala unaendaje kituoni bila kitabu? Hata wakiongeza idadi unajuaje?
Hivi ni kweli tuliamini hawa jamaa wataendesha Uchaguzi usiokua na figisu zozote mpaka tusahau jambo muhimu kama hili? Tuna wabunge wana uzoefu sana na hizi figisu, walishindwa kukumbuka jambo muhimu kama hili kweli? Sasa nini maana ya Mtumishi wa Tume kuita jina langu mara tatu ikiwa wakala hana popote anapo-verify?
Niliwaza nisiandike haya sababu uchaguzi umeshafanyika, lakini siwezi kukaa na dukuduku, hata baadae Uchaguzi ujao itasaidia.
Weekend njema.