Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
HILI NI JUMA ZIMA LA VITABU DUNIANI 5
''Rajabu Ibrahim Kirama Jemadari wa Vita Kuwa Jemadari wa Uislam''
Mwandishi: Mohamed Said
Mchapaji: Readit Books Ltd Dar-es-Salaam
Ukoo wa Rajabu Ibrahim Kirama wa Machame Nkuu umehifadhi kwanza kichwani historia ya wazee wao kwa simulizi kutoka kizazi hadi kizazi kwa takriban miaka 300.
Wamishionari walipoingia Uchaggani na kufungua shule na watu kuanza kusoma na kuandika Rajabu Ibrahim Kirama alihifadhi barua zake alizokuwa akiandika na kupokea.
Baadhi ya waandishi wa barua zake nyingine zikiandikwa kwa Kiingereza ni Paul Njau na Joseph Merinyo wazalendo muhimu katika historia ya Wachagga.
Nyaraka hizi zinakaribia miaka 100 na mwanae mkubwa Salim alizihifadhi nyaraka hizi baada ya kifo cha baba yake mwaka wa 1962.
Nyaraka hizi zimenifikia na nimeandika kitabu cha maisha ya Mzee Rajabu Ibrahim Kirama, mtoto wa Jemadari wa Vita katika Utawala wa ukoo wa Mangi Shangali.
Kama si kuingia kwa Wajerumani Uchaggani baada ya Mkutano wa Berlin wa 1884 Rajabu Kirama wakati huo akijulikana kwa jina la Kirama Muro angevaa deraya ya Jemadari wa Majeshi walizovaa babu zake miaka mingi iliyopita kulinda mipaka ya nchi yake.
Picha:
Jalada la kitabu.
Mwandishi na Mhariri wa kitabu Abdallah Saiwaad.
Marehemu Bi. Hawa Rajabu Kirama (Mama Ali) na mdogo wake Sheikh Idrissa Rajabu Kirama.
Mama Ali kwa upande wa mama yake ni Ukoo wa Mangi Shangali na kwa baba ni Ukoo wa Jemadari Muro Mboyo baba yake Rajabu Ibrahim Kirama na Rajabu Kirama amelelewa kwenye nyumba ya Mangi Sina wa Kibosho.
Mama Ali ndiye aliyenipa simulizi ya historia ya baba yake Rajabu Ibrahim Kirama.
Mama Ali alimshangaza mwandishi kwa ulimi wake wa kusoma Qur'an na kuzungumza Kiarabu.
Miezi michache baada ya kuzungumza na mimi wote wawili walifariki wa mwisho akiwa Sheikh Idrissa wakipishana kwa miezi michache.