Hili sharti kwenye APP ya CRDB Simbanking lina maana gani?

Hili sharti kwenye APP ya CRDB Simbanking lina maana gani?

Asamwa

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2012
Posts
3,711
Reaction score
2,462
Mimi ni mteja wa benki ya CRDB.

Kadi yangu ya benki imekwisha muda wake; hivyo jana nilikwenda kweny Tawi lao kwa ajili ya kupata kadi mpya.

Mhudumu wa benki aliniambia utaratibu wa kupata kadi mpya ni ku-apply kwa kutumia App ya CRDB. Nilifanikiwa ku-download App ila nilisita kukubali masharti kutokana na sharti moja ambalo ni: - “BENKI HAITAHUSIKA NA UPOTEVU UTAKAOTOKEA BAADA YA MTEJA KUTUMIA HUDUMA HII”.

Hili sharti limenishangaza sana! Ina maana kama ukitokea upotevu ambao mimi mteja sihusiki, ni nani atapaswa kuwajibika kama sio Benki?

Kama kuna wahusika wa Benki ya CRDB humu JF itakuwa vizuri wakatoa ufafanuzi kuhusu hili sharti.
 
Back
Top Bottom