Hili suala la kuonekana mamba Bahari ya Hindi lipo vipi?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
63,685
Reaction score
128,178
Wakazi na Wavuvi wa maeneo ya Vijibweni wamepatwa na taharuki baada ya fukwe za bahari katika maeneo hayo kuonekana ‘Mamba’ mkubwa anaetishia usalama wa maisha ya wakazi na wavuvi wa eneo hilo.

Baadhi ya wavuvi na wakazi wa eneo hilo wamezungumzia hofu na taharuki waliyonayo dhidi ya Mamba huyo, wakiongea na kipindi cha Drive cha East Africa Radio inayoruka kila siku za Jumatatu mpaka Ijumaa saa 10 jioni mpaka saa 2 usiku mmoja kati ya wavuvi hao, Athumani Ally amesema walitoa ushirikiano na wataalam wa wananyamapori lakini imeshindikana baada ya kuchana nyavu na kumpiga risasi mbili lakini hatukuweza kumkamata na amerudi tena baharini.

Kwa upande wa mtaalam wa Wanyama Pori bwana Sai Mahela Sabri ambaye ni afisa uhifadhi wa Wanyama Pori mkoa wa Dar es salaam ameongelea hilo jambo baada ya kufika eneo hilo na kushindwa kumpata moja kwa moja mamba huyo, Sai amesema kuwa hata wao imewashtua kwakuwa sio hali ya kawaida Mamba kukaa baharini.

“Kiukweli ata sisi imetushtua kukuta Mamba katika bahari maana inafahamika kuwa mamba anaishi maeneo ya maji baridi na kwa kawaida wanakuwa kwenye Maziwa au Mito lakini kwa kuwa hapa kuna mto mzinga inawezekana akawa anatokea kwenye mto huo na juhudi za kumtafuta mamba huyo bado zinafanyika”, amesema Sai.

bongofive

Yawezekana huyu Mamba nae 'katumwa' kwa Kazi 'Maalum' tu tena hasa Kipindi hiki cha Kampeni na tukiwa tunaenda 'Kumsulubu' Mtu Oktoba 28.
 
Ukiona hivyo ujue karibu Kuna makutano ya mto na bahari.

Hata mto rufiji maji yanapoingia baharini mamba wanakjaga sana na nishawaona mamba kwenye maji ya chumvi zaidi ya Mara 50.

Sema mamba asili yake syo maji chumvi na akija hakai sana anarudi alipotoka.

Kwa sisi Manguli wazee wa mishe Hali hiyo tunaona kawaida tu

Ova
 

Mbona 'Majibu' yako yana 'Mbwembwe' nyingi sana? Wewe ni 'Mhaya' Kikabila?
 
Na kuna yule alionekana pale darajani SINZA MUGABE
 
Na hilo ndio haswa jibu la hiyo sintofahamu,sema kuna watu kushirikisha bongo zao ni swala gumu mno kila kitu anataka kuleta JF
 
Ni ajabu kwa kuwa hatujazoea. Ukiangalia NatGWild utakuta sehemu fulani za Australia hilo ni jambo la kawaida. Na mamba baada ya miaka mingi wamekuwa wazoefu wa maji chumvi. Huanzia pale penye makutano ya mto na bahari. Kule Latin America nako kuna papa wanao onekana kwenye mito kwa umbali mkubwa ndani ya mto.
 
Na hilo ndio haswa jibu la hiyo sintofahamu,sema kuna watu kushirikisha bongo zao ni swala gumu mno kila kitu anataka kuleta JF
Mto rufiji unapoingilia baharini kna tokeaga mamba sana Sema Hawana uwezo sana ya kukaa kwa muda mrefu kwenye maji ya chumvi huwa wanarudi kwenye maji ya mto

Ova
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…