Upungufu wa nguvu za kiume ni tatizo la kimfumo mzima wa mwili.Usidanganyike hata siku moja kuwa kuna ugonjwa wa kukosa nguvu za kiume,isipokuwa unaweza kuwa na ugonjwa au tatizo la msingi litakalopelekea kukosa nguvu za kiume.
Kwa hiyo bila kutibu tatizo la msingi linalokusababisha kukosa hizo nguvu utamaliza dawa zote bila mafanikio au utakuwa unatumia booster kwa siku moja na tatizo linaendelea kuwa palepale na kuwa kubwa zaidi.
Mfano unaweza kuwa na tatizo katika mzunguko wako wa damu,matatizo ya shinikizo la damu na moyo,magonjwa ya kisukari au vidonda vya tumbo n.k lazima tu nguvu za kiume zitapotea au kupungua automatically.Lakini pia kuna watu wana changamoto ya michango au chango la kiume na wakati mwingine ngiri bila kuelewa,hawa pia wako kwenye hatari ya kukosa nguvu za kiume na wakati mwingine uume kusinyaa kuelekea ndani na kuwa mdogo zaidi kuliko awali.
Wengine pia wana mapungufu ya vichocheo mwilini au homoni,lakini pia baadhi misuli yao ya uume ilishaleghea kwa sababu walifanya sana punyeto kwa muda mrefu na matokeo yake wanayaona sasa.
Ni lazima kujua chanzo na baada ya hapo ukitibiwa kikamilifu unapona kabisa na nguvu huwa zinalejea zenyewe automatically baada ya mfumo ulioathirika kukaa sawa.