Hili suala la uhamisho kwa watumishi linashangaza sana!

Black Walker

Senior Member
Joined
Oct 8, 2018
Posts
119
Reaction score
254
Nimeona tangazo la UTUMISHI kuhusu suala la uhamisho kwa wenza! Kiukweli inashangaza kuona tunaletewa drama na maisha yetu.

Wapo watumishi wengi ambao maombi yao yako UTUMISHI AU TAMISEMI yakisubiria approval ya makatibu wakuu kwa muda mrefu.

Je, hao nao waandike barua upya kwenda kwa waajiri wao kabla ya hiyo 05/10/2024 au waendelee kusubiria barua?

IMG-20240927-WA0009.jpg
 
Maisha ya utumishi wa umma bwana unaweza kujikuta umafikia umri wa kustaafu bado ujajenga kisa kuamishwa amishwa. Sasa mzaliwa wa Tabora kazi kapangiwa Mtwara anajikuta hana interest ya kujenga kule kwa sababu kwao ni tabora. Baada ya miaka kumi anaamishiwa mkoa wa Tanga nako anakuta hana interest anakaa miaka nane anaamishiwa iringa hvyo hvyo yani hakuna mpango wowote wa maendeleo nikuamishwa tu.
 
Habari za Muda huu.

Napenda kuwapongeza Ofisi ya Rais-Utumishi kwa kutoa tamo kwa watumishi wanaohitaji kukaa na familia zao karibu.

Lakini bado kuna changamoto na sintofahamu kwa watumushi wale ambao wamefikia hatua ya kupata vibali kwa njia ya mfumo wa kubadilisha.

Je, kundi hili ambalo linasubiri vibali vya uhamisho wa kubadilisha kutoka kwa Katibu Mkuu wa Tamisemi wasitishe zoezi na kuendelea na hili zoezi jipya ambalo mwisho ni tarehe 05 Oktoba 2024?

Naomba kujua zaidi.
 
Attachments

  • F09EC7B1-A17D-4AD9-BCF7-D21123171FF8.jpeg
    F09EC7B1-A17D-4AD9-BCF7-D21123171FF8.jpeg
    98.3 KB · Views: 18
Mkuu, hivi utaratibu wa kuandika barua ukoje..
Halafu kama mtu anataka kumfuata mkewe ambae anafanya biashara bila kusahau watoto inakuwaje hapa
Binafsi nina ndugu yangu nimemjazia kwenye mfumo anavigezo vyote vilivyoainishwa kwenye hili Tangazo jipya. Kwa sasa anasubiri Approval kutoka kwa Katibu Mkuu Tamisemi.
 
Kwa mtazamo wangu pamoja na kuwa huyo ndugu yako kaomba uhamisho kupitia mfumo na status ni kusubiri approval ya KM bora pia apeleke hizo taarifa zake kwa mwajiri kama tangazo linavyosema ili atege huku na huku.
 
Hiyo wizara wapewe mabachela. Wasipewe ma single parents. Nadhani nimeeleweka
 
Maisha ya utumishi wa umma bwana unaweza kujikuta umafikia umri wa kustaafu bado ujajenga kisa kuamishwa amishwa. Sasa mzaliwa wa Tabora kazi kapangiwa Mtwara anajikuta hana interest ya kujenga kule kwa sababu kwao ni tabora. Baada ya miaka kumi anaamishiwa mkoa wa Tanga nako anakuta hana interest anakaa miaka nane anaamishiwa iringa hvyo hvyo yani hakuna mpango wowote wa maendeleo nikuamishwa tu.
Uhamisho wa kuhamishwa hamishwa kwa jinsi iyo siku izi haupo. Mtumishi wa huma hasa waliopo mamlaka za serikali za mitaa unaweza kaa kituo kimoja hata miaka 20 na ukihamishwa unahimishwa hospital kijiji au shule una hamishwa humo humo ndani ya kijiji au kata au halmashauri iyo iyo au wilaya jirani. Uhamisjo wa kutoka mkoa A kwenda mkoa B ni mgumu sana labda uwe umeomba mwenyewe. Pengine watumishi wa mashirika ya umma ndo huamishwa jinsi ulivyosema na kwa miaka hii ni mara chache sana.

Kingine kuna faida kubwa sana mtumishi kuajiriwa mbali na mkoa wa background yake hii inajenga sana utangamano na utaifa. Tanzania imefaidika sana na mfumo huu tofauti na kenya
 
Ni kweli kabsaa, inapunguza na uzembe kazini, mara leo naenda kumwangalia flan wa ndugu yangu anaumwa mara bibi kaletwa hospital yuko hoi, mara vikundi vya ujima hasa wazawa, mara kitchen party, yaani shughuri za kijamii kibao lkn wewe kama sio wa eneo husika/mkoa/ wilaya mambo mengine utayasikia tu wewe ni kazi tu.
 
Kingine imeondoa kma sio kupunguza ukabila.
 
Maisha ya utumishi wa umma bwana unaweza kujikuta umafikia umri wa kustaafu bado ujajenga kisa kuamishwa amishwa. Sasa mzaliwa wa Tabora kazi kapangiwa Mtwara anajikuta hana interest ya kujenga kule kwa sababu kwao ni tabora. Baada ya miaka kumi anaamishiwa mkoa wa Tanga nako anakuta hana interest anakaa miaka nane anaamishiwa iringa hvyo hvyo yani hakuna mpango wowote wa maendeleo nikuamishwa tu.
Binafsi huwa sipendi kukaa sehemu moja muda mrefu huwa nakuwa bored huwa nafurahia sana uhamisho wa mara kwa mara ni kama utalii fulani hivi
 
Hili tangazo limetoka ili kupitisha majina ya watoto wa wakubwa na uchaguzi mkuu. Baada ya hapo, utanikumbuka
 
Hii ni fani ya HR ni moja ya fani za kihuni sana nchi hii.Ninaamini tatizo linaanzia vyuoni.Kuna shida kubwa kwenye eneo la HRM kwani kwa asilimia kubwa imejaa binadamu wanaofurahia kuona watu wakiteseka na wao wakiwa kama miungu watu.
Kuna fani nyingine kama hizo lakini niligundua tatizo linaanzia vyuoni.Vyuo vyetu vikuu vinahitaji mapinduzi makubwa.
Kuna watu wapo huko wanajikuta ni miungu watu kwa kudhani wana akili za kipekee kumbe ni illusion tu.Mtaani kuna watu wana akili kuliko wao ila ni kwa vile kuna mgawanyo tu wa kazi na majukumu
 
Back
Top Bottom