Hili swala la kukusanya kodi mbona kama tunajichanganya wenyewe kama nchi

Hili swala la kukusanya kodi mbona kama tunajichanganya wenyewe kama nchi

covid 19

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2014
Posts
6,967
Reaction score
17,452
Hivi, najiuliza, inawezekanaje serikali yenye watumishi wengi na wenye taaluma za hali ya juu bado inashindwa kutatua tatizo la kwa nini Watanzania wengi hawalipi kodi? Hadi inafikia hatua rais kuunda tume maalum ya rais kwa ajili ya kutoa ushauri juu ya masuala ya kodi.

Mimi si mtaalamu sana kwenye sekta hii, lakini binafsi nadhani ni vigumu sana kupata kodi kutoka kwa watu wengi wakati watu wengi bado wanatumia malipo ya cash kulipana.

Kwa nini tusifikirie kuajiri taasisi kutoka mataifa yaliyoendelea, ambayo yana uzoefu mkubwa kwenye mifumo ya kisasa ya ukusanyaji kodi? Taasisi hizo zinaweza kuja, kutathmini mazingira yetu na vipato vyetu, na kutupa mapendekezo sahihi ya jinsi gani tunaweza kukusanya kodi kwa ufanisi, kutoka kwa watu wengi, kwa kutumia mifumo ya kisasa na iliyothibitika.

Hizi tume za ndani zinazoundwa kila leo mbona tija yake ni ndogo sana.
 
Back
Top Bottom