Hili tatizo linaigharimu Simba ila halizungumzwi

Singasinga

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2011
Posts
2,711
Reaction score
3,279
Habari wakuu,

Unapopanga kikosi kuna kitu kinaitwa team balance.

Tangu kocha Robatinho aje amekua akimtumia Chama kama winger kitu ambacho kinaiathiri sana team hadi kupelekea hata mechi ya juzi na Azam kufungwa goli la kipumbavu kisa waliambiwa wapige mipira mirefu kuelekea upande alioko chama na wakati inajulikana wazi Chama hana energy ya kugombania mpira na kukimbia.

Hiyo inapelekea muda mwingi lile eneo linabaki tupu labda Tshabalala ndo akipata nafasi anapatumia ila chama mda wote anapakimbia na kuja kurundikana humu kati alipo saidoo na bahati mbaya saidoo nae hajiongezi kwenda kucover kule.

Swali ni je kwanini kocha asiwe anampanga huko Saidoo ambaye angalau yeye anaweza kufanya operation zake akitokea huko tofauti na Chama ambae yeye ni mzuri akiwa humo shimoni hapo ni kama team ina watu9 maana kuna side tayari ina udhaifu haiwezi zalisha kama inavopaswa.

Pamoja na madhara yaliyojitokeza juzi nlishangaa kuona bado mipira mirefu ikawa inapigwa huko huko alipo chama ambapo ndo mpira ulichukuliwa ukazaa goli la mapema.


Sijawahi sikia wachambuzi wa bongo iwe humu au kwenye radio wakiliongelea hili zaidi ya kelele tu na kuishia kuongelea akina Bocco tu.

Naomba kuwasilisha.
 
Well said, very good point

Na ichi ndicho kinacho wagharimu sana Simba. Ni either Saidoo awe anatokea pembeni kama alivyokua anafanyaga mara Nyingi Yanga au mmoja kati ya Chama na Saidoo awe anaanza.
 
Well said, very good point

Na ichi ndicho kinacho wagharimu sana Simba. Ni either Saidoo awe anatokea pembeni kama alivyokua anafanyaga mara Nyingi Yanga au mmoja kati ya Chama na Saidoo awe anaanza.
Inawezekana kuna matatizo mengine ila hili kiukweli naliona liko wazi kibaya halizungumzwi wala halifanyiwi kazi.
 
Kocha wa simba anataka team ishambulie kutokea pembeni kitu ambacho ni ngumu kwa simba kwani falsafa ya simba ni kushambulia kupitia viungo sasa pembeni ni ngumu waliomleta kocha hawakuangalia hlo kwamba haendani na falsafa ya simba mda wote anabutua tu kama chandimu

Sent from my SM-N950F using JamiiForums mobile app
 
Well said, very good point

Na ichi ndicho kinacho wagharimu sana Simba. Ni either Saidoo awe anatokea pembeni kama alivyokua anafanyaga mara Nyingi Yanga au mmoja kati ya Chama na Saidoo awe anaanza.
Kocha alijaribu kumuweka Chama benchi, sisi washabiki tulisemaje??????
 
Sio lazima awekwe benchi,arudishwe humo shimoni anapopaweza then huyo saidoo ndo wamjaribu huko pembeni
Kocha ana version yake ya Simba anayoitaka, ila ametukuta sisi na ile version yetu tuliyoizowea. Hivyo ili kutufurahisha anajikuta anaidhohofisha team.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…