Hili ya Simba na Yanga utalielewa vizuri ukishaona uhusiano uliopo kati ya sayansi na maisha

Hili ya Simba na Yanga utalielewa vizuri ukishaona uhusiano uliopo kati ya sayansi na maisha

Jack Daniel

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2021
Posts
2,912
Reaction score
12,904
Habari ndugu zanguni.
Hope jumapili iko poa kabisa.

What is Science?

Hili ni swali ambalo wanafunzi wa kidato cha kwanza hupambana nalo pindi tu wakianza masomo ya secondari .

Jiografia ni sayansi,
Hesabu ni sayansi,
Kila kitu ni sayansi

Kuna ile Human and economics activities, yaani shughuli zote zinazofanyika ni Sayansi

Definition ziko nyingi kulingana na mazingira na aina ya shule au wakufunzi lakini maana huwa ileile kwani hakuna anayetoka kwenye mstari.

Wakuu maisha yote na kila tufanyacho kinahusisha sayansi moja Kwa moja,bila science hakuna maisha,uongozi,utawala,maamuzi,ubunifu na vingine vingi

Sayansi hiiihii ipo kwenye siasa pia,
Naam, Political Science,hii imewawezesha watawala wengi kuwacontrol watu wao bila kutumia nguvu kubwa ,ikiwa ni pamoja na kucheza michezo fulani na kufanikisha azma fulani bila kujulikana ama kutumia mabavu.

Ni rahisi kuwatuliza wananchi Kwa kuwachinjia nyama tu na kuwarudisha kwenye reli (ama kweli adui muombee njaa)

Lakini pia ni rahisi kusimamisha Treni lenye abiria mianne ili liwasubiri abiria wawili tu,kama unahisi haiwezekani,basi huijui sayansi.

Miaka fulani kule kijijini kwetu ilikuwa Baba anaweza kuagiza kuku achinjwe na aandaliwe lakini hakuna aliyethubutu Kula nyama ikiwa Baba hajarudi,kwanza mama haruhusu,ila atawaambia bado haijaiva,na ikiiva atawaambia kuna vingi sijaweka ,mpaka mwenye mji Baba arudi toka kwenye mihangaiko yake ,
Kwa miaka hii ni kama uonevu na ubabe wa kizamani lakini Kwa miaka ile ilikuwa ni kawaida tu japo manung'uniko yalikuwepo,lakini mnajisemea moyoni tu.

Yaani mababa walishaset standards zao,kiasi cha huo utaratibu kufuatwa.
Ni mahesabu madogo Sana yalitumika ili kuweka kautawala fulani kwenye familia.

Mtalaumu Yanga,
Mtalaumu Simba,
Mtalaumu TFF,
Mtalaumu TPLB ,

Lakini hata wao hawana nguvu na mamlaka kwenye utawala,lazima watii Sheria bila shurti ,tutaongopewa mengi kama mtoto anayesubiri chakula kabla ya wakubwa,ataambiwa bado hakijaiva mpaka wenye mamlaka wakirudi kila kitu kitakaa sawa. Najua tuna hasira lakini tutatulizwa na mnofu fulani utakaofyonzwa Kwa dakika 1,Kwa
 
Haha! Nilishawahi kuandika humu kuwa nchi hii inaongozwa na wafanyabiashara pamoja na ma masterminder ambao ndo haohao wanasiasa na wenye pesa zao!, yule tajiri alietekwa akapatikana michezo hii ndo anaipenda sana!..
Mtapiga zogo sana kwenye vyombo vyote vya humu ndani hakuna kitatokea!, kwasababu pesa inafanya kazi ukilambishwa unaufyata!.

Ndio maana sikuhizi wamezaliwa "machawa" kwasababu wamejua akili za maboss wanataka watu wa namna hiyo!.. huu ni ugonjwa mmbaya sana na ikiendelea hivi taifa litakuja kulipa kwa haya yanayotokea leo!.
Kama hakuna thinker tankers wa kubadilisha haya niwaambie tu kama taifa basi kitakuwa kimetulamba sana itakuja ku gharimu damu!.
 
Back
Top Bottom