Greatest Of All Time
JF-Expert Member
- Jan 1, 2017
- 23,620
- 52,790
bila kupoteza muda, Himid Mao Mkami ni mmoja kati ya viungo bora wa kukaba kuwahi kutokea nchini Tanzania kando ya akina Athuman Idd Chuji, Selemani Matola na hata Shaaban Nditi.
Himid amekuwa kwenye ubora wa kipekee kwa misimu kadhaa sasa, licha ya uwezo wake mkubwa alionao katika kuzuia mashambulizi ya wapinzani pia ana uwezo wa kushambulia kwa kupiga pasi maridadi na hata kupiga makombora hatari kwenda langoni mwa adui. Ni mmoja kati ya box to box midfielders waliokamilika katika nchi yetu.
Pamoja na yote hayo, Himid nje ya Chamazi na Azam yake, hana ustaa wowote, hatukuzwi, hapewi sifa kama wanavyopambwa wachezaji kadhaa wa kigeni ambao wengine hawafikii hata robo ya Himid.
Ni wakati sasa wa kuamka na kuanza kutambua uwezo wa Himid, tusingoje mpaka astaafu ndio tuanze kumtukuza au mpaka ahamie Simba na Yanga ndio tuanze kumuimba?
Povu ruksa.