Himid Mao Mkami: Mchezaji asiyeimbwa Tanzania

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2017
Posts
23,620
Reaction score
52,790
bila kupoteza muda, Himid Mao Mkami ni mmoja kati ya viungo bora wa kukaba kuwahi kutokea nchini Tanzania kando ya akina Athuman Idd Chuji, Selemani Matola na hata Shaaban Nditi.

Himid amekuwa kwenye ubora wa kipekee kwa misimu kadhaa sasa, licha ya uwezo wake mkubwa alionao katika kuzuia mashambulizi ya wapinzani pia ana uwezo wa kushambulia kwa kupiga pasi maridadi na hata kupiga makombora hatari kwenda langoni mwa adui. Ni mmoja kati ya box to box midfielders waliokamilika katika nchi yetu.

Pamoja na yote hayo, Himid nje ya Chamazi na Azam yake, hana ustaa wowote, hatukuzwi, hapewi sifa kama wanavyopambwa wachezaji kadhaa wa kigeni ambao wengine hawafikii hata robo ya Himid.

Ni wakati sasa wa kuamka na kuanza kutambua uwezo wa Himid, tusingoje mpaka astaafu ndio tuanze kumtukuza au mpaka ahamie Simba na Yanga ndio tuanze kumuimba?

Povu ruksa.
 
Wachezaji wazuri wapo simba na yanga
 
Mpira ni nyota, kama huna hataa ujtahidi vp huwezi onekana.
 
Ila tu kama sijakosea, ndio Captain Msaidizi wa National team.
 
Kinachomponza Himid ni kucheza Azam basi, ni kweli himid ni mmoja kati ya wachezaji mahiri hapa Tz, ila sasa soka letu limetawalwa sana na hawa Kulwa na dotto... Simba na Yanga ndio maana hata himid wengi wao hawamjui
 
Bado sioni ubora WA himidi mao. Kwanza ni mchezaji mwenye hasira timu ikifungwa.
 
Kinachomponza Himid ni kucheza Azam basi, ni kweli himid ni mmoja kati ya wachezaji mahiri hapa Tz, ila sasa soka letu limetawalwa sana na hawa Kulwa na dotto... Simba na Yanga ndio maana hata himid wengi wao hawamjui
Kweli mkuu,ona jina la Aishi Manula linavyorindima leo.juzi nilipita kijiji kimoja nikakuta madogo wanapiga ndondo. Nikawauliza aka zao,mmoja akasema Kichuya na kipa akasema Ishi Man
 
Nikusahihishe tu mleta Uzi himid kwa sasa anachezeshwa kama beki wa kulia ilianzia game ya taifa stars vs Benin ikaja kuendelea katika michuano ya cecafa Kenya na tangu arudi azam kachezeshwa kama beki wa kulia sio lengo langu kuwakosoa walimu wake wanaomfundisha kuanzia azam had taifa stars ila nadhan haikuwa nafasi sahihi kwake maana wot tunajua ubora wa himid katika eneo la kiungo!!!


Nb:- kiungo bora wa kati kwa sasa ni hawa kwa maono yangu
1. Mkude (Simba)
2. Himid (azam)
3. Mudathir (singida)
4. Pius buswita (yanga)
5. Jumanne elfadhili ( prisons)
 
Wacha kusifia bure,,, hemed mao sio fundi wa mpira,,, HANYUMBULIKI..... sifa za kiungo hana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…