Hip hop ni America tu anayebisha nani?

Najuwa lengo la thread ni kupromote jina la Diamond ili ujio wa mwana Daresalame usimfunike jumla, labda tuanze kwa wewe kutueleza Diamond anapiga category ipi ya muziki?
nipeni link huo wimbo wa mwana dar es salaam mbona siupati
 
We boya kweli,unajua mtu wa kwanza kutoka tanzania kushiriki cypher ya BET n msanii wa hiphop from A town njoo kiringeni ukutane na wakali tamaduni music msasani clubs likiongozwa na nikki mbishi,daimond anajua anajulkana ndyo n kufanya vzur ila co kudharau hiphop,
 
Asili ya hip hop ni Mmarekani mweusi aliyepelekwa america km mtumwa........
 

Mkuu utafiti wako ni batili karudie tena.

i) Kwenye wekundu una maana gani? Ina maana ukifanya hip hop na wewe si Mmarekani inakuwa sio hip hop?

ii) Kwenye bluu ni upotoshaji mkubwa, ungekuwa umefanya utafiti wako kwa umakini ungejua kuwa Drake na
Kardinal Offishall wanatoka Canada, Iggy Azalea anatoka Australia, Slick Rick, Miss Dynamite na Monie Love
wanatoka UK, Knaan anatoka Somalia ( via Canada), Supreme NTM ni Wafaransa.

iii) Kwenye Kijani ukiacha Knaan wengine ni kama Ice Prince na Str8Buttah ( Nigeria), Sarkodie (Ghana) na Pro Kid na Trusenz (South Africa).
 
mbona Sarkodie from Ghana anavuma sana mpaka huko America
 
Kumradhi bwana mgonjwa ila unaonekana mgonjwa kweli kweli..........ni hivi kwenye ile project ya R.kelly na one 8 ya hands across the world......hip hop iliwakilishwa na msanii NAVIO wa uganda kama sio kenya maana sina uhakika ni mkazi wa nchi gani kati ya hizo mbili. Bt anaimba hip hop,jambo la pili kukusaidia wasanii wengi wa bongo wanatatizo la kutojielewa wanafanya staili gani ya mziki ....mfano;madee haeleweki kuwa anafananya rap au anafanya mdumange Ney wa mitego pia anaugonjwa huo huo wa kuswichi style hana msimamo,......bt kukusaidia diamond kwa asilimia kubwa nyimbo zake kwa sasa anaimba african pop kwa.Na kuhusu hip hop kutokufanya vizuri kimataifa tatizo si aina ya muziki tatizo ni wasanii wetu hawajajiset kufanya project zenye kuvuta hisia za kimataifa sababu hip hop na hata mziki mwingine wowote unategemea zaidi research sana ili kuwa na tungo,maneno ya kiufundi na hata presentation ya kueleweka kimataifa....so please dont blame it on the game,.........blame it on the player.
 
Ukikubali kuwa mnyama hata uimbe kwaya kwa gwajima utatoka tu.
 

Mkuu umempa za ndani sana hawezi kuwajua hao huyu ni kizazi cha mulugo division five.

~Umenikumbusha long sana Chucan sa Mafia The Firm Baby.
 
Drake mkanada,Wale mnigeria,Jcole ni Mixer wa african-american+Germany na amezaliwa ujerumani wote wanahiphop na wanajulikana world wide labda wewe ulieyezaliwa 1997 unamjua diamond tu,Album ya Nas - It was written inatoka ulikuwa ujazaliwa,2pac anakufa haujazaliwa wakati big anakufa bado haujazaliwa!! Hivi vizazi vya mulugo ni sheeedaa.
 
nipeni link huo wimbo wa mwana dar es salaam mbona siupati

Km hauupati ujue hauhiti....mi mwenyewe toka utoke sijawahi kuusikia,lakini akitoa Diamond siku moja tu naupata kwa waendesha bodaboda
 
mimi naukubali sana huu mstari mimi ni bandubandu na wewe ni gogo ntakubandua mgonjwa upo hapo?
 
Hip hop ni muziki wa wamarekani weusi, ukibisha we bisha tu lakini huu ndo ukweli. Kwenye huu muziki wanaimba kuhusu mazingira na maisha yao, na soko la huu muziki lipo huko huko kwao. Kuna manguli wa hip hop kutoka ulaya kama Tinie Tempah na wengineo mpaka wamekwenda kuomba collabo unyamwezini ndio wanaonekana na sijui kama wana maisha marefu kwenye fani. Sasa we ukae bongo uimbe sijui kuhusu karafuu, watakusikiliza uko uko kwenu Pemba.
 
ukishapata jina ni rahisi kufanya harakati zingine...unafikiri mrII katika hali ya kawaida angeweza kuwa mbunge..?

pia ni ukweli kwamba wanaoimba wanauza zaidi hata mamtoni...huwezi linganisha celine dione na jayZ kwa mauzo ya mziki...ingawa jiga ana mawe zaidi sababu ya biz za pembeni...sasa hawa wakwetu hapa nao inabidi wachakarike
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…