Hipi ni sawa.............?

only83

JF-Expert Member
Joined
Oct 15, 2010
Posts
5,343
Reaction score
2,527
Nimekuwa napata shida watu wanaporipoti ajali.....Je ni,Watu wamekufa katika ajali au watu wameuwawa kwenye ajali...msaada samahani...
 
Mimi nadhani neno kuua/kuuawa linahusiha nia mbaya/tendo baya kuwapo kama kisababishi. Iwapo ni ajali ya kweli neno kufa naona linafaa zaidi.
 
Ajali husababibsha vifo ama ulemavu. Hivyo mtoa taarifa anaweza kusema ajali hiyo imesababisha vifo vya watu kadhaa. Ama kusema hivi, kutokana na ajali hiyo watu kadhaa wamepoteza maisha yao.
 
Mara nyingi kuuwawa ni tofauti na ajali, nadhani anaweza kusema kutokana na ajali fulani kutokea mahala fulani watu kadhaa wamepoteza maisha.

Na kingine hiyo title yako sio Hipi ni Ipi
 
DA umeona eeh! red..Kiswahili sahihi ni kupotesha maisha, kufa..sio kuuwawa ni kifo cha kukusudiwa yaani mfano mtu fulan kumuua mwenzako kwa sababu fulani..labda jambazi anavyokuwa anapambana na polisi halafu polisi wakifanikiwa hapo tunaweza kusema ameuwawa na polisi au majambazi..nawakilisha tuu jamen..
Mara nyingi kuuwawa ni tofauti na ajali, nadhani anaweza kusema kutokana na ajali fulani kutokea mahala fulani watu kadhaa wamepoteza maisha.

Na kingine hiyo title yako sio Hipi ni Ipi
 


Na pia sio kupotesha ni kupoteza!!!!!!!!!!! Tehe tehe haya mambo ya kiswahili ni magumu sana inabidi vingine tujue kuwa ni typing error
 
Hicho kichwa cha habari pia umekikosea, Hipi = Ipi
 
kama kifo kimetokana na ajali neno kufa au kupoteza maisha ni sahihi. ila ukisema "wameuwawa" ni kama vile kuna kundi la watu fulani au wanyama wenye dhamana ya kutekeleza hayo mauwaji.
 
Kama ajali ilitokea kimakusudi ni rahisi na neno uwawa linaweza kutumika, kwani lipo katika kuonyesha hali, kimsingi maneno wamekufa, mawefariki, au wameaga dunia, ni maneno stahiki katika kuelezea habari juu ya ajali.
Silipingi neno wamepoteza maisha, bali sikubaliani nalo kwani si stahiki, na hii nikutokana na kitendo cha kupoteza humrejelea muhusika, ilhali tunafamu wahusika wote huwa wametendwa katika mzingira ya ajali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…