Hisa za mgodi sasa kugawanywa nusu kwa nusu

ndiyomkuusana

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
666
Reaction score
426
HATIMAYE Serikali imeamua kuvunja ukimya na kutoa uamuzi kuhusu sakata la umiliki wa hisa za mgodi wa madini wa Tanzanite One uliopo wilayani Simanjiro mkoani Manyara na kuamuru wananchi pamoja na kampuni hiyo kugawana “pasu kwa pasu” asilimia 50 kila mmoja.

Hatua hiyo imekuja baada ya mvutano mkubwa kuibuka kuhusu umiliki wa mgodi huo kufuatia wachimbaji wadogo kutaka wapewe asilimia 50 kuchimba madini hayo ya vito huku sheria mpya ya madini ikiwabana wawekezaji hao kutochimba madini hayo ya vito kwa asilimia 100 isipokuwa si zaidi ya asilimia 50 tu.

Hata hivyo,itakumbukwa ya kuwa,Rais Jakaya Kikwete aliwahi kutoa ahadi katika kijiji cha Lengast wilayani Simanjiro mkoani humo wakati akijinadi katika kampeni za uchaguzi mkuu mwaka 2010 kwamba angemegea wachimbaji wadogo eneo la mgodi huo mara baada ya wawekezaji hao kumaliza mkataba wao ulioisha mwezi machi mwaka huu. Akizungumza katika mkutano wa kumpokea na kumkaribisha nyumbani Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM),Abdulrahamn Kinana, Waziri wa Nishati na Madini,Sospeter Muhongo alitamka kuwa hivi karibuni suluhisho litapatikana ambapo wawekezaji hao watamiliki asilimia 50 na wachimbaji watapewa asilimia 50.

Waziri huyo alienda mbali zaidi na kusisitiza ya kuwa Serikali inaangalia uwezekano wa kumiliki asilimia 60 katika mgodi huo huku akisema wamejidhatiti kuhakikisha migodi yote inalipa asilimia 4 kama mrabaha.

Naye Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Stephen Masele alitamka kwamba Serikali itahakikisha Mkoa wa Arusha unakuwa Kituo cha Kimataifa cha Madini ya Vito.

Alisema kuwa Serikali iko katika mchakato wa kuhakikisha kituo hicho kinajengwa hivi karibuni huku akiwaonya wale watakaowawekea vikwazo vijana wanaofanya biashara ya vito vya madini hususani ya Tanzanite.


source. mwananch.17.12.12
 
Hilo ni zuri sana ....... lakini tunataka hilo lifanyike kwa migodi yote nchini..... wananchi kupitia serikali lazima wamiliki 51%.......
 
Hii mbona wamechelewa sana huku mbele mbele kama Botswana ndio mikataba wanayosaini ila sasa kwa sabubu kuna viongozi wetu walishakula mlungula na uadilifu wao ziro ndio maana hii inaonekana kama kitu kigumu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…