Hisa ni sehemu ya mtaji anayowekeza mtu kwenye biashara. Kwa mfano Kampuni inaweza kuanzisha biashara na mtaji wa Tshs. 100,000.00 na kuwa na hisa 100 zenye thamani ya Sh. 10,000 kila hisa. Hivyo ukinunua hisa 2 utalipa sh. 20,000.00. Biashara ya hisa hufanyika kwenye soko la hisa kupitia kwa wakala. Faida ya kununua hisa ni kupata gawio kutoka katika sehemu ya faida ilioypatikana pia kutokana na kupanda kwa thamani ya hisa wakati wa kuuza. Katika kununua hisa kama katika biashara yoyote unaweza kupata hasara.