Hisia na mziki enzi hizo na Angalieni Mpendu

Hisia na mziki enzi hizo na Angalieni Mpendu

Freetown

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2008
Posts
882
Reaction score
78
Huyu jamaa, Angalieni Mpendu alikuwa maarufu sana kwenye hisia na muziki kipindi kilichojichotea washabiki wengi kwa ule umahiri wake wa kupangilia stori na muziki, nilikuwa napenda sana kusikiliza kipindi hiki, kuna anayekumbuka au aliyekuwa na mapenzi na kipindi hiki??? tujikumbushe, yaani kama naweza kupanda CD au hata kanda zilizo rekodiwa nitafurahi kwa anayeweza zipata tuwasiliane
 
  • Thanks
Reactions: 3D.
mi nilikuwa mpenzi mkubwa sana wa kipindi hiki, lakini sikurekodi kanda hata moja, labda tutafute rekodi kwenye maktaba za RTD
 
mi nilikuwa mpenzi mkubwa sana wa kipindi hiki, lakini sikurekodi kanda hata moja, labda tutafute rekodi kwenye maktaba za RTD

Itakuwa poa sana mkuu, jitahidi kuulizia ukipata ni pm au weka hadharani kwa faida ya wote
 
Ah, acha tu. Nilikuwa primary school lakini nakumbuka ....."Kwa mara nyingine tena Redio Tanzania Dar es Salaam inawaletea Hisia na Muziki, msimulizi ni Angalieni Mpendu" nakumbuka ala ya kipindi inakaribia kufanana na solo gitaa kwenye wimbo wa Asha Bora wa Sikinde. Katika kipindi hicho ndiyo nilisikia kwa mara ya kwanza wimbo wa Sabalkheri Mpenzi wa kundi la Culture (Mila na Utamaduni-Zanzibar). Those days...Those days... no politics here but Nyerere was alive..... those days..
 
Back
Top Bottom