Historia chungu ya maisha ya taifa la Ukraine, Mapinduzi ya utu (Maidan Revolution) hadi uvamizi wa 2022

Historia chungu ya maisha ya taifa la Ukraine, Mapinduzi ya utu (Maidan Revolution) hadi uvamizi wa 2022

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Tangu kupata uhuru wake kutoka USSR mwaka 1991 Ukraine lilikuwa ni taifa linalopata viongozi wanaopokezana mitazamo na mielekeo wakipokezana kufungamana kati ya West (EU&US) au Russia kwa vipindi tofauti lakini kadri muda ulivyosonga mbele raia wengi wa taifa hilo walizidi kuwa na muelekeo wa West zaidi hali iliyopelekea bunge na urais kutawaliwa na viongozi wenye mtazamo na wanaotaka kufungamana na West zaidi kuliko Russia.

Mwaka 2010 akachaguliwa Viktor Yanukovych kuwa Rais wa Ukraine ambaye alikuwa ni Pro-Russia na mwenye maslahi binafsi ya biashara na Russia lakini bunge bado likawa na wabunge wengi zaidi ambao ni Pro-West. Yanukovych akaingia na malengo ya kufuta maendele yaliyopigwa kuelekea Ulaya na mtangulizi wake Viktor Yushchenko ambaye alikuwa Pro-West, tatizo likawa hakuwa na idadi ya wabunge wa kutosha kupitisha sera za kuilekeza Ukraine upande wa Russia.

Mwaka 2013 bunge la Ukraine likapitisha muswaada wa Ukraine kuingia mkataba wa kisiasa na biashara huru na Umoja wa Ulaya. Yanukovych akogoma kuusaini mkataba dakika za mwisho kabisa . November mwaka huo yakaibuka maandamano makubwa nchi nzima yalioendelea mpaka 2014.

Rais Yanukovych ambaye alikuwa ni Pro-Russia aliondolewa madarakani kwa maandamano ya raia nchi nzima baada ya kukataa kusaini mkataba wa biashara na EU na madai mengine yaliyofuatia ya waandamanaji kama kuporomoka kwa demokrasia, uhuru wa raia na kukithiri kwa rushwa.

Putin kuona Russia kapoteza mtu wake muhimu Kyiv akaanza kufanya vurugu Crimea na maeneo mengine ya Ukraine mashariki kisha akaingiza majeshi huko na sababu kubwa ya kushindwa kuzuiwa wakati huo ni serikali ya dhaifu ya Ukraine.

Baada ya hapo EU na USA waliwekeza pesa nyingu na utaalamu kuijenga serikali ya Ukraine na jeshi lake, Putin akaendelea kuona Ukraine ikizidi kuimarika, ikamtisha na akajua hataweza tena kuifanya koloni lake "vassal state" akaivamia nchi nzima wakati huu kwa lengo la kuweka tena kibaraka wake Kyiv, akakutana na jeshi lililoimarika zaidi kuliko la 2015, akapata upinzani mkali.Aliposhindwa lengo kuu akahamishia nguvu mashariki ili aigawe hiyo nchi asitoke mikono mitupu.

Matokeo yoyote yatakayopatikana baada ya mgogoro huu ikiwa Ukraine itaendelea kubaki taifa huru itakuwa ni ushindi mkubwa kwake.
 
Kwani ni sababu zipi zilimfanya Russia kutoa majeshi yake Kyiv na kuyapeleka mashariki mwa Ukraine?[emoji848]
Wao Russia lengo lao kuu ni huko Donbass.kupiga kiev na maeneo mengine ni danganya toto.pia ni vizuri kujua kuwa hadi sasa Russia anatumia silaha nyepesi kabisa.Russia akiamua vita inaweza kuisha hata kesho.
 
Anhaa asante pia kwa majibu yako👍 . Ila lengo langu lilikuwa majibu yatoke kwa mtoa mada
 
Kujua hataweza kuichukua Kyiv kwa namna yoyote ile bila umwagikaji damu mkubwa na kuigeuza Kyiv majivu pamoja na wanajeshi wake.
Kwani ni sababu zipi zilimfanya Russia kutoa majeshi yake Kyiv na kuyapeleka mashariki mwa Ukraine?[emoji848]
 
Kujua hataweza kuichukua Kyiv kwa namna yoyote ile bila umwagikaji damu mkubwa na kuigeuza Kyiv majivu pamoja na wanajeshi wake.
Hii ndio sababu kuu iliyomfanya Russia kuondoa majeshi yake Kyiv na kuyapeleka mashariki mwa Ukraine 🤔
 
Yoda,

Kwa Historia hii nakupa 21%.

Huna tofauti na wale wanaochakachua Historia ya Zanzibar.

Kuna mambo mengi umeyaacha ili uinufaishe Ukraine kwa historia iliyoficha baadhi ya mambo ya msingi.
 
Badala ya kupiga porojo ungeleta hayo mambo niliyoficha
Yoda,

Kwa Historia hii nakupa 21%.

Huna tofauti na wale wanaochakachua Historia ya Zanzibar.

Kuna mambo mengi umeyaacha ili uinufaishe Ukraine kwa historia iliyoficha baadhi ya mambo ya msingi.
 
Back
Top Bottom