Ralph Tyler
JF-Expert Member
- Jul 31, 2015
- 2,828
- 3,579
Asante kwa kutukumbusha kwa usahihi. Mimi pia nilikuwa miongoni mwa wachangiaji wa mwanzo kule bcstimes na akina Mzee Sam, Mzee ES, mkandara, etc. Nikiwa na id nyingine of course.Nadhani Ilikuwa inaitwa Bstimes kwa sababu huko ndipo nilipoanzia hii mijadala ya tanzania online. Kulikuwa na watu kama marehemu Simba, Mwapachu na wengine ambapo mijadala ya wakati ule ilikuwa ni ya kiutu uzima sana kabla ya uchaguzi wa 2005.
Naikumbuka "Darhotwire"ilikua ya moto. Tumetoka mbali na bado safari ni ndefu . "Kweli tutafika Kisiwa cha Salamani?"Kabla hata ya jamboforums
Wadau tulikuwa na Darhotwire
Na Darhotwire.com chini ya East Africa RadioNinavyokumbuka, JamboForums (mtangulizi wa JamiiForums) ilikuja kujaza nafasi ya ombwe lililoachwa na nyenzi_dot_com; mahali ambako wahenga wa mtandaoni tulikuwa tukikutanika kwa midahalo motomoto...
Iko too shallow fanya utafiti kidogo uiboresheJamiiForums ni tovuti ya mtandao wa kijamii iliyoko nchini Tanzania iliyoanzishwa mnamo mwaka 2006.
Na Mwanzilishi wake Maxence Melo Mtandao huo ni jukwaa maarufu mtandaoni.
Ukurasa wa kwanza wa JamboForum kabla ya kubadilika kuwa JamiiForums
JamiiForums ilizinduliwa rasmi mnamo Machi 2006 kwa jina la JamboForums, na ilikuwa na vikao kadhaa mkondoni. Mnamo Mei 2008 walibadilisha jina na kuwa JamiiForums kutokana na masuala ya hakimiliki.
Mnamo Machi 2016, Jamii Media iliwasilisha kesi dhidi ya jeshi la polisi la Shirikisho la Tanzania, ikidai matumizi ya nguvu ya jeshi la polisi kutaka habari za binafsi za watu wanaoshukiwa kuhusika na uhalifu ni kinyume cha katiba. Kesi hiyo itashughulikiwa kupitia Mahakama Kuu ya Tanzania.
Hiyo ni kwaufupi Sana Kama nilivyo sema
SOMA hii interview na Maxence Melo: Exclusive Interview with JamiiForums' founder - Maxence Melo: The history and operations of the platform