Historia fupi ya mkoa wa sasa wa Shinyanga na wenyeji wake Tanganyika

Historia fupi ya mkoa wa sasa wa Shinyanga na wenyeji wake Tanganyika

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2018
Posts
21,711
Reaction score
35,644
Historia ya mkoa wa Shinyanga inaanza hata kabla ya wakoloni kuitawala Tanganyika mwaka 1890's-1961.

Wakoloni wa kwanza kutawala eneo la sasa la mkoa wa Shinyanga walikuwa ni wajerumani walioanza kutawala mwaka 1890's hadi waliposhindwa kwenye vita ya kwanza ya dunia mwaka 1918.

Wajerumani walipoingia na kuitawala Tanganyika walikuta eneo la sasa la mkoa wa Shinyanga linakaliwa na watu wa makabila ya Wasukuma, Wanyamwezi, Wasumbwa, Walongo na Watusi.

Katika utwala wa Wajerumani, waliweza kuigawa Tanganyika katika maeneo madogo ya kiutawala yanayoitwa Wilaya, ambapo eneo la sasa la mkoa wa Shinyanga lilikuwa ndani ya wilaya ya Tabora chini ya mkuu wa Wilaya anaye wajibika kwa Gavana wa Tanganyika.

Mara baada ya kuisha kwa vita ya kwanza ya dunia, Waingereza walianza kutawala eneo la sasa la mkoa wa Shinyanga kuanzia mwaka 1920 hadi wakati wa uhuru wa Tanganyika mwaka 1961.

Mara baada Tanganyika kupata Uhuru 1961, ilipofika mwaka 1963 wilaya ya Tabora iligawanywa na na serikali ya Jamhuri ya Tanganyika na kuzaa mkoa wa Tabora na Shinyanga.

#ASILI YA JINA NDAKI NA NGEREJA USUKUMANI WAKATI WA UKOLONI 1980's-1961.

Wakati, Wajerumani wanaingia usukumani kutawala walionekanani wakali na wakorofi sana.

Jambo ambalo wasukuma wakanda zote liliwafanya wawabatize kwa jina la "Bhadaki" wakiwa na maana ya Wakorofi/Wakali.

Hivyo Katika kipindi cha Wajerumani watoto wengi wa kiume waliozaliwa walipewa majina la "NDAKI".

Pia Katika kipindi cha Utawala wa Waingereza, Wasukuma walishindwa kutamka Waingereza badala yake wakawaita "Bhangereja."

Hivyo watoto wengi wakiume waliozaliwa Katika kipindi cha utawala wa Waingeraza walipewa majina ya "NGEREJA".

#ENEO LA SHINYANGA CHINI YA WATEMI(BHATEMI).

Kabla ya kuja kwa wakoloni eneo la mkoa wa Shinyanga lilikuwa chini ya watawala wa jadi wanaoitwa Watemi(Bhatemi)

Kila mtemi alimiliki eneo lake lenye mipaka linaloitwa Utemi(Bhutemi).

Mkoa wa Shinyanga ulikuwa chini ya watemi kutoka kabila la Wasukuma, Wanyamwezi na Wasumbwa.

Mfano eneo kubwa la wilaya ya Shinyanga na Kishapu lilitawaliwa na watemi(Bhatemi) wa kabila la wasukuma.

Eneo la wilaya ya Kahama lilitawaliwa na na watemi wa kabila la Wanyamwezi na eneo la Ushetu lilikaliwa na watemi wakabila la Wasumbwa.

#Ntemi Ng'hwaya Ng'wandu-BUSIYA
#Ntemi Kishimba -KAHAMA
#Ntemi Magope-USHETU

#Karibuni kwa nyongeza na kuboresha mapungufu ya makala hii.

#Imeandikwa na Mjukuuwa Nshimba ya Nyawa kutoka Nzega-Tabora.
FB_IMG_1577683668860.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Natarajia kujifunza mengi sana.

Lakini bado sijapata mantiki ya Watoto kuitwa majina ambayo asili sio ya Kisukuma kama hayo Ndaki!!

Lakini pia nataraji kujifunza asili ya neno shinyanga.

Haya ndio maoni yangu
 
Natarajia kujifunza mengi sana.

Lakini bado sijapata mantiki ya Watoto kuitwa majina ambayo asili sio ya Kisukuma kama hayo Ndaki!!

Lakini pia nataraji kujifunza asili ya neno shinyanga.

Haya ndio maoni yangu
YASEMEKANA KULIKUWA NA MIMEA MINGI IITWAYO "inyanga"-umoja na "manyanga" -uwingi. Kutokana na ugumu wa kutamka "Hinyanga" (Penye inyanga) kwa walowezi wa kizungu,waliishia kuita "SHINYANGA'
 
Jina Shinyanga linatokana na jina la mti mkubwa sana uliokuwa pale uliokuwa unaitwa Hinyanga.
 
Serikali ingeangalia jinsi ya kurudisha majina kama yanavyopaswa kutamkwa na wenyeji tofauti na wakoloni walivyoyaandika.
 
Hujaeleza vizuri kuhusu mkoa wa Shinyanga kabla ya uhuru. Ni kwamba eneo la Wilaya ya Kahama, Bukombe na Mbogwe yalikuwa upande wa Jimbo la magharibi wakati huo ilikuwa wilaya ya Kahama tu kabla ya Bukombe na Mbogwe kuwa wilaya. Jimbo la magharibi makao makuu yake yalikuwa Tabora na lilijumuisha wilaya za Tabora, Nzega, Mpanda, Kasulu, Kigoma na Kibondo. Eneo la Wilaya ya shinyanga, kishapu na mkoa wote wa Simiyu yalikuwa upande wa Jimbo la Ziwa ambalo makao makuu yake yalikuwa Mwanza. Wilaya za wakati huo zilizokuwa chini ya Jimbo la Ziwa ni Mwanza, shinyanga, Maswa,Kwimba, Geita, North Mara, South Mara, Ukerewe, Biharamulo, Ngara, Bukoba na Karagwe. Mwaka 1959 jimbo hili liligawanywa na kuzaliwa Jimbo jipya la Ziwa Magharibi lenye wilaya za Bikoba, karagwe, ngara na Biharamulo.

Tanganyika ilipopata uhuru mwaka 1961 kulikuwa na majimbo 9 tu nchini Tanganyika nayo ni mashariki, ziwa, ziwa magharibi, kaskazini, magharibi, nyanda za juu kusini, kati, kusini na Tanga. serikali uhuru ya Tanganyika mwaka 1963 ikaamuwa kuanzia mikoa mingine kutoka tisa hadi mikoa 17 mwaka 1963. Ndipo mkoa wa shinyanga ulipoanzishwa kwa kuchukua wilaya mbili (shinyanga na maswa) kutoka jimbo la ziwa na wilaya ya Kahama kutoka jimbo la magharibi na kuunda mkoa wa Shinyanga.

Pia siyo kweli kwamba wakati wa utawala wa wajerumani Kahama ilikuwa iko chini ya wilaya ya Tabora. Ukweli ni kwamba Kahama ni wilaya iliyoanzishwa na wajerumani na ilikuja kuzaa wilaya ya Nzega mwaka 1928 wakati wa utawala wa mwingereza ila ilikuiwa jimbo la magharibi makao makuu yakiwa Tabora kama nilivyoeleza hapo juu.

Ila ni ukweli kwamba wakati wa utawala wa Wajerumani wilaya shinyanga ilikuwa Chini ya jimbo la magharibi lenye makao makuu Tabora lakini wakati wa utawala wa Waingereza ilihamishiwa jimbo la ziwa lenye makao makuu mwanza. Waingereza ndio waliotenga eneo la unyamwezi na usukuma(sukumaland) na mpaka ukawa mto manonga. Ndio maana Wilaya za Kahama na Nzega zilihesabika ni unyamwezini. Ukiwa barabara kuu ya shinyanga/nzega ukifika Tinde na ukavuka mto manonga tayari unafika unyamwezini(nata). Na ukiwa kwenye train ukifika stesheni ya isaka ukavuka mto manonga ukafika Lohumba tayari umeingia sukumaland na Isaka inabaki unyamwezini. Hapo nimekuongezea mnofu katika ulichokusudia kukielezea.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama sijasahau; Shinyanga inatokana na jina la mti mkubwa sana uliokuwa pale uliokuwa unaitwa Hinyanga.
Ukweli ni kwamba mahali ilipo Shinyanga ya sasa maeneo ya mtaa wa Kambarage kulikuwa na mti mkubwa unaoitwa "inyanga", mti huo ilikuwa unatumika sana kama ukumbi wa mikutano yote katika eneo hilo. Watu walikuwa wakialika mikutano walikuwa wanasema mkutani utafanyikia kwenye mti wa inyanga yaani kwa Kisukuma walisema " dugumanhija h'inyanga makanza asa'ibili" kutoka na ugumu wa kutamka "h'inyanga" Wakoloni wakaongeza S ikawa Shinyanga!
 
Back
Top Bottom