Historia Fupi ya Mwanamapinduzi Che Guevara, Alivyokamatwa na Kuuawa Kikatili

Historia Fupi ya Mwanamapinduzi Che Guevara, Alivyokamatwa na Kuuawa Kikatili

geophrey140

Senior Member
Joined
May 4, 2013
Posts
134
Reaction score
208
7003eeb104771128658741825ca5e777--ernesto-che-che-guevara.jpg

Jina kamili : Ernesto Guevara

Kazi : Daktari, mwanamapinduzi wa kijamaa (marxist)

Uraia : Argentina

Kuzaliwa : June 14 1928

Kufariki : October 9, 1967 ,Bolivia milima ya La heguera

Chanzo cha kifo : kuuwawa kwa kupigwa risasi

Kama kijana msomi wa shahada ya udaktari, che Guevara alisafiri nchi nyingi sana huko bara la Amerika ya kusini na rafiki yake, akawa ni mtu mwenye uchungu mkubwa kuona maisha ya dhiki,njaa, magonjwa nchi za America ya kusini, akawa na mwamko mkubwa kubadili hali ile kwa kuwa aliamini ya kuwa mfumo wa ubepari ndio chanzo kikubwa kilichokuwa kinaitafuna Latin America.

Miaka ya 50 akiwa anasoma udaktari huko Mexico Che Guevara alikutana na Fidel Castro na Raul Castro ambapo watatu hao walipanga mapinduzi ya kumg’oa raisi wa Cuba wakati huo Fulgencio batista ambaye alikuwa na huhusiano wa kimaslahi na America, Che akapata nguvu na uaminifu mkubwa kutoka kwa Fedel Castro na kupandishwa kuwa kiongozi wa wanamgambo (guerilla insurgents)

Punde tu baada ya Fulgencio batista kukimbia CUBA,Che alihusika kama mtu muhimu katika serikali ya Cuba iliyoongozwa na Fidel Castro, akiwa kama Gavana wa benki kuu ya Cuba ambapo saini yake ilianza kutumika katika noti za CUBA , baadae kama waziri wa kilimo wa Cuba.

Mwaka 1964 akiwa kama mmoja ya msafara wa watu wa serikali ya Cuba umoja wa Mataifa New York MArekani, aliweza kupata “sifa” ya “mwanamapinduzi halisi wa kukumbukwa” pale alipotoa hotuba ndefu katika ukumbi wa UN akilaumu wazi ukimya wa Umoja huo juu ya kilichokuwa kinaendelea Afrika ya kusini (ubaguzi wa Rangi) alinukuliwa akisema

“wale wanaoua watoto wao na kuwabagua kila siku kwa sababu ya rangi ya ngozi zao, wazungu wanawaua watu weusi na hawakamatwi, serikali ya kikaburu inawalinda wauaji, na mbaya Zaidi inawaadhibu watu weusi kwa kuwa tu wanatataka haki zao na utu wao, vipi watu hawa (makaburu) wakaitwa watetezi na walinzi wa Amani?”

MGOGORO WA CONGO – DRC
Miezi michache baada ya kutoa hotuba UN, Che alitoweka katika maisha ya kawaida “public life” na hakuna aliyejua alikwenda wapi mpaka baadae ilipokuja gundulika Che alikuwa akipigana sambamba na Laurent Kabila huko Congo dhidi ya wabeligiji na baadhi ya wapiganaji wa ki cuba waliokuwa Afrika, vita ambayo ilishindikana na akakimbilia Tanzania na kukaa maeneo ya karibu na ziwa Tanganyika na baadae Dar es salaam huku akiishi kwa kujificha

Baadae mwaka 1966 alirejea Cuba kumuaga kwa Fudel castro na kusafiri kwenda Bolivia kuendeleza harakati zake za kuzikomboa nchi za America ya kusini kutoka kwenye makucha ya Ubepari…aliingia Bolivia akiwa kama mfanyabiashara hasiyejulikana baada ya kunyoa upara, kuweka mvi bandia na kuyoa ndevu zake zote, akaweka kambi na baadhi ya wapiganaji wenzake aliowakuta Bolivia maeneo ya milima ya montane dry fores

KUKAMTWA NA KUUWAWA
Mwaka 1967, makachero wa Bolivia wakisaidiwa na CIA amabye alikuwa akiwakilsha ndugu Felix Rodriguez waligundua maficho ya ache na kundi lake huko milimani Bolivia, asubuhi ya October 8 mwaka 1967 wanajeshi takribani 1,800 walizingira maeneo yoote ya milima walikokuwa wamejificha akina Che na ikapiganwa vita ya masaa kadhaa na Che akipigwa Risasi za miguu na kukamatwa na wenzake,

Yasemekana baada ya kuzidiwa katika mapigano yale alisema
“Usifyatue risasi, mi ni Che Guevara nina thamani kubwa kuwa hai kuliko kunikamata nimekufa”

Alifungwa kama na wenzake akakamatwa na kupelekwa kijiji cha La higuera ambapo baada ya raisi wa Bolivia ndugu kusikia amekamtwa alitoa amri auwawe haraka sana, wakati huo huo CIA walimtaka apelekwe Panama akahojiwe kwa kina na salama yake ili hasiuwawe alikuwa apelekwe America japo haikutokea.

Siku moja kabal ya kuuwawa alichukuliwa na baadhi ya wanajeshi na kupiga picha ya kumbukumbu na kesho yake akauliwa na askari mmoja aliyejitolea na kumpiga risasi sita za kifua na kufa palepale

Kabla hajapigwa risasi na muuaji wake haya ndio yalikuwa maneno yake ya mwisho

“Najua umekuja kuniua, shoot mtu mwoga wewe!!! na ufahamu utakua umeua mwanaume kamili”
Aliacha wake wawili na watoto watano.

Zaidi soma=> Mjue Ernesto Rafael Guevara de la Serna au Che Guevara
 
KUKAMTWA NA KUUWAWA

Mwaka 1967, makachero wa Bolivia wakisaidiwa na CIA amabye alikuwa akiwakilsha ndugu Felix Rodriguez waligundua maficho ya ache na kundi lake huko milimani Bolivia.....

Alifungwa kama na wenzake akakamatwa na kupelekwa kijiji cha La higuera ambapo baada ya raisi wa Bolivia ndugu kusikia amekamtwa alitoa amri auwawe haraka sana, wakati huo huo CIA walimtaka apelekwe Panama akahojiwe kwa kina na salama yake ili hasiuwawe alikuwa apelekwe America japo haikutokea.

Siku moja kabal ya kuuwawa alichukuliwa na baadhi ya wanajeshi na kupiga picha ya kumbukumbu


Uandishi wako hovyo sana.. Unaandika kama bata...
 
Umejitahidi kuandika.. Ila kuna vitu unapotosha km unavyosema walikutana na Che Guevara akiwa masomoni Mexico.... Ukweli ni kwamba hakua masomoni kipindi hicho... Ukitaka kujua zaidi soma kitabu kilichoandikwa na Richard Harris.. Kuhusu historia ya Che Guevara upate ukweli halisi...... Kama ukikitaka ni pm nitakupa au nenda book lab pale mikocheni utakipata.
 
Alizaliwa mnamo 14 Mei 1928 Rosario nchini Argentina. Alikuwa mtabibu aliyekuwa mfuasi wa itikadi za Kisoshalisti za Karl Marx. Guevara anajulikana zaidi kwa harakati zake za kimapinduzi dhidi ya tawala za kibepari huko Amerika ya Kusini na Afrika.
Wakati akisomea utabibu, Che Guevara alizunguka katika nchi mbalimbali za Marekani ya Kusini ambapo alijionea mwenyewe umasikini uliokithiri. Alisikitishwa sana na maisha ya ufukara waliokuwa wakiishi wananchi wengi huku wachache wakiwa wanamiliki mali za nchi hizo. Alifikiria jinsi ya kuweza kubadili hali hii na kuamua kuwa njia pekee ya kuondoa umasikini na ukandamizaji ni mapinduzi.
Miaka ya 50 akiwa anasoma udaktari huko Mexico Che Guevara alikutana na Fidel Castro na Raul Castro ambapo watatu hao walipanga mapinduzi ya kumng'oa raisi wa Cuba wakati huo Fulgencio batista ambaye alikuwa na huhusiano wa kimaslahi na America, Che akapata nguvu na uaminifu mkubwa kutoka kwa Fedel Castro na kupandishwa kuwa kiongozi wa wanamgambo (guerilla insurgents)
Punde tu baada ya Fulgencio batista kukimbia CUBA,Che alihusika kama mtu muhimu katika serikali ya Cuba iliyoongozwa na Fidel Castro, akiwa kama Gavana wa benki kuu ya Cuba ambapo saini yake ilianza kutumika katika noti za CUBA , baadae kama waziri wa kilimo wa Cuba.
Mwaka 1964 akiwa kama mmoja ya msafara wa watu wa serikali ya Cuba katika umoja wa Mataifa UN, aliweza kupata sifa ya mwanamapinduzi halisi wa kukumbukwa pale alipotoa hotuba ndefu katika ukumbi wa UN akilaumu wazi ukimya wa Umoja huo juu ya kilichokuwa kinaendelea Afrika ya kusini (ubaguzi wa Rangi) alinukuliwa akisema
"Wale wanaoua watoto wao na kuwabagua kila siku kwa sababu ya rangi ya ngozi zao, wazungu wanawaua watu weusi na hawakamatwi, serikali ya kikaburu inawalinda wauaji, na mbaya Zaidi inawaadhibu watu weusi kwa kuwa tu wanatataka haki zao na utu wao, vipi watu hawa (makaburu) wakaitwa watetezi na walinzi wa Amani?"
Mwaka 1965 ikiwa ni Miezi michache baada ya kutoa hotuba UN, Che alitoweka katika maisha ya kawaida public life na hakuna aliyejua alikwenda wapi mpaka baadae ilipokuja gundulika Che alikuwa akipigana sambamba na Laurent Kabila huko Congo dhidi ya wabeligiji na baadhi ya wapiganaji wa ki cuba waliokuwa Afrika, vita ambayo ilishindikana na akakimbilia Tanzania na kukaa maeneo ya karibu na ziwa Tanganyika na baadae Dar es salaam huku akiishi kwa kujificha.
Baadae mwaka 1966 alirejea Cuba kumuaga kwa Fudel castro na kusafiri kwenda Bolivia kuendeleza harakati zake za kuzikomboa nchi za America ya kusini kutoka kwenye makucha ya Ubepari, aliingia Bolivia akiwa kama mfanyabiashara hasiyejulikana baada ya kunyoa upara, kuweka mvi bandia na kuyoa ndevu zake zote, akaweka kambi na baadhi ya wapiganaji wenzake aliowakuta Bolivia maeneo ya milima ya montane dry forest.
Mnamo mwaka 1967, makachero wa Bolivia wakisaidiwa na CIA amabye alikuwa akiwakilsha ndugu Felix Rodriguez waligundua maficho ya ache na kundi lake huko milimani Bolivia, asubuhi ya October 8 mwaka 1967 wanajeshi takribani 1,800 walizingira maeneo yoote ya milima walikokuwa wamejificha akina Che na ikapiganwa vita ya masaa kadhaa na Che akipigwa Risasi za miguu na kukamatwa na wenzake.
Yasemekana baada ya kuzidiwa katika mapigano yale alisema
"Usifyatue risasi, mi ni Che Guevara nina thamani kubwa kuwa hai kuliko kunikamata nimekufa".
Alifungwa kamba na wenzake akakamatwa na kupelekwa kijiji cha La higuera ambapo baada ya raisi wa Bolivia ndugu René Barrientos kusikia amekamtwa alitoa amri auwawe haraka sana, wakati huo huo CIA walimtaka apelekwe Panama akahojiwe kwa kina na salama yake ili asiuwawe alikuwa apelekwe America japo haikutokea.
Siku moja kabal ya kuuwawa alichukuliwa na baadhi ya wanajeshi na kupiga picha ya kumbukumbu na kesho yake akauliwa na askari mmoja aliyejitolea na kumpiga risasi sita za kifua na kufa palepale.
Kabla hajapigwa risasi na muuaji wake haya ndio yalikuwa maneno yake ya mwisho,
"Najua umekuja kuniua, shoot mtu mwoga wewe!!! na ufahamu utakua umeua mwanaume kamili"
Baada ya kifo chake, Guevara alichukuliwa kama nguzo ya vuguvugu la kimapinduzi ya kishoshalisti duniani. Picha yake na kofia aina ya Beret aliyopenda kuivaa vimekuwa kama alama za mapinduzi ya mrengo wa kushoto duniani.
Aliacha wake wawili na watoto watano
 
Uandishi wako hovyo sana.. Unaandika kama bata...
Kwani ni LAZIMA KUSOMA Uzi Wa watu?unakashifu UZI WA WENGINE wakati hujawahi hata KUANDIKA chochote humu,,,, hata UGOMVI WA KUKU....hujawahi KUANDIKA ....wacheni WIVU WA KIPUUZI .....
 
Watu wa namna hii zama hizi za 2000s HAWAPO!...Siku hizi vita inapiganywa kweyr keyboard !


Jamaa anaungurumisha taarifa za adui na kummaliza kwa kutumia drone!

Kizazi hicho cha kina Castro, Che, Na wengine kama hao masalia yao ndio kina Koni.

Ila hawa wa kizazi hiki hawapigani kwa ajili ya nchi zao au bara lao. Wao wanalenga matumbo yao tu!

Hebu fikiria leo likatokea jitu karba ya Che likaamua kufanya yake ya kuwapindua marais wote .adikteta akianzia Afrika!....yupo mtu huyo asiyefungwa na mipaka ya wakoloni?
 
Kuna watu wengine humu wimbo Wa mwanza uliofungiwa unawahusu. Hongera mwandishi kwa kutupa mwangaza kuhusiana na huyu mwanaharakati
 
Back
Top Bottom