Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
HISTORIA FUPI YA OFISI ZA AFRICAN ASSOCIATION (AA), TAA, TANU HADI CCM 1933 - 2021
Picha ya kwanza ni ofisi ya African Association (AA) siku ya ufunguzi wake mwaka wa 1933.
Hii picha ya ufunguzi ambayo Kleist Sykes, Mashado Ramadhani Plantan, Mwalimu Mdachi Shariff wako pamoja na Gavana Donald Cameron inatoka katika Maktaba ya familia ya Sykes.
Imeshindikana kupata majina ya wanachama wengine katika picha waokuwapo katika siku hii ya ufunguzi wa ofisi ya AA.
Picha hii ipo katika kitabu cha Abdul Sykes.
Picha ya pili ni ofisi za TAA na TANU hadi kufikia uhuru 1961 na jengo la tatu CCM ikijenga ofisi yake mpya.
Picha ya tatu no ofisi ya CCM ikichukua nafasi zilipokuwa ofisi za African Association, TAA na TANU.
Ofisi ya African Association ilijengwa kwa wanachama kujitolea kila Jumapili kuanzia 1929 -1933 ilipokamilika.
Abdul Sykes anasema yeye akiwa mtoto mdogo amemuona baba yake na wenzake wakifanya kazi ya ujenzi hapo Mtaa wa New Street na Kariakoo kwani baba yake alikuwa akimchukua kwenda pale kila siku ya Jumapili asubuhi.