Historia fupi ya Zanzibar

Historia fupi ya Zanzibar

Tokyo40

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2013
Posts
2,065
Reaction score
1,925
Masultani wa Zanzibar waliitawala Zanzibar iliyojulikana kama "Sultanate of Zanzibar" rasmi tangu mwaka 1856.

Sultani wa Oman, Said bin Sultan, aliitawala Zanzibar kutoka Oman, tangu 1804. Kabla ya hapo, Zanzibar ilikuwa "overseas holdings" au ardhi ya nje inayomilikiwa na Oman tangu 1698. Na kabla hapo, Zanzibar ilikuwa koloni la Ureno kwa zaidi ya miaka 200.

Msikiti wa kwanza ulijengwa na Waarabu wa Yemen, mwaka 1107 AD huko Kizimkazi, kusini mwa Unguja.

Kati ya 1832 na 1840, Sultan Said alihama Oman na kuja Zanzibar. Uchumi wa Zanzibar ulitegemea karafuu iliyolimwa kwa kutumia nguvu ya Watumwa na biashara za Wahindi.

Sultan Said aliwakaribisha Wahindi Zanzibar kwa kuwa walikuwa wafanyabiashara wazuri. Yeye akapata kodi yake na vitu vingi vikaletwa Zanzibar kutoka Bara Hindi na sehemu nyingine za dunia.

Baada ya Sultan Said kufariki 1856, watoto wake wawili waligombania Usultani. Zanzibar na Oman ikagawanywa. Sultan Thuwaini bin Said akawa Sultani wa Oman, na Majid bin Said akawa Sultani wa kwanza wa Zanzibar iliyojulikana kama "Sultanate of Zanzibar".

Sultani aliyomfuata, Barghash bin Said, aliijenga Zanzibar na pamoja na Sultani wa tatu, Khalifa bin Said.

Barghash bin Said alikubaliana na Uiingereza kusimamisha biashara ya utumwa mwaka 1870. Akafunga soko la utumwa la Mkunazini.

Barghash bin Said alipelekwa India kusoma na Uiingereza ili asilete matatizo ndani ya Usultani wa ndugu zake wawili waliosaidiwa na Uiingereza kuingia madarakani Oman na Zanzibar alipokufa baba yao akiwa baharini akirudi Zanzibar kutoka Oman kwa kikazi.

Barghash bin Said alileta maji katika mabomba mjini na kuwaomba Waiingereza walete usafiri wa kila siku wa meli ya abiria baina ya Aden na Zanzibar. Usafiri huu ulisaidia kufanya mawasiliano ya barua kati ya Zanzibar na dunia kuwa rahisi. Aliweza pia kuifanya Zanzibar kuwa na mawasiliano ya "telegraph" baada ya kuvutiwa cable baharini kutoka Aden, koloni la Uiingereza.

Khalifa bin Said, Sultani aliyomfuata, akatawala miaka miwili tu, kuanzia 1888-1890. Aliugua homa na kufariki ghafla akiwa na miaka 36. Kabla ya kufa, alishatunga sheria ya kumpa mtumwa yoyote uhuru wake akikanyaga ardhi ya Zanzibar.

Sultani Ali bin Said akamfuata na kuifanya Zanzibar na Pemba kuwa chini ya Uiingereza "Protectorate of Zanzibar" mwaka 1890.

Mpaka 1886, njia nyingi za biashara katika bahari ya Hindi, pwani ya Afrika Mashariki, pamoja na baadhi ya ardhi Bara ilikuwa chini ya Sultani wa Zanzibar (sphere of influence).

Wajerumani na Waiingereza walipima na kuamua kuwa ardhi ya "Zanj" ya Sultani ni kutoka Cape Delgado (sasa Msumbiji) mpaka Kipini (sasa Kenya) pamoja na Mombasa na Dar es Salaam, pamoja na visiwa vingine vidogo vya Bahari ya Hindi.

Uiingereza na Ujerumani hawakupendelea Zanzibar kumiliki hizi njia za biashara wala ardhi Bara. Walikutana kisiri na kujigawania sehemu zilizokuwa chini ya "sphere of influence" ya Ufalme wa Zanzibar barani Afrika.
Mpaka ilipofika mwaka 1892, ardhi yote Bara ikachukuliwa na Wakoloni wa Ulaya.

Ardhi iliyo chini ya Sultani wa Zanzibar barani Afrika Mashariki ilikuwa ni " sphere of influence" yake.

Yaani, haijulikani kisheria kama ni ardhi yake. Hajapeperusha bendera yake wala kuwaweka jeshi lake kulinda ardhi au njia zake za biashara kama China inavyojaribu kufanya leo katika Bahari ya Kusini ya China.

Sultani wa Zanzibar alipopinga kuchukuliwa ardhi yake katika Bara la Afrika Mashariki na Carl Peters huko Bara, Kiongozi wa Ujerumani, Otto von Bismark akatuma meli tano za Kijeshi na mizinga ikaelekezwa Zanzibar. Sultani wa Zanzibar inabidi akubali nguvu za kijeshi za Ujerumani na kuwaachia wajigawanyie Afrika Mashariki kati ya Ujerumani na Uiingereza.

Ujerumani ikachukuwa ardhi iliyojulikana kama "German East Africa" ambayo itakayojulikana baadae kama Tanganyika, Rwanda na Burundi.

Mwaka 1890, Sultani Ali bin Said akasaini mkataba wa " Heligoland- Zanzibar Treaty" na Uiingereza na Zanzibar ikawa chini ya Uiingereza na kujulikana kama "Protectorate of Zanzibar".

Mkataba huo ulikuwa pia baina ya Ujerumani na Uiingereza.
Uiingereza ikakubali kurudisha ardhi ya Ujerumani ya Heligoland karibu na Bahari ya Kaskazini huko Ulaya na Ujerumani ikamwachia Uiingereza kuichukua Zanzibar na kuendelea kuitawala ardhi ya Kenya na kwingineko katika Bara la Afrika.

Ujerumani pia ikapata ardhi ambayo leo ni nchi huru ya Namibia.

Mwaka 1896, Uiingereza na Zanzibar walipigana vita vya dakika 38. Uiingereza walitaka kibaka wao, Hammoud bin Mohamed kuwa Sultani wa Zanzibar.

Khalid bin Barghash, mtoto wa Barghash bin Said, alichukuwa Usultani baada ya kifo cha Sultani Hamid bin Thuweini. Waiingereza walimpa saa moja kuondoka madarakani na kumpa Usultani Hammoud. Khalid akakataa na kupigana nao kwa dakika 38 na mwisho kukimbia nje ya nchi na kumwachia Usultani Hammoud bin Mohammed.

Alipofariki, mtoto wake, Ali bin Hamoud, aliyeishi na kusomeshwa Uiingereza, akawa Sultani mwaka 1902.

Alipoalikwa Uiingereza kuhudhuria kuapishwa kwa Mfalme George V mwaka 1911, aliamua kuacha madaraka na kufa Paris mwaka huo huo. Watoto wake wakakataa kuchukua madaraka Zanzibar.

Sultan Khalifa bin Haroub akachukua madaraka mpaka 1960.

Mwaka 1925, Uiingereza ukaamua kuifanya Zanzibar koloni badala ya kuwa "Mlinzi". Waiingereza wakajenga barabara, wakatanua bandari, wakajenga shule na mahospitali.

Mtoto wa Khalifa, Abdulla bin Harub, akachukuwa madaraka. Alikuwa baada miaka mitatu tu na kisukari mwaka 1963.

Jamshed bin Abdulla, mwanae, akachukua madaraka na kupinduliwa katika Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964. Mpaka leo, anaishi Uiingereza.

Kabla ya kupinduliwa, Uiingereza iliwapa Zanzibar uhuru na Zanzibar ikawa ndani ya utawala wa kikatiba wa kifalme (Constitutional Monarchy) wa Sultani Jamshed bin Abdulla.

Jina la Zanzibar likabadilishwa na kuitwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar na Pemba.

Mnamo April 1964, Jamhuri hii ikaungana na Tanganyika na umoja wao ukaitwa Jamhuri ya umoja wa Tanganyika na Zanzibar na baada ya miezi sita, jina likabadilishwa tena na umoja wao kuitwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Chanzo:

Ayany, Samuel G. (1970), A History of Zanzibar: A Study in Constitutional Development, 1934–1964, Nairobi.

Ingrams, William H. (1967), Zanzibar: Its History and Its People.

Keane, Augustus H. (1907), Africa 1 (2nd ed.), London.

Michler, Ian (2007), Zanzibar: The Insider's Guide (2nd ed.), Cape Town.

Turki, Benyan Saud (1997), "The Sultan of The Arab State of Zanzibar and The Regent 1902–1905".

James Stuart Olson; Robert Shadle (1991). Historical Dictionary of European Imperialism. Greenwood.

William L. Langer, The Diplomacy of Imperialism, 1890-1902 (1951).

Perras, Arne (2004). Carl Peters and German Imperialism 1856–1918: A Political Biography. Clarendon Press.

Angelfire.com
 
Hi ni historia ilopindwa pindwa sana na wakoloni wazungu ili kuhalalisha uovu wao waliokuwa wakiufanya dhidi ya watu watu wa East Africa.

Someni kitabu "Dola Kongwe ya Zanzibar kutoka Oman hadi Congo"
 
Ungesaidia kuelimisha jamii kwa kutoa mwangaza zaidi juu ya hicho kitabu.

Vitabu vingi vya maana havipatikani kirahisi Tanzania na watu wengi ni wavivu wa kusoma.

Pia, lazima uchanganye ubongo unavyosoma kitu.

Superpower wa dunia wanajulikana kwa waliyoaacha nyuma... Aztec civilization, Pharaoh, Timbaktu, Inca civilization, ancient Greek and Roman civilization, Ottoman Empire etc.

Tuelimishe Mkuu, kuhusu Dola Kongwe ya Masultan wa Zanzibar na Oman.
 
Back
Top Bottom