Historia hutengenezwa namna hii

Historia hutengenezwa namna hii

Makonyeza

Member
Joined
Feb 2, 2020
Posts
72
Reaction score
261
Pichani ni bwana mdogo wa Kinaijeria anaitwa Samuel Chukwueze anayeitumikia Club ya Villarreal ya Hispania na pia ni mchezaji wa timu ya taifa ya Nigeria [emoji1184] kama kiungo wa pembeni, yaani 'Winger' .

Usiku wa Jana ameisaidia timu yake ya Villarreal kuwatupa nje ya mashindano wababe Buyern Munich kwa kufunga bao muhimu na la ufundi la kusawazisha dakika ya 87 ya Mchezo na kufanya uwiano wa mabao kuonesha Villarreal 2-1 Buyern Munich baada ya Munich kutangulia kwa goli la mbabe Robert Lewandowski.

Villarreal ilinufaika na ushindi wa goli moja iliyoupata katika Mchezo wa kwanza.

Yes, kijana ameweka historia kwa kuwapeleka wa-Hispaniola nusu fainali ya mashindano ya UCL.

Ni bonge la historia kwa sababu si kwa ajili yake tu, lakini pia kwa nchi ya Hispania kuipeleka timu mbili nusu fainali kufuatia Real Madrid nao kuwatupa nje ya mashindano Chelsea ambao licha ya ushindi walioupata haikuwasaidia kwenda hatua ya nusu fainali.

Jina la Dogo wa Kinaijeria litabaki katika historia na pia ameongeza thamani yake maradufu.
Hivyo ndivyo historia huwekwa katika soka[emoji123][emoji123]

_20220413_083110.JPG
 
Hakika inapendeza, hasa mashindano makubwa Kama UCL
 
Ila bayern katuchania sana mikeka jana.
 
Back
Top Bottom