Kanungila Karim
JF-Expert Member
- Apr 29, 2016
- 20,743
- 25,564
SEHEMU YA KWANZA
Naomba nianze kwa kusema kuwa, kwa asilimia kubwa watu wanaamini kuwa Waafrika weusi walifika Amerika mara baada ya Christopher Colunbus kugundua bara la Amerika kwenye miaka ya 1490, ( japo mimi kama mwanahistoria sijaona alichokugundua, bali aliwakuta watu na ardhi yao na wakiwa na maisha yao na shughuri zao za kila siku, ambazo zilikuwa ngeni kwa watu wa Ulaya na sio kugundua).
Yaani wengi tunaamini kuwa historia ya mwafrika barani Amerika ilianza mara baada ya biashara ya utumwa kuanza.lakini ukweli ni kwamba historia ya Waafrika kwa kiasi kikubwa imefichwa sana na bado Waafrika hatujisumbui kutafuta historia ya kweli juu ya maisha yetu.yaani tumekuwa watu wa kukubali kila kinachosemwa na watu wa magharibi.ikumbukwe kuwa hapo mwanzo Waafrika tulikuwa na mfumo wetu wa elimu ambao ulikuwa ukitoa elimu sawina na yenye uhalisia na maisha ya Waafrika.
Lakini baada ya ujio wa wakoloni wametuletea elimu ambayo kila kukicha ikakuza tamaduni zao na kudumaza tamaduni zetu za kiafrika, “eti tukidai kuwa zimepitwa na wakati” huu tunaita ni “ulevi” hasa ulevi wa fikra za kimagharibi na sijajua ulevi huu utatuisha lini.
Yaani imefikia wakati, Kutokana na elimu ya kimagharibi Waafrika wamefikia hatua ya kujikataa wenyewe kwa kupinga yale ambayo Waafrika wa zamani walikuwa wanafanya. Na ndio maana watu wanadhani na kuamini kuwa Waafrika hawakuwa na historia yoyote katika bara la Amerika kabla ya Christopher Columbus. Yaani historia ya Mwafrika barani Amerika ilianzia kwenye miaka ya 1490 mara baadea ya biashara ya utumwa kuanza, jambo ambalo sio la kweli.
Lakini leo nataka niwape ukweli juu ya uwepo wa Waafrika barani Amerika hata kabla ya ujio wa wazungu. Ukisoma vitabu hivi, They Came Before Columbus, African Presence In America Before Columbas, Civilization Of America ,Civilization Of Africa Na Civilization Of Asia,utagundua kuwa Waafrika walikuwepo barani Amerika hata kabla ya ujio wa wazungu. Kwa kuwa vitabu hivi vimeandikwa kwa lugha mbalimbali na sio kwa lugha ya Kiswahili, ilikuwa vigumu kwa Mtanzania kujua ukweli.
Ila leo makala hii fupi inakupa mwanga juu ya historia ya Mwafrika katika bara la Amerika kabla ya miaka ya 1490, na ni matarajio yangu kuwa mara baada ya kusoma makala hii fupi, tunatarajia jamii kujua ukweli wa historia ya Mwafrika katika bara la Amerika…
SEHEMU YA PILI
USHAHIDI WA KIMAANDIKO
Maandiko Ya Peni Ya Christopher Columbus 1490’S, kwa ufupi ni kwamba, Wareno na Wahispania walikuwa watu wa kwanza kufika Amerika wakitokea barani Ulaya. Na kila sehemu walizopita waliweza kuandika kila kitu walichokiona. Kwa ujumla Wareno na Waspania waliandika mambo mengi sana. Maandiko yao, yapo yailiyohifadhiwa na kuna mengine hayakuhifadhiwa kutokana na sababu mbalimbali.
Sasa yale yaliyohifadhiwa yalisaidia sana kutoa ushadihi juu ya mabishano ya kihistoria juu ya historia ya Mwafrika kuwepo barani Amerika kabla ya 1490. Sifa kubwa ya maandishi ya wapelelezi wa kale ni kwamba, yalikuwa yakiandikwa kutokana na mtu alivyoona, yaani mwandishi aliweza kuandika kile anachoona au kile anachosikia kwa wakati huo.
Kutokana na maisha ya mwanzo biandamu hakuwa na haja ya kuongopa waliyokuwa wakiyasimulia, kwani hakukuwa na vyombo vya habari wala mitandao ya kijamii kama hivi sasa, ambapo tumekuwa tukisikia taarifa nyingi za ukweli na uongo. Hivyo kila kitu kilichokuwa kikiongelewa kilikuwa sahihi na waandishi waliandika kwa usahihi.
Kwa namna hiyo tunapozungumzia juu ya maandiko ya Christopher Columbus aliyepata kuishi kwenye miaka ya (1450-1500), haya yalikuwa maandiko ambayo yaliandikwa kwa mkono wake mwenyewe kwa kutumia wino wa peni. Maandiko hayo yanasema kuwa “alipofika katika maeneo ya Haiti, aliwakuta wenyeji ambao ni Wahindi wekundu, na wakamwabia kuwa, kabla ya ujio wako hapa kulikuwa na watu wenye ngozi nyeusi (Black-skinned People) wakifanya biashara ya dhahabu, ambao walitokea kusini-mashariki mwa bahari ya Antlantiki.
Na zaidi biashara waliokuwa wakifanya ilihusisha dhahabu na zana za chuma kama mishale kwa ajili ya uwindaji” ( Kwani jamii za Olmeki walikuwa wawindaji na waliishi kwenye misitu mikubwa). Kwa ufupi olmeki ni moja ya falme ya mwanzo kupata kuwepo Amerika iliundwa na wahindi Wekundu hata kabla ya 1400.
Kutokana na taarifa hizo zenye kuhusisha biashara ya dhahabu na chuma, Wareno walijaribu kulinganisha dhahabu za Waafrika na ya Wahindi ikaonekana zipo sawa kwa uzito na kwa ubora kwa asilimia kubwa. Wapo waliouliza kuwa Waafrika hao walitokea wapi? Na jibu lilikuwa jepesi na lenye kueleweka kuwa, Waafrika hao, wapo waliotokea Misri (Wanubia wa Kusini) na wapo waliotokea Afrika magharibi.
Kuna Mpelezi mwingine wa Kihispania ambaye pia aliandika maandiko yake akielezea jinsi alivyowakuta Wahindi wekundu barani Amerika wakionyesha kidole uelekeo wa bara la Afrika. Na alipata majibu kama aliyopewa Christopher Columbus. Mpelelezi huyu alifahamika kwa jina la Vasco Nunes De Balbo aliyepata kuishi kwenye miaka (1470-1520 ).
Alianza kutembelea bara la Amerika kwenye maika ya 1510. Maandiko yake yalikuwa kwenye miaka ya 1513. Vaso Nunes De Balbo aliandika kwenye maandiko yake siku ya kwanza alipofika Amerika na kuwakuta Wahindi Wekundu wakizungumzia habari za watu weusi (Black-skinned people) kuwa walikuwepo hapa na walifanya biashara na kuondoka maeneo haya. Maandiko hayo yanasema kuwa kila sehemu walipowakuta Wahindi walizunguzia hivvyo hivyo.Kwa namna hiyo maandiko ya Christopher Columbas na Vasco Nunes De Balbo yalichangia sana kutoa ushahidi juu ya uwepo wa watu weusi barani Amerika kabla ya watu wa Ulaya.
.Na mwisho maaandiko ya Christopher Columbus na Vasco Nunes De Balbo yalikubaliwa na wanahistoria na wanaakiolojia kuwa ni moja ya ushahidi kuwa Waafrika historia yao haikuanzia kwenye miaka ya 1490 kama tunavyokalilishwa.
Sent using Jamii Forums mobile app