SoC02 HISTORIA: Mama yangu popote ulipo lala Salama

SoC02 HISTORIA: Mama yangu popote ulipo lala Salama

Stories of Change - 2022 Competition
Joined
Mar 4, 2017
Posts
11
Reaction score
26
Habari,

Kwa majina naitwa (Geniva Joseph) sio majina halisi, ila nipo hapa kuwasilisha historia fupi ya maisha yangu yangu na jinsi gani uwajibikaji ni muhimu sana katika jamii yetu

Nilizaliwa kijijini cha Katangaro mkoani Geita, Baba yangu kama baba wengine wasiokuwa wawajibikaji ilikuwa wiki imepita hajarudi Nyumbani Wala kujali familia inaendeleaje huku mama angu akiwa na ujauzito wangu, akihangaika na familia, kupika na shughuri za shamba

Usiku mmoja haukuwa usiku mzuri sana kwa Mama yangu kwani alianza kuumwa sana na kupiga kelele za msaada wala hakuna mtu aliyeweza kumsikia, alilia sana lakini baadae aliona Bora ajikaze kwani yeye ni Mama hivyo alifanikiwa kujifungua bila msaada wa mtu yeyote lakini ilipofika alfajiri Mama yangu alikuwa amepoteza damu nyingi sana na mida kama ya saa 11 Hadi saa 12 hivi mama yangu, kipenzi changu, alienipa zawadi ya uhai alikata Roho nikiwa chini ninapigwa na baridi Kali.

Kutokana na kelele zangu za kitoto kulia sana mithili ya kukaukiwa ndipo majirani waliokuwa wakipita kwenda shamba asubuhi walipita na kunihifadhi huku wengine wakilia na kuomba msaada maana mama hatukuwa nae Tena!....

Nasikia Baba yangu alifika Nyumbani siku hiyo saa mbili za asubuhi akiwa amebeba kitenge chenye ua la mfagio, lakini maskini aliemletea alikuwa tayari ameshatangulia. .

Nilichukuliwa na shangazi yangu aishie jijini Mwanza, maisha yangu mapya yalianza huku kwani Baba hakuweza kunilea, nimekuwa nikimuita shangazi Mama kwani ukweli sikuujua, nilikua mtoto mwenye furaha sana lakini baada ya Baba kufariki (mjomba) maana hata baba yangu mzazi sikuwahi kumjua, Shangazi (Mama) akawa na depression na kuwa mkali sana

Kabla mjomba kufariki tulikuwa tumeshahamia jijini Dar, mambo hayakuwa marahisi kwangu ndugu zangu wakaanza kunitenga, nikawa napigwa sana, kiasi cha baadhi ya marafiki na majirani kunihoji ( huyu kweli ni mama Yako mzazi?) Kwakweli nilikuwa siwaelewi kwani nilikuwa nampenda sana Mama yangu na ningefanya chochote au lolote Ili kumridhisha lakini kwake sikuwahi kutosha na kuna kipindi akanitamkia "Baba Yako hajawahi hata kukununulia chupi' lakini unakula unavaa Wala hajali, kwakweli nilikuwa confused lakini sikuthubutu kumuuliza...!

Nikaanza kuingiliwa na kaka yangu yaani mtoto wa shangazi yangu nikiwa na umri kama miaka 6/7 kama sikosei vizuri, nilikuwa najua ninachofanyiwa hakikua sawa lakini nitawaambia nani, shangazi ni mkali zaidi ya pilipili, yaani yeye huwezi kumwambia chochote zaidi ya yeye kuongea na wewe kufata maelekezo, siku zikasogea shangazi akaleta kijana ambae ni ndugu aje kufuga kuku, naye huyo kijana haikumchukua muda kunifanya mimi mke wake.

Maisha yangu ya utoto yakaanza kuwa ya upweke sana uliojawa na hofu, Haya yote yanafanyika shangazi yangu alianza kulewa anarudi Nyumbani usiku sana na akirudi ni kelele tu, kama nilivyosema hii inahusu uwajibikaji ndani ya jamii sipo hapa kumlalamikia mtu lakini nipo hapa kufikisha ujumbe Kwa jamii yangu

Kila mmoja ana jukumu la kulinda mtoto ndani ya jamii inayotuzunguka, fast forward Jambo hili lilinifanya kuwa mchunguzi na kuja kujua kuhusu mimi ni nani, nilipojua nililia na kumlaumu sana Baba yangu maana nilikuwa naamini asingemuacha mama yangu na kuwa na mahusiano mengine nje yamkini ningelelewa na Mama yangu na mambo yangekuwa tofauti kwangu lakini kumbe kazi ya Mungu haina makosa

Leo hii nimekua nina familia yangu, nimeolewa na nina Binti mmoja.

Asanteni sana WanaJamiiForums

Kama unaona nastahili kushinda tafadhali like na comment na unipigie kura Ili ujumbe huu ufike mbali zaidi na watu wabadilike.

Shukrani sana Kwa uongozi wa JamiiForums maana kupitia nyie tunapata kujifunza elimu ya mambo mbali mbali.
 
Upvote 7
Back
Top Bottom