Mhaya
JF-Expert Member
- Aug 20, 2023
- 1,831
- 5,489
Halloween ni tamasha la kila mwaka linaloadhimishwa Oktoba 31. Asili yake inarejea kwenye sherehe za zamani za Ki-Celtic, hasa sherehe zilizojulikana kama Samhain, ambapo Wacelt (ambao walikuwa ni watu wa zamani wa Ulaya Kaskazini, Uingereza, na Ireland) walikuwa wakisherehekea mwisho wa majira ya mavuno (Autumn) na kuanza kwa majira ya baridi (winter season).
Kwa kipindi hicho, ilikuwa inaaminika kwamba mpaka au kizuizi baina ya ulimwengu wa waliohai na wafu ulikuwa unafifia, na hivyo roho za wafu zingeweza kurejea duniani. Katika sherehe hiyo, Wacelt walichoma moto mkubwa na kuvaa mavazi maalum ili kufukuza roho mbaya na walivaa mavazi maalum ya manyoya na vinyago vya kutisha ili kufukuza roho mbaya ambazo zilidhaniwa kurudi duniani. Moto huo pia ulikuwa na maana ya kinga, wakiamini kwamba ungewalinda na kuwaongoza kupitia kipindi kigumu cha majira ya baridi na barafu (winter season).
Kwa kuwa Wacelt hawakuwa na kalenda ya kidini inayofanana na ya sasa, waliamini kuwa sherehe za Samhain pia zilikuwa ni kipindi ambacho miungu yao walikuwa karibu na binadamu, wakidhibiti hali ya hewa, mavuno, na afya.
Mwaka wa 43 BK, Warumi walipovamia maeneo ya Wacelt, walichanganya tamaduni za Samhain na sikukuu mbili za Kiroma: Feralia, iliyoadhimishwa kuwakumbuka wafu, na Pomona, aliyekuwa mungu wa miti na matunda. Katika utamaduni wa Warumi, apple ilikuwa ni tunda muhimu, na inasemekana kuwa huu ndio msingi wa utamaduni wa sasa wa "bob for apples" wakati wa Halloween.
Feralia: Hii ilikuwa ni sikukuu ya Kiroma iliyofanyika mwishoni mwa mwezi Februari. Feralia ilikuwa siku ya kuwakumbuka na kuwaenzi wafu, ambapo Warumi walitoa sadaka na kufanya maombi ili kutoa heshima kwa marehemu. Walidhani kwamba kipindi hicho roho za wafu zilirudi kutembelea dunia, na kwa njia hii walijaribu kuziridhisha ili roho zione zinakumbukwa na ndugu zao, kama umewai kuangalia animation ya Coco 2017 utakuwa umeelewa sherehe hii inafananaje. Hili lilikuwa jambo ambalo liliendana kwa kiasi na Samhain, kwani pia lilihusisha wazo la mipaka baina ya dunia ya roho na ya walio hai kuwa nyembamba.
Pomona: Hii ilikuwa ni sikukuu ya kumuenzi Pomona, mungu wa Kiroma wa miti na matunda, hasa apple. Pomona alihusishwa na mavuno na uzalishaji wa mazao, na hivyo sikukuu yake ilikuwa inaendana na msimu wa mavuno wa Wacelt. Wakati Warumi walipounganisha sikukuu ya Pomona na Samhain, matunda kama apple yakawa na nafasi maalum katika sherehe. Hii ni sababu mojawapo inayoweza kueleza mchezo wa "bobbing for apples" katika Halloween ya sasa, ambapo watu hujaribu kuokota apple kwa mdomo kutoka kwenye chombo chenye maji.
Baada ya Warumi kuendeleza ubabe na utawala wao maeneo mbalimbali ya ulaya (Roman Empire Expansion). Kanisa Katoliki lilianza kuingilia sherehe za Samhain na mila nyingine za kipagani wakati lilipokuwa likieneza Ukristo Ulaya nzima. Katika juhudi zake za kusambaza imani ya Kikristo na kukomesha tamaduni za kipagani, Kanisa lilitumia mbinu ya kuunganisha au kubadilisha baadhi ya sikukuu za kipagani ili ziwe na maana za Kikristo. Njia hii iliitwa "kutakasa" tamaduni za kienyeji ili kuziunganisha ndani ya Ukristo.
Katika karne ya 8, Kanisa Katoliki lilijaribu kubadilisha tamaduni hizi kwa kuanzisha sherehe ambazo zingeshabihiana na sikukuu za wacelt
Mnamo mwaka Mwaka 609 BK, Papa Boniface IV aliweka Siku ya Watakatifu Wote mnamo tarehe 13 Mei ambayo ilijulikana kama All Saints' Day (Siku ya Watakatifu Wote), ili kusherehekea na kuwakumbuka watakatifu waliokufa kwa ajili ya imani yao. Hata hivyo, mwaka 835 BK, Papa Gregory III alihamisha tarehe ya sherehe hii kwenda tarehe 1 Novemba ili ikubaliane zaidi na kipindi cha Samhain. Lengo lilikuwa ni kutoa maana mpya ya Kikristo kwa sherehe ya zamani ya Wacelt. Siku hii ilikusudiwa kuwaenzi watakatifu wote ambao hawakuwa na siku maalum ya kusherehekea.
Usiku wa kuamkia siku hii ( yani usiku wa kumalizia tarehe 31 Oktoba) uliitwa All Hallows’ Eve, ambao baadaye ulijulikana kama Halloween. Kwa hiyo, Halloween inachukua mambo kutoka kwenye historia za kidini na za kitamaduni, ikijumuisha mahusiano na ulimwengu wa roho, watakatifu, na utamaduni wa kuwakumbuka waliotutangulia.
Mwaka 1000 BK, Kanisa liliongeza Siku ya Marehemu Wote mnamo tarehe 2 Novemba. Hii ilikuwa ni siku ya kuwakumbuka marehemu wote wa Kikristo. Katika mila za kanisa, waumini walihimizwa kufanya maombi maalum kwa ajili ya marehemu, ili kuwasaidia roho zao kutoka kuzimu na kuingia mbinguni. Sherehe hii pia ililingana na imani ya Wacelt kuhusu roho na uhusiano kati ya walio hai na wafu.
Baada ya ushindi wa Warumi dhidi ya Wacelt, baadhi ya tamaduni za Kiroma zilijumuishwa katika sherehe za Samhain, na kuunda msingi wa Halloween ya sasa, kama tulivyoijua.
Kwa Nini Halloween Inaenziwa?
Leo hii, Halloween inaadhimishwa kwa sababu kadhaa ambazo zimetofautiana na maana yake ya asili. Kwanza, tamasha hili limekuwa na mvuto wa kiutamaduni, hasa kwa watoto, ambao huvaa mavazi ya kutisha au yenye maana maalum na kushiriki katika michezo ya kutembelea nyumba mbalimbali wakiwaomba wenyeji "treats" kama pipi. Aidha, ni fursa ya watu wa umri wote kusherehekea kwa njia za kipekee kwa mavazi, sherehe na michezo, wakati wakiwa wamejikita katika maudhui ya kutisha, vichekesho, au vinyago vya ajabu. Katika utamaduni wa kisasa wa Marekani na nchi zingine, Halloween pia ni tamasha linalosaidia kujenga hisia za jamii, mahusiano mazuri na ni fursa ya kufurahia kwa pamoja.
Ingawa baadhi ya tamaduni na dini zinaona Halloween kuwa na asili inayohusiana na ushetani, ushirikina au wafu, wengine huona kama ni burudani na njia ya kujenga umoja miongoni mwa jamii, hivyo inabaki kuwa na umuhimu tofauti kulingana na eneo, imani, na utamaduni wa wahusika.
Hapa ni jiji la New York, Marekani watu wakicheza wimbo wa Michael Jackson - Thriller wakisherehekea Sikukuu ya Halloween