Historia ya Adolf Hitler, kuzaliwa kwake mpaka kifo chake

Historia ya Adolf Hitler, kuzaliwa kwake mpaka kifo chake

Ushimen

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2012
Posts
40,828
Reaction score
99,523
hitler1.jpg

Alizaliwa nchini Austria mwaka 1889, akaingia shule ya sekondari mwaka 1900 lakini hakufaulu, hivyo alishindwa kuendelea na masomo.

Alijaribu tena kurejea shuleni, zamu hii katika shule ya uchoraji iliyojulikana kama Akademia ya Usanii ya Vienna akafeli tena.

Baada ya kifo cha wazazi alikosa msaada wa familia akakaa kwa muda katika nyumba kwa ajili ya watu wasio na makazi. Tangu alipohama nyumbani aliacha kufuata dini ya mama yake, Klara, akachukia moja kwa moja Kanisa Katoliki kwa kuliona halipendelei Wajerumani.

Baada ya kujaribu maisha ya msanii na mchoraji, alikuwa mwanajeshi wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia.

Mwanajeshi 1914 - 1918

Mwaka 1913 alihamia Munich katika jimbo la Bavaria (Ujerumani). Mnamo Agosti 1914, wakati wa mwanzo wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia, alijitolea kwa jeshi la Bavaria ambapo kutokana na bidii na ukakamavu wake alipanda cheo na kuwa praiveti. Mwisho wa vita mwaka 1918 alikuwa na cheo cha koplo.

Baada ya vita alikosa kazi lakini aligundua kipawa chake cha kuhutubia watu, akajiunga na siasa na kuingia katika chama kidogo cha Nazi (NSDAP) alikopanda ngazi haraka.

Hitler alivutwa sana na mfano wa Benito Mussolini, kiongozi wa kifashisti wa Italia, aliyefaulu mwaka 1922 kupindua serikali ya Italia kwa maandamano makubwa ya wafuasi wake kuelekea Roma.

Mwaka 1923 Hitler alijaribu kumwiga Mussolini kwa kupindua serikali ya Bavaria - kama utangulizi wa kupindua serikali ya kitaifa huko Berlin- lakini alikamatwa na kuhukumiwa kwa uasi huo kifungo cha miaka mitano, ingawa alitumikia miezi tisa tu. Chama chake kilipigwa marufuku.

Hitler akiwa kijana aliwahi kusoma vitabu vya Mwingereza Chamberlain aliyedai kwamba kuna mbari mbalimbali za watu zenye tabia na thamani tofauti sana.

nazi_monochrome_historical_adolf_hitler_parade.png


Akiwa gerezani aliandika kitabu kilichoitwa "Mein Kampf" ("Mapambano Yangu") alikojaribu kueleza imani na siasa zake. Humo alieleza pia chuki dhidi ya Wayahudi na itikadi yake ya ubaguzi wa kimbari.

Katika itikadi hiyo mbari ya juu ni watu wa Ulaya ya Kaskazini aliowaita "Waaria", na wale ambao ni duni zaidi ni watu weusi. Vikundi vingine vimo katikati. Lakini watu wabaya kabisa katika itikadi hiyo ni Wayahudi ambao ni wajanja wakuu upande mmoja, lakini hawana uwezo wa kuunda kitu kwa upande mwingine. Hivyo wanajaribu kwa ujanja wao kutawala dunia kwa kuiba fikra na mafanikio ya Waaria.

Baada ya kutoka gerezani alirudia siasa. Alijitahidi kushika utawala wa chama cha NSDAP akakubaliwa kuwa kiongozi mkuu. Ndani ya chama alianzisha vikosi viwili vilivyovaa sare vikifanya mazoezi kama wanamgambo na kuwa tayari kupigana na maadui wa kisiasa wakati wa maandamano.

Kikundi cha SA ("Sturmabteilung" - "Kikosi cha kushambulia") kilikuwa na watu wengi sana kikavuta hasa wanaume wasio na kazi waliovaa sare ya kahawia. Kikosi cha pili kilikuwa na watu wachache kikaitwa "SS" ("Schutzstaffel" - "Kikosi cha ulinzi") waliovaa sare nyeusi.
Chama chake hakikufaulu hadi 1929, wakati uchumi wa dunia pamoja na wa Ujerumani ulipoporomoka vibaya. Mamilioni waliachishwa kazi na kuona njaa. Katika hali hiyo watu walianza kupigia kura vyama vyenye itikadi kali.

Katika uchaguzi wa mwaka 1930 kura za NSDAP ziliongezeka kutoka 2.6% hadi 18.3%. Serikali za Ujerumani zilikuwa za vyama vingi na dhaifu.

Mwaka 1932 chama cha NSDAP kilipata 33% na kuwa chama chenye kura nyingi zaidi nchini na chama kikubwa katika bunge la Reichstag. Katika hali hiyo viongozi wa Dola la Ujerumani waliamua kumwingiza Hitler katika serikali mwaka 1933.

Tarehe 30 Januari 1933 Hitler akawa Chansela wa Ujerumani. Mara moja alichukua nafasi kuwakandamiza wapinzani wake na baada ya mwaka mmoja hata wale waliomwingiza madarakani.

Baada ya mwaka mmoja utawala wake ulisimama imara kabisa ilhali wapinzani wengi walikamatwa na kupelekwa katika makambi ya KZ.

Hitler alifuata siasa ya kujenga uchumi na kurudisha watu kazini akibahatika kwamba uchumi wa dunia ukapaa tena.

Hitler alifuta mapatano yote ya Ujerumani yaliyodai ukubwa wa jeshi lake kuwa watu 100,000 tu akajenga jeshi kubwa, akaanzisha utawala wa kidikteta wa "Dola la Tatu" akipiga marufuku vyama vya upinzani. Alitesa wapinzani wote na watu wa mbari alizochukia, hasa Wayahudi.

hitler2.jpg

Chuki dhidi ya Wayahudi aliionyesha kwa sheria mbalimbali zilizokuwa kali zaidi na zaidi. Idadi ya Wayahudi katika Ujerumani ilikuwa ndogo, takriban nusu milioni kati ya wakazi milioni 62. Kila Mjerumani akitaka kuajiriwa na serikali au kupata nafasi ya masomo alitakiwa kuorodhesha wazazi na mababu hadi kizazi cha pili.

Kwa njia hiyo Hitler alipanga Wajerumani wote katika vikundi vya "Waaria" (ambao hawana Wayahudi katika familia), "Wayahudi" (watu wenye asili ya Kiyahudi, hata kama wameshakuwa Wakristo tangu vizazi kadhaa au hawakufuata dini), "Wayahudi nusu" kama mzazi mmoja alikuwa Myahudi, "Wayahudi robo" kama mmoja kati ya mababu na mabibi wanne alikuwa Myahudi. Wayahudi na Wayahudi nusu walifukuzwa katika ajira ya serikali na walikataliwa kufanya kazi mbalimbali.

Sheria kuhusu "Aibu wa mbari" ilikataza ndoa kati ya "Waaria" na "Wayahudi"; "Wayahudi" waliondolewa uraia kamili.

Tokeo moja la siasa hiyo lilikuwa kuondoka kwa Wayahudi wengi kidogo katika Ujerumani; baada ya mashambulizi makali na mauaji mwaka 1938 mwelekeo huo uliongezeka.
Siasa yake mwaka 1939 ilisababisha Vita Kuu ya Pili ya Dunia.

Hitler alifuata siasa ya kukusanya Wajerumani wote wa Ulaya katika Dola la Ujerumani.
Mwaka 1938 alifaulu kuteka Austria na maeneo ya Wajerumani katika Ucheki bila upingamizi wa kimataifa.

Lakini aliposhambulia Poland tarehe 1 Septemba 1939 tendo hili lilikuwa mwanzo wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia kwa sababu Uingereza na Ufaransa walisimama imara kwa mikataba ya kusaidiana na Poland.

Wakati wa vita Hitler alichukua mwenyewe uongozi mkuu wa jeshi. Mwanzoni alifaulu hata dhidi ya ushauri ya majenerali wake, hasa wakati wa vita dhidi ya Poland na Ufaransa. Lakini maazimio yake ya 1941 ya kushambulia Urusi na kutangaza hali ya vita dhidi ya Marekani yalikuwa mwanzo wa mwisho wake. Nguvu ya kiuchumi wa Ujerumani haikutosha kushindana na dunia yote.

Wakati wa vita aliamuru uuaji wa Wayahudi wote wa Ulaya, na inakadiriwa alifaulu kuwaua takriban milioni sita (2/3 ya Wayahudi wote wa Ulaya) pamoja na watu mbalimbali kama Wasinti (kati ya 200,000 na 1,500,000).

Hasa alipoona ya kwamba vita dhidi ya Urusi haikufaulu haraka jinsi alivyotegemea aliamua kumaliza jambo lililosababisha chuki yake hasa. Azimio la "usuluhisho wa mwisho wa suala la Kiyahudi" lilichukuliwa mwisho wa mwaka 1941 na kutangazwa mbele ya viongozi wachache mnamo Januari 1942 katika Mkutano wa Wannsee.

Baadaye siasa ya kuwatenda Wayahudi vibaya na kuwaua katika maeneo fulani ilibadilishwa kulenga Wayahudi wote katika nchi zote zilizokuwa chini ya athira ya Ujerumani au kutekwa na jeshi lake. Hadi mwisho wa vita Wayahudi walikusanywa kutoka kote Ulaya na kupelekwa kwa reli hadi makambi ya mauti.

Gazeti la Marekani "Stars and Stripes" la tarehe 2 Mei 1945 latangaza kifo cha Hitler.
Maafisa wa jeshi ya Ujerumani walipanga mara kadhaa kumwua Hitler. Tarehe 20 Julai 1944 alijeruhiwa na bomu ya Stauffenberg lakini hakuuawa.

Mwishoni mwa vita Hitler alikaa Berlin hadi jeshi la Kirusi lilipokuwa limeshaingia mjini.

Tarehe 30 Aprili alijiua kwa sumu pamoja na mpenzi wake Eva Braun (alimwoa masaa tu kabla ya kujiua) na mbwa wake mpendwa "Blondi". Maiti zilichomwa kwa petroli lakini zilitambuliwa na Warusi kutokana na meno yake.
 
Habari members wote wa hili jukwaa! kwanza kabisa niungane na wapenda maendeleo na mabadiliko ya kweli na wote waliokumbwa na mshtuko wa ghafla baada ya wanaharakati mashuhuri Dr.W.P.Slaa na mwenzake Prof. Lipumba kustaafu siasa na nyazifa zao ktk vyama vyao kwa ghafla mno na bila kutarajiwa hasa wakati tunapoelekea uchaguzi mkuu ambao una kila aina ya hamasa toka kwa wapiga kura hasa vijana.

Kilicholeta zaidi gumzo ni kitendo cha Dr.Slaa kutumia zaidi muda mwingi siku ya mkutano wake na vyombo vya habari kumshambulia mgombea mmoja tu wa urais ndugu Edward Lowasa kama ni fisadi na baadhi ya makada waliotoka ccm na kuhamia cdm mf. ndugu Sumaye kwamba nao sio wasafi huku akishindwa kutoa maoni yake kuhusu wagombea wengine wa kiti hicho cha urais kama wanafaa au la.

Tunafahamu kilichotokea baadae ambapo wapenda mabadiliko wengi wamemuona dr.slaa kama msaliti,mbinafsi,mtu anayejiona n mtakatifu kuliko wengine na mtu mwenye chuki hasa baada ya chama chake cha cdm kumpokea Lowasa na kuwa mgombea wao kupitia mwamvuli wa ukawa ingawa kwa upande wa pili dr. ameonekana shujaa kwa maana huenda akafifisha nguvu ya upinzani! Sasa tuje kwenye mda.

Adolf Hitler ni mjerumani aliyezaliwa na kukulia nchi jirani na ujerumani(Austria) mwaka 1889.Jamaa alipokua mdogo alipata bahati mbaya ya kupoteza wazazi wake wote wawili hivyo ndoto zake za kusoma zikafutika.Aliishi maisha ya uchokoraa hadi vita ya 1 ya dunia ilipoanza mwaka 1914 ambapo alivuka mpaka na kujiunga na jeshi la ujerumani.Baada ya vita ujerumani iliyokua nchi kubwa duniani tangu ikamilishe muungano wake mwaka 1871 ilipoitandika Ufaransa ktk vita ya Franco-Prussian wa 1870/1871, uchumi wa ujerumani ulivurugika! nchi ilikumbwa na matatizo lukuki mf. ukosefu mkubwa ajira,umaskini wa kutupwa, mfumuko wa bei na kushuka kwa thamani ya pesa yao ( deutchemark) kwa kiwango cha ajabu!

Serikali ya jamhuri iliyokuwepo wakati huo (Weimar Republic) ikashindwa kabisa kutatua matatizo yaliyokuwa yanawakabili wajerumani walio wengi.Hivyo alipoibuka Hitler mtu ambaye hakumaliza hata shule, aliyekua rais wa ujerumani wakati huo Paul von Hindenburg alimuomba Hitler awe chancellor (waziri mkuu mtendaji) wa ujerumani baada ya chama chake cha kinazi kupata ushindi wa viti 229 kuwakilisha bunge la ujerumani(Reichstag) ktk uchaguzi wa mwaka 1932. Inafahamika pia baadae Hitler aliigeuza ujerumani kuwa nchi ya kidikteta hadi aliposhindwa na majeshi ya washirika mwaka 1945.

Lengo la historia hii fupi nini? Uchaguzi wa mwaka huu sio wa kuupuuza na kuutabiria hasa kwa chama tawala! Ni tofauti kabisa na ule wa 1995, 2000, 2005 na ule wa 2010! Chama tawala hakina budi kujipanga hasa ktk kutoa sera na mikakati ya jinsi ya kuondoa kero zinazowakabili watanzania bada ya kuendelea kutoa ahadi! Watanzania kwa sasa wengi wana elimu ya uraia hivyo wanajua haki zao.

Usiombee ukakutana na watu ambao wanasema ni bora wachague JIWE! kuliko kuchagua chama flani! hii inaweza ikasababisha yale wajerumani kumchagua ili awaondolee kero zao badala ya wale wanaotoa ahadi zisizotekelezeka huku wananchi wengi wakizidi kuwa maskini halafu wachache wakiitafuna keki ya Taifa wakiwa na marafiki zao, watoto wao na ndugu zao. Mungu ibariki Tanzania na tuombee uchaguzi wa mwaka huu 2015 uwe huru, wa haki na amani! Ameen!
 
Jifunze kuweka aya basi
halafu Hitler ni Magufuli au Lowassa?
 
Kama akili yako the boos iko sawa umeelewa acha kushikiwa akili
 
Kwanza historia hujui sijui umekurupuka tu,, jifunze kuchunguza kwanza, historia kabla ya kuandika,,

Kukukosoa tu Adolf Hitler baada ya kufiwa na wazazi wake nchini Austria alilelewa na mjomba wake, kijijini akawa anamsaidia mjomba wake kazi ya kilimo, mpaka alipokwenda kujiunga na jeshi la ujerumani wakati Wa vita kuu ya kwanza 1914 , Hivyo Adolf hittler hakuwahi kuishi mitaani kama chokoraa huo ni uzushi na upotofu wa historia,
 
mbona hujasema Hitler alifanya kazi ya shoe shiner na painting halafu Kule vienner alijifunza extreme nationalism na antisemitism kwa Karl lueger? Magufuri undo kama Hitler though Hitler was a real man.hivi mbona Chato inaongoza kwa mauaji ya albino
 
Kwanza historia hujui sijui umekurupuka tu,, jifunze kuchunguza kwanza, historia kabla ya kuandika,,

Kukukosoa tu Adolf Hitler baada ya kufiwa na wazazi wake nchini Austria alilelewa na mjomba wake, kijijini akawa anamsaidia mjomba wake kazi ya kilimo, mpaka alipokwenda kujiunga na jeshi la ujerumani wakati Wa vita kuu ya kwanza 1914 , Hivyo Adolf hittler hakuwahi kuishi mitaani kama chokoraa huo ni uzushi na upotofu wa historia,

''The death of Hitler's father in january 1903 changed everything, the absence of a dominant father figure altered Hitler's position in the family.
He spent much of his time playing and dreaming, did poorly in his studies,and left school in 1905.
His mother died in 1908, in reality, when he had exhausted his inherited funds; Hitler,unwilling to take a job, he ended up in a homeless shelter he mostly wandered about the city of Vienna,admiring its public buildings and frequently attending operas where he became a street boy''
Mwisho wa kunukuu!! Hakuna aliyekuwepo wakati huo hivyo hakuna sababu ya kunitolea maneno makali!
Isitoshe lengo la hii mada ni kujaribu tu kuoanisha sababu zilizowafanya wajerumani kumchagua mtu kama Hitler ili tu awaletee mabadiliko wala si kuonyesha ufahari wa kuijua historia!
Na nimetoa angalizo kwa chama tawala waje zaidi na mikakati thabiti na sera nzuri za kuwapelela watanzania mbele zaidi kimaendeleo badala ya kuendelea kutoa ahadi maana baadhi wamekata tamaa na wapo tayari kuchagua mabadiliko! Sorry kama hukunielewa.
 
mbona hujasema Hitler alifanya kazi ya shoe shiner na painting halafu Kule vienner alijifunza extreme nationalism na antisemitism kwa Karl lueger? Magufuri undo kama Hitler though Hitler was a real man.hivi mbona Chato inaongoza kwa mauaji ya albino

Upo correct! ishu ni kwamba niliweka wazi tangu awali ya kuwa ningeilezea kwa ufupi historia ya huyo jamaa kwa kuwa natambua ni ndefu pia nafahamu kuna watu wanaijua zaidi yangu.
Lengo langu lilikua ni kuwakumbusha tu wadau wa siasa ya kuwa uchaguzi wa mwaka si kama wa miaka ya nyuma kutokana na kundi kubwa la watu kutaka mabadiliko na wengine kukiri wapo tayari kuchagua jiwe na si chama fulani. Ila nashukuru kwa mchango wako wa mawazo.
 
Upo correct! ishu ni kwamba niliweka wazi tangu awali ya kuwa ningeilezea kwa ufupi historia ya huyo jamaa kwa kuwa natambua ni ndefu pia nafahamu kuna watu wanaijua zaidi yangu.
Lengo langu lilikua ni kuwakumbusha tu wadau wa siasa ya kuwa uchaguzi wa mwaka si kama wa miaka ya nyuma kutokana na kundi kubwa la watu kutaka mabadiliko na wengine kukiri wapo tayari kuchagua jiwe na si chama fulani. Ila nashukuru kwa mchango wako wa mawazo.

I salute mkuu,umeonesha umeelimikaassa
 
hakuwahi kutokea kiongozi imara kama hitler aliujenga uchumi wa ujeruman kuwa imara kwa miaka michache sana

Mwaga dondoo mkuu, binafsi nikua na kiu sana ya kutaka kufaham zaidi kuhusu huyu jamaa alie thubutu kuitikisa dunia
 
Alikua ni katili ambae hajawahi kutokea au pengine hatotokea hata Firauni hakua kama huyu Hitler.

Aliendeshwa na visasi na chuki na uchu wa kuitawala dunia kwa udiketa.
 
Last edited:
Binadam mwenye roho mbaya kama huyu jamaa hatakaa atokee!
 
There is a bunch of ruthless dictators in history even Hitler is just a Kindergarten baby.
On top of the food chain we have Iosif Stalin or Joseph Stalin as some of you may call him.
Just below Stalin we have the Red Bandit Chairman Mao Tse Tung.
Then there is Pol Pot of Cambodia.

The only difference they have is that Hitler was the Orchestra Master of The Second World War.
 
There is a bunch of ruthless dictators in history even Hitler is just a Kindergarten baby.
On top of the food chain we have Iosif Stalin or Joseph Stalin as some of you may call him.
Just below Stalin we have the Red Bandit Chairman Mao Tse Tung.
Then there is Pol Pot of Cambodia.

The only difference they have is that Hitler was the Orchestra Master of The Second World War.
If you can state the difference between them it's much better to stop calling him(Hitler) a kindergarten
 
wajerumani wenyewe wanampenda kisirisiri japo hawawezi kusema wazi..alikuwa mbaguzi wakati mwingine alipofikiria waafrica alisema angeona hilo shimo wanakotokea watu weusi angeliziba wafe wote
 
Back
Top Bottom