Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Kenya, Tanzania na Uganda zilikuwa zikishirikiana tangu karne ya 20. Bandari ya Mombasa ilifanya Kenya na Uganda kuungana tangia 1917, ambapo nchi iliyokuwa Tanganyika kipind hicho ilijiunga na muungano huu mwaka 1927, ilifuatia East African High Commission (EAHC) kuanzia 1948 mpaka 1961, The East African Common Services Organisation (EACSO) kuanzia 1967 na 1967 mpaka 1977 kulikuwa na East African Community.
Shughuli za serikali ya kikoloni ya Mwingereza iliendesha shughuli zake Kenya, Uingereza pia ilikuwa mdhamini wa Uganda (Uganda ilikuwa kwenye vita baina ya Wakatoliki, Waislam na Waprotestant kuanzia 1885-1887, Uingereza ilisaidiana na kiongozi wa Kiprotestant kumaliza vita hivyo kwa makubaliano kuwa Uganda itakuwa na power of autonomy). Makubaliano ya mwingiliano wa maslahi kati ya nchi moja na nyingine ulianza kufikiwa mwaka na EACSO mwaka 1948, ambapo azimio lake lilikuwa kuwa na serikali ya pamoja kati ya nchi hizi tatu. Mipango hii haikwenda kama ilivyopangwa kwa kukosekana mfumo na mipango ya pamoja. Mwaka 1967, EACSO ilibadilika na kuwa EAC. Nia ya EAC ilikuwa kuweka nguvu za pamoja katika soko huria, bandari, na huduma nyingine za jamii na kuweza kuweka hali ya uchumi sawa katika eneo hili.
Mwaka 1977, EAC ilikufa baada ya miaka kumi. Sababu ya kifo ilikuwa ni pamoja na Kenya kutaka viti zaidi kuliko Uganda na Tanzania katika kikao cha maamuzi ya jumuia, kutoelewana hna diktekta wa Uganda Idi Amin pia kulipelekea mvunjiko huo, ambae alihoji kuwa Tanzania ikiwa mwanachama wa jumuia kwanini inapigania kumtoa madarakani kiongozi mmoja kati ya nchi za jumuia? Kutofautiana kwa siasa, wakati huo Tanzania ilifuata siasa za ujamaa na Kenya walifuata siasa za kibepari. Nchi hizi tatu zilivunja uhusiano uliodumu kwa takriban miaka 60. Kulikuwa na hasara nyingi katika mvunjiko huo kwani shughuli za uzalishaji na mawekezo yalikuwa makubwa, ingawa viongozi wa Kenya walifurahia mvunjiko huo kwa mvinyo.
Baadae, Rais Moi wa Kenya, Mwinyi wa Tanzania, na Museveni wa Uganda walitia sahihi makubaliano ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki mjini Arusha, Tanzania, hiyo ilikuwa 30 November 1993 uhusiano huu ulishirikisha nchi tatu. Uhusiano huo ulilenga kwenye maswala ya siasa, maswala ya jamii, maswala ya tamaduni, utafiti na tekinologia, usalama, na sheria.
Mkataba uwa ushirikiano wa East Africa ulikamilika 30 November 1999, na ilianza kufanya kazi rasmi 7 July, 2000, hii ikiwa miaka 23 baada ya jumuia kuvunjika jumuiya ya zamani na viungo vyake. Maswala ya kibiashar yalitiwa sahihi March 2004, na yalianza kutekelezwa 01 January 2005. Kenya, ni mfanyabiashara mkubwa wa kusafirisha bidhaa nchi za nje kati ya hawa watatu na iliendelea kulipia kodi katika bidhaa zilizoingia katika nchi nyingine mpaka 2010. Kuna mfumo mmoja unaoongelea bidhaa zinazoingizwa kutoka nchi nyingine katika jumuia.
Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) inamaswala yanayoshirikisha serikali ya pamoja na inaundwa na nchi tano ambazo ziko kwenye maziwa makubwa yalimo Afrika Mashariki, nchi hizo ni Burundi, Kenya, Rwanda, Tanzania na Uganda. Sudan ya Kusini ilisaini mkataba wa kujinga na umoja huo mwezi April 2016, na itakuwa mwanachama kama itakubali matakwa ya umoja huo. Mwenyekiti wa umoja huo kwa sasa ni rais John Pombe Magufuli. Mwaka 2008 baada ya mazungumzo pamoja na Southern African Development Community (SADC) na the Common Market for Eastern and Southern Africa (COMESA), EAC ilikubali kwamba kuongezeka kwa soko huria miongoni mwa nchi wanachama ni muhimu kwa nchi hizi tatu wananchama. EAC ni muhimu sana katika uchumi wa nchi za Afrika.
Jumuiya ya Afrika Mashariki ni muhimu kwa uanzishaji wa Shirikisho la Afrika Mashariki ambayo imejadiliwa na wanachama wake. Katika shirikisho hilo, wanachama watakuwa huru kutembea au kufanya kazi kati nchi moja kwenda nyingine bila kuhitaji vibali. Mwaka 2010, shirikisho hilo liliazimia kuwa na pesa ya pamoja na baadae kuwa na mji mkuu wa pamoja. Mwaka 2013 walitia sahihi mkataba wa mipango ya pesa katika kipindi cha miaka 10.