Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
HISTORIA YA BI. TITI KATIKA KITABU CHA ABDUL SYKES 1955
Mikutano ya TANU ya siku za mwanzo ilikuwa ikifanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja mbele ya Princess Hotel.
Kwenye jukwaa lililojengwa kwa miti walikuwa wakikaa wale viongozi wa mstari wa mbele ndani ya TANU - Nyerere rais wa TANU, Sheikh Suleiman Takadir, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU, Bibi Titi Mohamed, John Rupia na Clement Mtamila.
Sahani ya santuri ilikuwa ikipigwa katika gramafoni kupitia kipaaza sauti.
Mwimbo uliokuwa ukipigwa ulikuwa wa Frank Humplink. Frank alikuwa kijana wa Kichagga kutoka Moshi.
Baba yake alikuwa Mzungu. Humplink alikuwa mwimbaji na mpiga gitaa maarufu sana wakati ule akipiga muziki wake na dada zake wawili Maria na Regina Humplink.
Wimbo uliopendwa sana na TANU na ndiyo uliokuwa ukipigwa katika mikutano yake yote na uliosisimua wananchi ulikuwa na mashairi yafuatayo, ‘’Uganda nayo iende, Tanganyika ikichangamka, Kenya na Nyasa zitaumana.’’
Mwimbo huu ulikuwa na ujumbe wa kisiasa kwa Waafrika wa Tanganyika.
Ujumbe katika wimbo huo ulikuwa kuwa, Tanganyika itakapoamka, kutakuwa vilevile na mapambano nchini Uganda, Kenya na Nyasaland.
Wimbo huu ulikuwa ukivuma toka kwenye vipaza sauti mfululizo kabla ya mkutano huku watu wakikusanyika viwanjani.
Haikupita muda mrefu serikali ya kikoloni ilipata maana halisi ya wimbo huo.
Mara moja mwimbo huo ukapigwa marufuku na serikali.
Serikali ya kikoloni iliamuru kwamba mashairi ya wimbo huo yalikuwa watu kuasi.
Lakini kabla ya wimbo huo kupigwa marufuku ulipendwa sana na ulikuwa ukiombwa na wasikilizaji na kupigwa katika kituo cha radio Sauti ya Dar es Salaam.
Baada ya amri ya serikali kituo hicho kiliacha kupiga wimbo huo.
Huenda huu ulikuwa wimbo wa kwanza kupigwa marufuku katika historia ya utangazaji Tanganyika.
Kwa muda mrefu sana wimbo huu ulikuwa kama wimbo rasmi wa TANU.
Inaelekea uzalendo na shauku ya uhuru ndiyo vitu vilivyomtia hamasa Humplink hata akatunga na kuuimba wimbo huo.
Picha ya kwanza ni Bi. Titi Mohamed kama alivyokuwa mwaka wa 1955 mshichana mdogo wa miaka 29.
Picha ya pili kulia ni Clement Mohamed Mtamila, Julius Nyerere, Maria Nyerere na Zuberi Mtemvu wako juu ya jukwaa.
Picha ya chini ni kituo cha radio Sauti ya Dar es Salaam.