Kanungila Karim
JF-Expert Member
- Apr 29, 2016
- 20,743
- 25,564
SEHEMU YA KWANZA
KWA UFUPI TU:Katika taaluma ya theolojia duniani wanatambua uwepo wa dini ya hindu. Kihistoria dini hii ya hindu ilianzia kuchipuka mnamo kwenye miaka ya 500KK-300BK.
Dini hii kwa mara ya kwanza ilipata kuchipukia kwenye maeneo ya Bonde la Indus(sehemu ambayo ustaharabu kwa watu wa bara hilo ulipoanzia), na inasemekekana hata neno Hindu ndipo lilianzia huko. Asilimia kubwa waumini wa kwanza walikuwa Wahindi waliopata kuishi kwenye maeneo hayo ya bonde la Indus, ambapo kulikuwa na mito ambayo ndio iliyosababishwa ustaharabu kwa Wahindi waliopata kuishi huko. Hakika katika historia ya Afrika mashariki tunatambua sana uwepo wa wahindi. Hii ina maana kuwa ujio wa Wahindi Afrika mashariki kulileta mabadiliko makubwa sana. Kwani Wahindi hao walikuja na utamaduni wao ambao aidha ulipendwa au haukupenda na watu wa waafrika mashariki. Ukweli ni kwamba sio kila sehemu au nchi Wahindi hawa walipata kufika. Hivyo tunapozungumzia ujio wa dini ya hindu Afrika mashariki tunaangalia maeneo kama Zanzibar, Kenya na Uganda. Maeneo yaliorodheshwa hapo ndio tutakayo anagalia namna dini ya Hindu ilifika na kukua kwake.
DINI YA HINDU KISIWANI ZANZIBAR. Historia inafafanua kuwa, ujio wa waarabu wa awamu ya pili ulilenga mabadiliko makubwa sana ya uchumi. Mabadiliko hayo ya uchumi yalileta mabadiliko mpaka kwenye masuala ya kijamii, hasa ukuaji wa dini ya Uislamu na Hindu. Kwa hakika ujio wa wafanya biashara wa kiarabu ulisababisha ujio wa Wahindi kisiwani Zanzibar. Inafafanuliwa kuwa mara baada ya Said Sayyid kuhamisha makazi yake kutoka Mascat, Oman na kuja kisiwani Zanzibar mnamo miaka ya 1840, kwa lengo la kukuza baishara.Ukweli ni kwamba alifanya mabadiliko makubwa sana. Na kutokana na wakati huo harakati za kupinga biashara ya utumwa zilishaanza, kwa Said Sayyid ilikuwa changamoto kubwa sana. Hivyo aliamua kufanya mabadiliko makubwa sana katika mfumo wa biashara. Na kutokana na idadi ya wafanyakazi wa kiarabu kuwa ndogo, Sayyid Said aliamua kualika Wahindi kwa lengo la kufanya baishara. Wapo Wahindi ambao walikuwa wafanyakazi kwenye mashamba na viwanda vya sultan Sayyid Said, na wapo Wahindi ambao walianzisha maduka yao wenyewe. Hivyo ujio wa wahindi hao ulifanya maendeleo ya biashara kukuwa kwa kiasi kikubwa.
Inaendelea
Sent using Jamii Forums mobile app