Historia ya Gen. Tito Okello Lutwa wa Uganda

Historia ya Gen. Tito Okello Lutwa wa Uganda

Echolima

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2007
Posts
3,824
Reaction score
2,079
Gen.Tito Okello Lutwa alizaliwa katika kijiji cha Nam Okora wilaya ya Kitgum wakati wa vita vya kwanza vya Dunia mwaka 1914,Kuhusu elimu yake mengi hayajulikani mengi hata hivyo alijiunga na Kings African Rifles(KAR)May 16,1940 kama ilivyokuwa kwa Idd-Amin naye alipigana vita vya Mau-Mau huko Kenya wakiwa upande wa waingereza mwaka 1957.

Gen.Tito Okello Lutwa alijiunga na Jeshi la Uganda na alipanda cheo kufikia Lieutenant mwaka 1962 na alifikia kuwa Colonel mwaka 1968.Wakati Amin anampindua Obote mwaka 1971 Gen.Tito Okello Lutwa alikimbilia Tanzania na alikaa sana Dar-es-salaam lakini pia alishawahi kukaa Nachingwea,Morogoro na Masange Tabora.

Mwaka 1978 wakati wa vita vya kumng`oa Idd Amin Gen Tito Okello Lutwa aliongoza kikosi maalumu(Special-Force)kikosi ambacho mimi mwenyewe nilikuwemo tulipigana bega kwa bega na waganda hao mpaka kung`oa Idd Amin madarakani mwaka 1979.

Mwaka huo huo 1979 baada ya Amin kuondolewa alikuwa sehemu ya Tume ya kijeshi,na baadaye 1980 alikuwa mkuu wa Majeshi wakati huo huo akiwa kwenye Tume ya kijeshi.Mwaka 1984 Alipandishwa cheo na kuwa Lieutenant General.

Gen.Tito Okello Lutwa alipitia magumu sana kipindi hicho maana kulikuwa na mambo mabaya sana jeshini Ukabila ulikuwa umetawala sana kulikuwa na vita kati ya makabila ya Acholi na Langi ilimuwia ngumu sana hata katika uteuzi wa maafisa wa jeshi mfano alimteua Bri.Smith Opon Acak toka kabila la Langi kuziba pengo la Maj.Gen.David Oyite-Ojok uteuzi huo ulipingwa sana na wanajeshi toka kabila la Acholi ambao wao walitaka mtu kutoka kabila lao Brig.Olara Okello ambaye alikuwa na uzoefu katika nafasi hiyo

Mwaka 1984 vita na waasi wa NRA alikuwa ameongeza mashambulizi yao kwa serikali hii pia iliezesha jeshi la taifa kugawanyika vipande viwili uapande mwingine ukiunga mkono Acholi na mwingine Langi kabila la Obote na Oyite Ojok.

Baada ya migogoro isiyokwisha ndani ya Jeshi la taifa UNLA na mapigano makali yaliyokuwa yakiongozwa na NRA chini ya Mseven Gen.Tito Okello aliamua kumpindua Rais Milton Obote July 25-27,1985 na Obote kukimbilia Kenya ka nia ya Barabara na kaenda uhamishoni Zambia ambako alifariki October 2005.

Baada ya mapinduzi hayo Gen.Tito Okello Lutwa alitangaza kuwa Uganda itatawaliwa na Baraza la kijeshi nay eye akiwemo kwa miezi 12 kabla ya Uchaguzi kufanyika.hata Gen.Okello alijaribu kuliunganisha jeshi ambalo tayari lilikua vipande vipande alijaribu kuunda serikali ya Mseto iliyojumlisha vyama vya Federal Democratic movement,Uganda National Rescue Front,Uganda Freedom Movement na NRA iliyokuwa inaongozwa na Yoweri Kaguta Mseven,Hata hivyo aligundua janja ya nyani aliyokuwa anataka kucheza Gen.Tito Okello na akakataa serikali hiyo na kuendelea na mapambano dhidi ya majeshi ya serikali UNLA

Yoweri Kaguta Mseven aliweka masharti magumu ili kukwamisha mazungumzo ya Amani yaliyokuwa yanaendelea huko Nairobi chini ya Rais Daniel Arap Moi wakati huo vikosi vyake vya NRA vilizidi kusonga mbele katika miji ya karibu na Kampala Barabara ya Masaka,Mubende,Mbarara na Katonga zote zilifungwa na kusababisha usalama katika maeneo yote kuwa hatarini Askari alianza uporaji na utekaji wa magari na vituo vya Mafuta,Maskini Gen.Okello hata hakumaliza kipindi alichoweka ili uchaguzi ufanyika na akapinduliwa January 26,1986 na alikimbilia uhamishoni hatimaye June 3,1996 alifariki akiwa na umri wa miaka 82,na mabaki ya mwili wake yalirudishwa Uganda na kuzikwa nyumbani huko wilaya ya Kitgum katika mazishi yake Rais Yoweri Kaguta Mseven alimtaja kuwa alikuwa mtu mkuu aliyelitumikia taifa lake na atakumbukwa kwa juhudi zake za kuleta Amani Uganda.

January 2010 wakati wa kumbukumbu ya vita vya Kagera alitunukiwa nishani ya Kagera National Medal Kwa heshima yake kwa kupigana vita kwenye miaka ya 1970-1979 dhidi ya Nduli Idd Amin.
 
Asante kwa Madini naomba pia ukiweza ulete ya Gen Oyite Ojok
 
Back
Top Bottom