Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
MUASISI WA TANU TANGA: HAMISI HERI AYEMBA
Tanga iliibuka mwaka 1955 na kukabiliana na serikali ya kikoloni kupitia juhudi binafsi za kikundi cha wafanyabiashara wadogo wadogo katika soko la Ngamiani.
Kikundi hiki kiliongozwa na kijana Peter Mhando, katibu wa zamani wa kile kikundi cha majadiliano cha wasomi wa Kibondei.
Akikiongoza kikundi hiki ambacho kilikuwa alikuwa baharia mstaafu, Hamis Heri Ayemba.
Hamis Heri alikuwa Mmanyema kutoka kabila la Wakusu kutoka Belgian Congo.
Peter Mhando alikuwa akifanya kazi kama mhandisi katia Noran Industries- wanunuzi wa nazi na watengenezaji sabuni pale Tanga.
Hamisi Heri alikuwa na umri wa katikati na katika ujana wake alikuwa baharia na alipata kusafiri chombo kimoja na Abeid Amani Karume, ambae baadae alikuja kuwa rais wa Zanzibar.
Baada ya Vita Kuu ya Pili, Hamisi Heri alirudi kwao Tanga ili aanze biashara.
Hamisi Heri alikuwa mtu aliyejikuza na kujielimisha mwenyewe; na alikuwa amesafiri sana. Hamisi Heri alizungumza vizuri sana Kiingereza na Kiarabu.
Katika miaka yake ya mwanzo katika biashara, alikuwa dalali.
Hamisi Heri aliwashangaza wateja wake kwa uhodari wake wa lugha mbali mbali, akinadi bei kwa Kihindi au Kiarabu, kutegemea utaifa wa watu waliokuwepo pale mnadani.
Harakati za kudai uhuru zilipoanza Heri alikuwa ametajirika na mmoja wa Waafrika wenye kuheshimiwa sana mjini Tanga.
Peter Mhando alipochoshwa na kile kikundi cha majadiliano, alijiunga na Hamisi Heri na kikundi cha wenyeji wana mji ambao walikuwa wakijitahidi sana kuunda tawi la TANU.
Wakati huo mwanasiasa mwenye uzoefu mkubwa kuliko wote mjini Tanga alikuwa Mwalimu Kihere.
Lakini siasa za mapambano baina ya ule uongozi wa TAA chini ya jamii ya Kiarabu na kikundi cha majadiliano zilimzuia kutoa mchango wowote wa maana.
Mwalimu Kihere alikuwa amehudhuria mikutano kadhaa ya African Association tangu mwaka 1946.
Wakati wa uongozi wa Abdulwahid Sykes alikuwa amedumisha uhusiano mkubwa sana baina yake yeye mwenyewe binafsi, Abdulwahid na Dossa Aziz.
Hii ilifanya vilevile adumishe mawasiliano ya karibu sana na makao makuu ya TAA.
Lakini kwa sababu ya mizozo katika siasa hapo Tanga, ule mkutano mkuu wa kuasisiwa TANU uliofanyika Dar es Salaam mwaka wa 1954 ulipita bila ya Tanga kupeleka mjumbe.
Kile kikundi cha wafanyabiashara wadogo wadogo katika soko la Ngamiani kiliitisha mkutano katika Ukumbi wa Tangamano tarehe 5 Septemba, 1955.
Waliohudhuria mkutano huo walikuwa Hamis Heri, Peter Mhando, Mohamed Kajembe,Tuwa Abdallah, Dhili Mgunya, Abdallah Rashid Sembe, Victor Mkello, Mohamed Sadik, Hassan, Peter Ramadhani Jembe na Ali Mohamed.
Peter Ramadhani tayari alikuwa mwanachama wa TANU huko Arusha na alikaribishwa mkutanoni ili waasisi wa TANU wanufaike kutokana na uzoefu wake.
Wasomi wa Makerere, uongozi wa TAA chini ya jamii ya Kiarabu na Mwalimu Kihere hawakuwepo kwenye mkutano huu muhimu.
Mkutano ulifunguliwa na Hamis Heri saa tisa adhuhuri na ulifungwa saa mbili baadae kwa uamuzi kuwa mkutano mwingine wa kuchagua viongozi wa chama ufanyike tarehe 23 Oktoba.
Mkutano uliamua vilevile kuwa juhudi zifanyike kupata waanachama wengi iwezekanavyo.
Kiasi kidogo cha fedha kilikusanywa na Harir Omari Siagi alipewa aende makao makuu ya TANU, Dar es Salaam kununua kadi 70 za TANU.
Tarehe 23 Oktoba, wanachama wa mwanzo wa TANU huko Tanga walikutana kuchagua uongozi wao chama.
Hamisi Heri alichaguliwa kuwa mwenyekiti na Peter Mhando katibu.
Jumla ya watu 45 walihudhuria mkutano huo na wakapewa kadi za TANU.
Mwalimu Kihere alihudhuria mkutano ule lakini hakuchaguliwa katika nafasi yoyote ya uongozi.
Kamati ya wanachama iliundwa kutokana na wale wanachama 11 waasisi waliokutana katika ule mkutano wa kwanza mwezi uliopita.
Kamati hiyo ilikuwa na wajumbe wafuatao: Abdallah Rashid Sembe, Mohamed Kajembe, Victor Mkello, Dhili Mgunya, Ali Mohamed, Abdallah Mohamed na Mohamed Sadik. Peter Mhando alijitolea nyumba yake kuwa ofisi ya kwanza ya tawi la TANU mjini Tanga.
Mara tu baada ya mkutano huu wazee wa Tanga wakiongozwa na Makoko Rashid, mwanachama wa zamani wa TAA walianza kufanya kampeni kwa ajili ya TANU.
Chama kilipata msukumo mwingine na kuongezeka nguvu wakati Sadik Ali Patwa Muasia tajiri alipoingia TANU.