Historia ya jamii za kale

Historia ya jamii za kale

dosho12

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2023
Posts
596
Reaction score
1,475
Wote tunajua kuwa binadamu aliumbwa na MUNGU na kutuma rangi, jamii na mataifa tofauti tofauti hii ni katika dini ya kiislamu, wakristo na wayahudi, wana sayansi wakaja na theory yao kwamba binadamu ametokana na nyani na akaanza ku develop kadri siku zinavyoenda ila kuna jamaa mmoja anaitwa Bill carson mwana historia ya jamii za kale na ana elimu ya neuroscience yeye ana amini kuna viumbe walio endelea walikuja duniani waliwakuta viumbe wakiishi walifika na kutaka kutawala na wakasaidia kutengeneza rangi ya ngozi zetu na jamii. Walikuwa viumbe wanne anawaita Anunakis walitaka kuwaongoza binadamu hivyo kila kiumbe alienda sehemu yake na ili waweze kuwatambua kama vile mfano una mifungo yako ili uzitambua utaziwekea brand au alama ili akipotea iwe vyepesi kuzitambua hivyo wao hao Annunaki walitupa rangi ya ngozi ili waweze kujua kuwa hawa watu ni wa nani na hawa wa nani walio afrika wakapewa rangi nyeusi wengine wakapewa nyeupe wengine blown na hivyo ndio ukuwa mwanzo wa asili na rangi ya ngozi zetu

Ushahidi wa hao viumbe anasema upo mfano pyramid zilizo jengwa Misri anasema kwa muda zilipo jengwa ni muda ambao anahisi binadamu alikuwa hajafika level hiyo ya maendeleo kwa sababa zimejengwa kwa ustadi na elimu kubwa na zinaendana na mzunguko wa jua na sayari za karibu na vipimo ambavyo ni vigumu kwa mtu aliye chini ya ardhi mpaka uwe juu zaidi ndio utaweza kupima pia kuna sehemu ukipama unapata spidi ya mwanga na ndani kuna michoro ambayo inauonyesha kama spaceship na vifaa vya kisasa na pyramid hizi zimesambaa sehemu nyingi ya dunia siyo Misri tu

Pia kuna historia ya makabila mbali mbali yakielezea walitembelewa na viumbe wasyivo vijua na, pia wana michoro ya vitu vinavyopaa angani, mfano kuna kabila moja lipo mali linaitwa” DOGON “ mwanasayansi mmoja alienda akakuta wana elimu ya nyota inaitwa sirius B ambapo Ilikuwa ni zamani hata nasa wao walikuwa hawajui kama kuna nyota hiyo wao wakisema ni elimu waliorithishwa na wazee wao toka vizazi na vizazi huku wakisema walipewa elimu hiyo na viumbe walitoka angani

Mabaki ya maandishi kutoka kwenye dini za wahindu pia zinaonyesha amichoro ya viumba wa waliotoka angan na matumizi ya vifaa vya kisasa i, ukienda mexico kabila la “MAYANI” pia wanahistoria ya viumbe walikuja angani na kuwasadia jamii hiyo kuna mmoja wanamuita “the feathered god” au “kulkul khan” ambao kampuni ya Marvel wanamtumia kwenye comics na movie zao kama kwenye Black panther wakanda forever

Mimi naona huenda viumbe wa zamani walikuwa wanaelimu na ujuzi mkubwa na kidini huenda MUNGU alikuwa akituma malaika wake kwenda kuwasaidia. We unaonaje unahisi jamaa anaweza akawa sahihi

Reference

View: https://youtu.be/V77_Rrnw_H0?si=us0t7K7CEm-kina7


View: https://youtu.be/livgMzeO-ZY?si=CU4hwdzr0uaNqMlj



View: https://youtu.be/JZLL3X6DC90?si=QHFJnESmevbjPAKm
 
Back
Top Bottom